Hapo kwa Macca kupiga DM badala ya Deep play marker ni kweli hapa Klopp anatudanganya sana na uzuri mpira ni mchezo wa wazi sana. Tunaona Macca anavyo struggle.
Kwa ishu ya kumtoa Tsimikas, nakubaliana na Klopp 100%. Kwa nini? Unahitaji goli kama sio magoli kwa timu kama Everton ambayo toka mpira unaanza kabla ya red card plan game ilikuwa ni Njooni mtushambulie siye twazuia nyuma huku, tukiwapokonya ni counter tu. Sasa baada ya red wakapata sababu ya kukaa nyuma 100%. Hapo inabidi kama kocha uongeze mashambulizi na kupunguza kujilinda, ndio akafanya akiwa na target ya kupata magoli na kuanza ku relax. Na sub pekee ilikuwa na Tsimikas.