Hawezi kukuelewa, amechagua ujinga.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bro nakushauri nyamaza unatutia aibu hata sisi.
ELEWA HAYA:
- Goalkeeper: Ni mchezaji kama wachezaji wengine, linapokuja suala la offside sharia haitambui kitu kinachoitwa Goalkeeper bali inamtambua kuwa ni mchezaji kama wachezaji wengine.
VIPI MCHEZAJI ANAHESABIWA KUWA OFFSIDE?
- Ni pale awapo katika Half ya Pitch ya Wapinzani iwapo:-
1) Amebakisha mchezaji mmoja tu wa upinzani mbele yake! Si lazima mchezaji huyo awe Goalkeeper, hata kama Goalkeeper ametoka golini na akabakia Beki au Kiungo au Mshambuliaji pekee.
2) Mbele yake hakuna mchezaji hata mmoja wa upinzani, Mfano Timu nzima akiwemo na Goalkeeper wameenda kushambulia kwa kupigwa Corner then Mshambuliaji akawa ameshavuuka Half pitch ya Upinzani na ukapigwa mpira mrefu ukamfika akiwa peke yake mbele hakuna mchezaji wa upinzani yeyote.
VIPI MCHEZAJI ANAKUWA SI OFFSIDE?
√ Iwapo yupo Half Pitch ya Opponents wake lakini mbele yake kuna wachezaji kuanzia Wawili (au zaidi).
Hao Wachezaji Wawili wanaweza kuwa BEKI na KIPA.
Si lazima Kipa awepo, inawezekana Mabeki Wawili pale iwapo Kipa ametoka kwenda kujaza Kona.
NOTE:
Ni kosa kuamini kuwa Offside inahesabika kufa kwa kuwepo Beki mmoja! Pale hapahesabiki Beki, Bali panahesabika kuwa kuna wachezaji Wawili (Beki na Kipa).
Sent using Jamii Forums mobile app