Liverpoolfc: Ulionywa kwamba KAUNDIME ni habari ingine ukabisha, sasa kiko wap?

Liverpoolfc: Ulionywa kwamba KAUNDIME ni habari ingine ukabisha, sasa kiko wap?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
35.jpg


Jana bwana wadau wa JF Dar Wing tulipata ugeni kutoka Arusha wing, sasa ikabidi ni coordinate na baadhi ya wadau wenzangu kina Madam B, amu, Kipaji Halisi, Kaizer Paloma, Bujibuji, Asprin, Vin Diesel na mdau mmoja aliyevamia meza yetu na kujitambulisha kwa jina ambalo miongoni mwetu hakuna aliyewahi kukutana na jina hilo hapa JF.

Tuachane na hayo maana hata jina lenyewe nimeshalisahau. Bujibuji hebu nikumbushe, yule jamaa BONGE alisema anaitwa nani vile, maana nakumbuka alisema anajuana na yule Mbunge Mtata wa chama Tawala wa kule Singida….. Hebu ngoja nimpotezee kwanza nisije nikapoteza point ya kile nilichotaka kusema.

Sasa, pale Leo Tupo Hapa Pub, Bwana mkubwa MJEDA kafanya reshuffle kidogo, kaleta binti mmoja kutoka mji kasoro bahari ili kuchukua nafasi ya Binti mwingine aliyepangiwa kazi maalum.

Huyu Binti mpya, ambaye alitambulishwa kwetu na MJEDA kwamba anaitwa KAUNDIME, kwa kweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia. Ni binti mfupi kidogo kama amu, rangi ya mwili wake uko kama chocolate, ana kijikalio cha kushuka na miguu iliyoshiba hasa. Macho yake madogo kama anasinzia na matiti ya kutuna kwa juu. Lakini pia amejaaliwa sauti nyororo na akizungumza ni kama vile hataki ana anahisi uvivu….

Sasa chalii yetu kutoka Arusha nikamuona macho kodo kodo, nikajua hapa lazima pataumana, ikabidi nitafute mwenyeji, ili nipate wasifu wa yule binti maana wakati huo Mjeda alishaondoka. Si nikampata kijana mmoja anayesaidia shughuli za pale Pub, akaniambia yule binti ni habari ingine, ukiingia kwenye himaya yake ufanye kazi ya ziada kuchomoka maana binti anayajua mahaba ya pwani kuliko.

Aliniambia kwamba ashavunja ndoa zaidi ya 6 huko Magomeni na baada ya kutangaziwa vita ndio akahamia Mwanyamala kwa Ali Manjunju.

Wakati namegewa habari za mrembo Kaundime, Upande wa pili naona mawasiliano kati ya Chalii yetu kutoka A Town na Kaundime yamepamba moto. Chalii hataki kuhudumiwa na mtu yeyote isipokuwa Kaundime. Nikajua hapa Ngondo Igwa. Lakini nikaona hapa lazima nimuokoe chalii yetu, Nikamshirikisha Bujibuji ili ampe somo, Bujibuji kamsomesha Chalii, lakini kwani aliewa. KONTENSA zishashuka kule kunako kichwa cha chini…. Chalii haelewi soma, ni yeye na Kaundime………….Kaundime na yeye.

Mie na Kaizer tukaondoka lakini nikaacha maagizo kwa Bujibuji ili aweke ulinzi shirikishi tusije mpoteza chalii halafu Mwenyekiti wa arusha Wing Arushaone atuletee noma.

Nilipofika Home Bujibuji akanipigia simu kunijuza kwamba Chalii kutoka Arusha katoweka katika mazingira ya kutatanisha. Swali langu la kwanza niliuliza iwapo Kaundime yupo, Bujibuji akaniambia kwamba na yeye haonekani katika eneo la tukio, nikajua chalii keshanasa katika mtego wa Kaundime.

Nilijaribu kupiga simu yake haipatikani, mpaka asubuhi hii simu yake haipatikani, nikajua hapa sasa wana JF wa Dar Wing tuna kesi ya kujibu. Ni hivi punde nimepokea simu kutoka wka chalii.....

" Aisee Mtambuzi, unajua nimeshangaa bado niko Mwananyamala hadi mida hii na simu yangu ilikuwa imezimwa lakini sikumbuki kama ni mimi nilizima maana naona bado iko na chaji……..…"
Nikamuuliza uko na nani..

"Ah, we acha tu tutaongea jioni…."

Sikukubali jibu jepesi nikambana mpaka akaamua kuniambia ukweli…..

"Mzee Mtambuzi acha, yaani acha kabisa, kumbe huku Dar mnafaidi jamaa yangu……………….. Kale kabinti si kalinichukua pale kakaniambia kananipeleka kunionyesha kwake, kisha katanirudisha, basi tulipofika hata sijui nguo nilivua mwenyewe au nilivuliwa, nilishangaa niko juu nazungushwa kama pangaboi la helikopta, yaani hakuna rangi sikuacha ona…… we acha kabisa kale katoto ni kadogo lakini kanajua mambo. Hata sijui nitawambia nini wenyeji wangu…….."

Nikamuuliza sasa nikufuate nikurudishe nyumbani…

"Mzee Mtambuzi hebu subiri kwanza……" aliposema hivyo simu ikakatwa, na nilipojaribu kupiga haipatikani kabisa…… Mpaka mida hii bado haipatikani kabisa.

Nahisi tutakuwa na kesi ya kujibu kwa wadau wa arusha Wing

Mh,Mbona Kaundime anataka kutuletea balaa aisee…..

Bujibuji msaada tafadhali
 
Mtambuzi. Machalii wa Arausha + Kilimanjaro ni mambumbu wa mapenzi. Wanawaza pesa tu.

Tafadhali toa taarifa ktk kituo cha polisi kilichokaribu na wewe.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Nakwambia ya kwamba hata chenji niliyokuwa nayo ya Kenya shilling zaidi ya elfu kumi na tatu nimeiona ilipo? Hapa ndiyo nipo hapa Kariakoo NBC BRANCH kwenye ATM nafanya namna nipate chenji ya kuweka mfukoni.

Baada ya hapa ntakupigia Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Nakwambia ya kwamba hata chenji niliyokuwa nayo ya Kenya shilling zaidi ya elfu kumi na tatu nimeiona ilipo? Hapa ndiyo nipo hapa Kariakoo NBC BRANCH kwenye ATM nafanya namna nipate chenji ya kuweka mfukoni.

Baada ya hapa ntakupigia Mtambuzi

Hebu subiri kwanza.....

Hapo uko na nani vile................?
 
Mtambuzi. Machalii wa Arausha + Kilimanjaro ni mambumbu wa mapenzi. Wanawaza pesa tu.

Tafadhali toa taarifa ktk kituo cha polisi kilichokaribu na wewe.
Hivi kumbe eh.............!

Aisee Machalii wa A-Town hebu mzikilizeni huyu Mzee kwanza..............!
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Mtambuzi. Machalii wa Arausha + Kilimanjaro ni mambumbu wa mapenzi. Wanawaza pesa tu.

Tafadhali toa taarifa ktk kituo cha polisi kilichokaribu na wewe.

Wewe mjinga watake radhi hawa wakongwe wa A town acha kutoa misemo mingine isiyo na macho.
 
Last edited by a moderator:
hii ni kali zaidi jamani mabesti wa kiume kueni macho mkija hapa bongo

"Aliniambiwa kwamba ashavunja ndoa zaidi ya 6 huko Magomeni na baada ya kutangaziwa vita ndio akahamia Mwanyamala kwa Ali Manjunju.
"
 
Back
Top Bottom