Liverpool yamsajili Alexander Isak na kuweka rekodi Ligi Kuu England

Liverpool yamsajili Alexander Isak na kuweka rekodi Ligi Kuu England

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Liverpool wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexander Isak kutoka Newcastle United, wakiweka rekodi mpya ya usajili England kwa mara ya pili msimu huu wa joto.

IMG_6071.jpeg


Alexander Isak ametangazwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Liverpool kwa usajili wa rekodi wa £125m kutoka Newcastle kwa Mkataba hadi Juni 2031.

IMG_6073.jpeg

Baada ya kunyakua taji la Ligi Kuu msimu uliopita, Liverpool wamewekeza kwa kiwango cha juu kuhakikisha wanatetea ubingwa wao msimu huu.

IMG_6072.jpeg

Usajili wa Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen kwa £116 milioni ($156.6 milioni) ulivunja rekodi ya kihistoria ya Ligi Kuu, huku wachezaji wengine kama Hugo Ekitiké, Milos Kerkez, Jeremie Frimpong, Giovanni Leoni, Ármin Pécsi, na Freddie Woodman wakijiunga na kikosi cha Arne Slot.

IMG_6068.jpeg
 
utashangaa watu wanapiga kelele Nyokores Nyokores, mwamba huyo hapo msomali katua Anfield na atawaweka nyingi sana
 
Jamaa watakuwa wa moto sana msimu huu
 
You Will Never Walk Alone
Tukutane Baadaye Sasa
 
Sijui Man United wanafeli wapi kusajili vyuma kama hivi ambavyo kukupa goli kuanzia 10+ kwa msimu ni jambo la kawaida.
 
Hiyo first eleven Haina muingereza hata mmoja na hakuna kelele njoo kizimkazi Sasa ukutane na Julio
 
Back
Top Bottom