Liverpool mbona kulimwaga huko England ni dakika sifuri

Liverpool mbona kulimwaga huko England ni dakika sifuri

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
LEICESTER City wamekuwa kwenye kiwango bora kweli kweli msimu huu na kuwa wapinzani wapya wa Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Straika, Jamie Vardy yupo kwenye kiwango bora kabisa akiongoza vyema kwenye fowadi ya Leicester City, ambapo imekuwa ikigawa tu vichapo na sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, pointi nane nyuma ya vinara Liverpool.

Timu hiyo inayonolewa na Brendan Rodgers imejiweka kwenye nafasi nzuri pia ya kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, pointi 14 juu ya timu inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo, Manchester United.

Lakini, kwa kiwango chake na moto cha kugawa tozi kinaonekana kuwatisha Liverpool, ambapo kikosi hicho cha Jurgen Klopp kipo kwenye presha kubwa ya kushinda mechi zake ili kuwazuia Leicester City wasirudie maajabu yao ya msimu wa 2015/16 walipobeba ubingwa wa ligi hiyo.

Kama Leicester City watachukua ubingwa haitakuwa kitu cha kushangaza tena, jambo linalosubiriwa kama Liverpool watapoteza uongozi wao huo mkubwa wa pointi na kuwaachia wapinzani wao kubeba tena ubingwa mbele yao kwa ulaini kabisa.

Hata hivyo, suala la timu kupoteza uongozi wake wa pointi nyingi kwenye Ligi Kuu England si jambo la kwanza hasa kwa kipindi hiki ambapo, Liverpool inakabiliwa na mechi tano ngumu ndani ya muda mchache kitu ambacho kinanweza kubadili kila kitu.

Cheki hapa timu ambazo zilikuwa zikiongoza kwa pengo kubwa la pointi ikiziacha timu zinazowafuatia kwenye msimamo wa ligi, lakini zilishindwa kwenye kubeba ubingwa mwishoni mwa msimu kwenye Ligi Kuu England.

Norwich City 1992/93 – pointi 8
Baada ya kumaliza kwenye nafasi ya 18 katika Ligi ya Daraja la Kwanza msimu wa 1991/92, pointi tatu tu juu ya zile zilizoshuka daraja, hakuna ambaye alikuwa na imani kwamba Norwich City wangekwenda kuwa timu ya kushindania ubingwa katika msimu wa kwanza kabisa wa michuano ya Ligi Kuu England.

Lakini, timu hiyo iliyokuwa chini ya Mike Walker iliwaduwaza wengi kwa kiwango chao walichocheza na kuwafanya waongoze kwa pointi katika mechi 18.

Shida ni kwamba Norwich walishindwa kuendeleza makali yao hayo kwenye mzunguko wa pili wa ligi na matokeo yake walicheza kwa kiwanngo cha hovyo, wakichapwa mara mbili na Manchester United katika msimu huo na kuwafanya wapinzani wao hao kwenda kujibebea tu ubingwa kiulaini mwishoni mwa msimu.

Newcastle United 1995/96 – pointi 12
Hakuna anayeweza kusahau hili namna Manchester United ilivyopora ubingwa wa Ligi Kuu England kutoka kwenye mikono ya Newcastle United. Wababe hao wa St James’ Park walikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 12 na hapo kulikuwa na mechi zimebaki msimu kufika mwisho. Kwenye dirisha la Januari wakafanya usajili wa Faustino Asprilla kuja kuongeza nguvu na wengi waliamini hakuna ambacho kingeenda kuizuia Newcastle kwenda kuchukua ubingwa wa ligi.

Lakini, kabla mambo yalikuwa hovyo, wakichapwa mechi tano kati ya nane walizocheza kati ya FebruarI 21 na Aprili 8 na jambo hilo lilitibua zaidi kuwafanya Man United kusogea na kwenda kuchukua ubingwa wa ligi hiyo kibabe. Kitu kitabu zaidi, Man United walikwenda kuifunga Newcastle United 1-0 na hivyo kwenda kujichukua ubingwa.

Man United 1997/98 – pointi 11
Wababe wa Ligi Kuu England katika miaka ya 2000, Manchester United walifanya balaa la mwaka baada ya kulimwaga kwenye mchakamchaka wa ligi hiyo licha ya kuongoza kileleni kwa pengo la pointi 11. Man United walikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi hizo huku mechi zikiwa zimebaki tisa tu, lakini wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa kwa wakati huo, Arsenal walilikata pengo hilo la pointi na kwenda kuchukua ubingwa.

Arsenal walikuwa na mechi tatu mkononi, lakini Man United bado walikuwa mbele kwa pointi. Mechi yao iliyopigwa Old Trafford, Arsennal walikwenda kuichapa Man United 1-0 na hivyo kujisogeza pazuri zaidi na kufanikiwa kwenda kubeba ubingwa kibabe wakiwaacha Man United kwenye mshangao mkubwa wakijiuliza pengo lao la pointi 11 lilipokwenda.

Arsenal 2002/2003 – pointi 8
Kocha Sir Alex Ferguson na chama lake la Manchester United alipata nafasi ya kulipa kisasi dhidi ya Arsenal ya Arsene Wenger baada ya kulikata pengo la pointi nane hadi kufikia Machi na kwenda kubeba ubingwa.

Arsenal walikwenda kupoteza mechi dhidi ya Leeds United huku zikiwa mechi mbili zimebaki, matokeo ambayo yaliifanya Man United kubeba ubingwa huku timu hiyo ikijiokoa kwenye kushuka daraja.

Kitu matata kabisa ilichofanya Man United katika kulikata pengo hilo la pointi walishinda mechi zao 15 kati ya 18 za mwisho na kwenda kuchukua ubingwa wakiwa na pointi tano mbele.

Mashabiki wa Arsenal halikwenda kuwaumiza hilo kwa sababu msimu uliofuatia walikwenda kucheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi na kunyakua ubingwa.

Arsenal 2007/2008 – pointi 5
Arsenal walikuwa kwenye kiwango bora na kuonekana kama vile wanakwenda kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wa 2007/08 baada ya kuweka pengo la pointi tano kileleni. Licha ya kwamba ilitoka kuwapiga bei mastaa wake muhimu kama Thierry Henry, lakini hilo halikuonekana kuwakwaza na Arsenal walionekana kuwa moto, ambapo waliweka pengo la pointi tano kileleni huku wakiwa wamepoteza mechi moja tu kwa msimu wote.

Lakini, mambo yalikwenda kutibuka kwenye mechi yao ya ugenini kwa Birmingham iliyopigwa Februari, ambapo Eduardo Silva alivunjika na kuishia kupata sare. Baada ya hapo waliendelea tena kuboronga hadi kufikia Aprili walikuwa wamewashawaruhusu wapinzani wao Chelsea na Manchester Unitd wote kuwavuka. Matokeo yake msimu ulipomalizika, Arsenal walijikuta wakiwa kwenye nafasi ya tatu.

Man United 2011/12 – pointi 8
Manchester United ilionekana kama vile inakwenda kushinda taji lake la tano la Ligi Kuu England ndani ya misimu sita wakati walipopata ushindi wa 2-0 dhidi ya QPR na hivyo, kuweka pengo la pointi nane dhidi ya Manchester City huku mechi nane zilikuwa zimebaki.
Man City walishindwa kupata ushindi dhidi ya Stoke, Sunderland na Arsenal na kufanya kutokea kwa pengo hilo kubwa la pointi kileleni.

Lakini, Man United ilikwenda kuchapwa 1-0 na Wigan iliyokuwa ikipambana isishuke daraja na hapo ikawafanya Man City kupunguza pengo.
Man United wakaenda kupata sare pia ya 4-4 dhidi ya Everton uwanjani Old Trafford na kisha kwenda kuchapwa 1-0 na Man City uwanjani Etihad na hapo ikawa kila kitu kimetibuka, ambapo mechi ya mwisho, Man City waliichapa QPR na kubeba ubingwa licha ya kwamba Man United waliipiga Sunderland.

Liverpool 2013/14 – pointi 3
Hili halikuwa pengo kubwa zaidi la pointi, lakini ndio hivyo Liverpool ilitibua tena na kukosa ubingwa dakika za mwisho. Kikosi hicho kikiwa chini ya Brendan Rodgers kilibakiza mechi chache kubeba ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya miaka 24. Walikuwa wanaongoza kwa pointi tatu dhidi ya Manchester City na kulikuwa mechi tatu tu zimebaki kumaliza msimu.

Lakini, Liverpool wakalimwaga, Steven Gerrard alianguka kwenye mechi dhidi ya Chelsea na kusababisha bao katika kipigo cha 2-0 kabla ya kwenda kufanya hovyo kwenye mechi ya Crystal Palace, ambayo ilimfanya Luis Suarez kumwaga machozi. Timu hiyo ilipoteza uongozi wake wa mabao matatu ndani ya dakika 11 za mwisho kwenye mchezo huo wa Palace na hivyo, kuwaachia Man City ubingwa kiulaini. Mashabiki wa Liverpool bado hawaamini kilichotokea hadi sasa.

Liverpool 2018/19 – pointi 9
Ilionekana kama vile Liverpool wameshamaliza kazi baada ya kuichapa Arsenal 5-1 na kuweka pengo la pointi tisa kileleni dhidi ya timu iliyokuwa ikishika nafasi ya pili, Tottenham Hotspur, Desemba 29.

Wakati huo, Manchester City ilikuwa haijacheza mechi yake dhidi ya Southampton, ambapo ilishinda na kufanya pengo la pointi kuwa saba.
Liverpool walikwenda kufungwa mechi yao muhimu zaidi dhidi ya Man City Januari, kabla ya kupata sare za bila kufungana na Manchester United na Everton.

Baada ya hapo, Man City ya Pep Guardiola ilishinda mechi 14 mfululizo na kwenda kubeba ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa pili mfululizo, pointi moja zaidi ya Liverpool, ambao walivuna 97 huku mastaa wake, Mohamed Salah na Sadio Mane kila mmoja akifunga mabao 22 na kugawana Kiatu cha Dhahabu huku kipa Alisson akichaguliwa kuwa bora kwa msimu baada ya kucheza mechi 21 bila ya kuruhusu wavu wake kuguswa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hujaweka wazi,hizo timu zilikuwa zinaongoza zikiwa zimecheza mechi zaidi ya wanaofuatia au kwa idadi ya mechi sawa?! Pia weka wazi nini kilitokea miaka hyo kusababisha hao walioongoza kushindwa kubeba ndoo. Kisha ndio uifananishe Liverpool ya sasa na hayo mazingira kabla hujafunga mjadala wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool ya 2018/19 na hii ya sasa 2019/20 zina utofauti gani Mkuuu, mimi naona timu ile ile benchi lile lile ila msimu tofauti, hawa Liver siyo wa kuwaamini kwa 100%
Utofauti ni kwamba Liverpool ya 2018/2019 ilikuwa inakabiliana na timu bora ilikuwa kwenye ubora wake Man city, 2019/2020 yupo Leicester ambayo haiwezi kuwa bora kama man city msimu uliopita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool ya 2018/19 na hii ya sasa 2019/20 zina utofauti gani Mkuuu, mimi naona timu ile ile benchi lile lile ila msimu tofauti, hawa Liver siyo wa kuwaamini kwa 100%
Hazina utofauti mkuu kwahiyo inawezekana liver akafikisha 90+ sasa yule aliyemzuia liver msimu uliopita ana ubavu msimu huu?
 
Back
Top Bottom