King Ngwaba
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 3,117
- 6,897
◾Huu ndio muundo mpya na kamili ndani ya Liverpool kupelekea msimu ujao
▪️🇬🇧Michael Edward CEO
▪️🇳🇱Arne Slot Head Coach
▪️🇬🇧Richard Hughes Sporting Director
▪️🇬🇧Julian Ward Technique Director
▪️🇬🇧Mark Burchill Chief of Scouting
▪️🇵🇹Pedro Marques Director of Football Development
Huu ni muundo sahihi kwa Liverpool hasa ukizingatia malengo ya klabu kwa nyakati zijazo na hata ufanisi wa hilo jopo la watu tajwa hapo juu ni mkubwa na wamesha dhihirisha hilo katika ulimwengu wa mpira
FSG wana malengo yao kama wamiliki wa klabu kubwa kama Liverpool ndio maana waka amua kuteuwa watu sahihi ambao wataisukuma klabu kwa ushirikiano bila kuathiri uwekezaji wao kama wamiliki na kuendelea kuikuza thamani ya klabu kama walivyo fanya tangu walipo inunua Liverpool ikiwa na thamani ndogo na sasa kukuwa mara dufu.
Kocha Arne Slot 🇳🇱 atakuwa hana cha kulaumu kwakuwa ameandaliwa watu makini sana watakao mzunguka na kumrahisishia kazi yake, Watu wote wanao mzunguka watakuwa na umoja utakao mfanya kocha afikirie zaidi maendeleo ya timu kuliko jambo lingine.
Mashabiki wa Liverpool wanapaswa kutambua nyakati zina badilika na lazima zibadilike kwakuwa huwezi kuishi kwa njia moja miaka yote, huu ni wakati wa kusimama na FSG pamoja na waajiri wao walio waamini kuivusha Liverpool baada ya kipindi hiki cha Jurgen Klopp 🇩🇪 kufikia tamati
Naweza sema bado Liverpool itaendelea kuwa katika mikono salama na hakutokuwa na presha yoyote hii nikwa wale Liverpool dam dam achana na wale Liverpool makelele.
Muundo huu mpya utaendeleza yale yale ya kufanya biashara rafiki ndani ya klabu na kuzingatia misingi ya biashara ya mpira,kukuza, kununua na kupambania mataji, Kuvivaa viatu vya Jurgen Klopp 🇩🇪 ni kazi ngumu lakini tunapaswa kujua kila mpambanaji ana aina yake ya kubadili mbinu ya kushinda pambano
Binafsi kama Kop Dam Dam na amini sana muundo mpya wa Liverpool na nipo sambamba na FSG na watu wake.
Tulisha amka tayari kikubwa nikuwa makini tusilale tena wakati wa safari.
#Ynwa
Huo ni muundo sahihi lakini je hela ipo? Au ndiyo yaleyale tu sell to buy.