Liverpool inaweza Ikakosa ubingwa endapo coronavirus vikiingia Uingereza

Liverpool kufungwa jana na Watford Nasikia ni kwa sababu ya kuogopa Korona
 
  • Calum Hudson Odoi winga wa Chelsea FC na kocha wa Arsenal - Mikel Arteta wakutwa wana virusi vya Corona (COVID-19)
  • Baadhi ya wachezaji wa Chelsea, Lampard na baadhi ya wasaidizi wake watengwa
  • Kocha wa Arsenal na baadhi ya wasaidizi wake pamoja na baadhi ya wachezaji wa Arsenal watengwa
  • EPL iko 50/50 kuendelea sijui contingency plan yao waliafiki nini?
  • Ni suala la muda tu serikali kupiga marufuku makusanyiko yote ikiwemo EPL
  • Sasa swali Liverpool watatangazwa bingwa kabla hajamaliza mechi au kufikisha points za kumfanya kuwa bingwa?
  • Mechi zote za La Liga zimeahirishwa angalau kwa wiki mbili baada ya baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wa basketball wanaoshirikiana maeneo ya mazoezi na wachezaji wa mpira wa miguu kukutwa na virusi na wote kutengwa
  • Mechi zote za Serie A zaahirishwa hadi April 3
  • Maoni yangu, hali ikizidi kuwa tete na inavyoelekea inazidi kuwa tete, kuna uwezekano ligi hizi zote zikasimamishwa na wala sio kuahirishwa
  • 1584069537273.png
 
  • View attachment 1386503
Mhhhhhhhh!!!! Tunakoelekea pressure na heart attack zitatumaliza kabla hata corona haijatukuta!
 
Ni heri Corona iingie Dunia nzima kuliko Liverpool kuwa bingwa 😎
Hili janga hatulitaki huku kwetu,bora Liverpool awe bingwa kuliko Corona isambae dunia nzima.
 
Inakuwa km ilivyokuwa kipindi cha vita ya dunia.KILA MTU ANABAKI NAFASI YAKE. Wa juu anakuwa bingwa...wa kushuka ana shuka...poleni wenye roho za nyau kwa liverpool

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mechi zote za EFL na EPL zahairishwa hadi April, 4
 
BREAKING NEWS
Serikali ya Uingereza imesema inafikiria kupitisha sheria ya kupiga marufuku mikusanyiko yote nchini humo ili kupunguza kasi ya maambukizi ya Korona
Baada ya kulaumiwa na nchi zingine na taasisi mbalimbali kama WHO kwamab serikali ya Uingereza haikuchukua hatua madhubuti ili kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson amesema serikali inafikiria kuchukua hatua ya kuvipiga marufuku makusanyiko yote wiki ijayo ili kupunguza kasi ya maambukizi

Plans are under way to ban mass gatherings in the UK from next week just days after the government faced criticism for not taking tougher action against the Covid-19 pandemic, despite other European countries introducing strict social distancing measures.

Emergency legislation bringing in stronger powers will be published next week and there could also be a move towards more people working from home, a Whitehall source told the PA.

This morning, a World Health Organisation spokesperson questioned the UK's plan to build up immunity within the population to fight coronavirus over a prolonged period, rather than introducing mass lockdowns.

Sources: SkySports muda mfupi uliopita pamoaj na WHO joins in criticism of UK's coronavirus 'herd immunity' plan as government accused of 'playing catch-up' - follow live

My Take
Hizi sio taarifa nzuri kabisa
Haya mashindano ya EPL, Serie A, La Liga, na ligi zote kub wa duniani ndio mwisho wake hapa angalau kwa msimu huu
Safari za ndege zimeshaanza kufutwa
Kuingiliana kijamii duniani hakutakuwepo tena sijui mapaka lini?
Tutegemee uchumi kudorora na tutarudi kule kwenye ujima ule wakati wa kuuziana vitu kwa kubadilishana
 
Hapa tatizo lipo kwenye viwanda kuendelea kuzalisha bidhaa, lkn kama vikizalisha bidhaa zitaendelea kusafirishwa tu

Liverpool is ‘likely’ to be awarded the 2019-20 Premier League title, with reports there are mounting fears it will be impossible to complete the season this summer.
The Telegraph reports there is “little opposition” from rival clubs for Jurgen Klopp’s side to be awarded the title, with Liverpool 25 points clear of second-placed Manchester City. As it stands, two more wins will hand the Reds the league.

English football has already suspended all fixtures until April 4, but the report suggests resuming play on that date - when experts believe coronavirus will be peaking - is extremely optimistic.
 
MAAMUZI MAGUMU!
HATMA YA UBINGWA WA LIVERPOOL KUPITIA MBINU HIZI.

LICHA ya kusimamisha Ligi Kuu England kwa wiki tatu hadi Aprili 3 mwaka huu, vichwa vinawauma mabosi wa bodi ya EPL, kutokana na kutakiwa kuja na majibu ya nini kitafanyika iwapo virusi vya Corona vitaendelea kuitesa nchi hiyo.
Hadi sasa hakuna jibu la moja kwa moja linalotolewa na mabosi hao ambao wanatarajiwa kufanya kikao cha dharura wiki hii, kuhusiana na nini kitafanyika ikiwa tatizo la Corona litadumu kwa muda mrefu maana Ligi Kuu England haina kanuni inayoeleza hatua gani zitachukuliwa iwapo ligi itavunjika.

Lakini, wachambuzi wa soka la England wamekuja na aina nne za uamuzi mgumu ambazo vigogo hao wanaweza kuchagua moja.

UAMUZI WA KWANZA:
Kuvunja Ligi
Huu ni uamuzi unaowakera zaidi mashabiki wa Liverpool waliokuwa wanaamini huu ni mwaka wao na baada ya mechi 29 msimu huu wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 25 mbele ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili na wanahitaji mechi mbili tu kutwaa ubingwa wao wa kwanza baada ya miaka 30.
Lakini, kwa mujibu wa uamuzi huu uliowekwa mezani na Makamu Mwenyekiti wa West Ham, Karren Brady, kwa upande wake anashauri ligi ivunjwe na kila kitu kianze upya kuwe hakuna bingwa wala timu ya kushuka daraja, hii ni nzuri kwa timu yake inayoshika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 27 na wastani mzuri wa mabao kulinganisha na timu zilizo chini ya mstari wa kushuka daraja.
Uamuzi huu unaiathiri zaidi Liverpool inayokaribia kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30, lakini pia uamuzi huu utaiathiri Leicester City ambayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

UAMUZI WA PILI:
Kumalizia MECHI
Huu ndiyo uamuzi ambao mabosi wa EPL, wanaona hauna utata kila timu na itapata inachostahili, kupitia uamuzi huu wanataka kusubiri na kumaliza ligi kivyovyote na hata kama tatizo la virusi vya Corona litachukua muda mrefu kiasi gani, lakini vikiisha tu ligi imaliziwe ndipo msimu mpya uanze.
Lakini, ili hili litokee lazima michuano ya Euro 2020 isifanyike ili kutoa nafasi kwa klabu kucheza mechi za ligi wakati wa kiangazi, maana kama michuano hiyo ikiwapo wachezaji watajiunga na timu zao za taifa na hawatapata nafasi ya kucheza soka katika ngazi ya klabu.

UAMUZI WA TATU:
Ligi kuisha hapa
Kama tatizo la Corona lisipomalizwa mapema basi mashabiki wengi wa Liverpool wanataka uamuzi huu ambao ni kumaliza ligi katika hatua hii na kuwapa ubingwa huku. Norwich City, Aston Villa and Bournemouth zikishushwa daraja.
Uamuzi huu unainufaisha zaidi Liverpool ambayo itapata ubingwa ambao inastahili, lakini unaziumiza timu nyingi, kuanzia zile zitakazoshushwa daraja wakati zikiwa na nafasi bado ya kupamba na kubaki Ligi Kuu hasa kutoka na ukweli kuwa tofauti kati ya timu ya 18 na ya 17 na 16 ni mabao tu.
Lakini pia timu ambazo zinapambana kutafuta nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester United, Wolves na Sheffield United zitaathiriwa na uamuzi huu kwa sababu bado zina nafasi ya kuingia nne bora kama ligi ikiendelea, lakini ikimalizwa hapa basi hawatashiriki michuano hiyo mwakani.

UAMUZI WA NNE:
Kuongeza idadi ya timu
Ili kuepusha kelele ya timu zitakazoshuka daraja na pia kuiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa ambao imeupigania sana msimu huu, basi Bodi ya Ligi inaweza kuamua hakuna kushusha timu daraja na kuipa ubingwa Liverpool.
Na ili kuzipa haki zile timu ambazo zimekuwa na msimu bora Ligi Daraja la Kwanza, timu za Leeds na West Brom zipewe nafasi ya kupanda daraja, hii itamaanisha kuwa msimu ujao utakuwa na timu 22 badala ya 20, huku kila timu ikifurahi, japokuwa zile za timu zinazowania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa zitalia lia tu.

Ndugu mwanamichezo nini maoni yako?

Hbr njema kwa ASTON VILLA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom