Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Anasema alipewa kazi ya ulinzi Kiwango Security, katika kazi yake ya ulinzi, kuna siku alipangiwa kulinda kwa Capt. Komba, ndipo alipokutana na mkewe Edina alikuwa house girl kwa Komba, akamletea kanda ya nyimbo za dini, akaiomba, huo ukawa mwanzo!.

P.
........zo! baada ya kuingia chumbani kuikwamua kanda iliyokwama.
 
Nimeangalia hicho kipindi,kuna jambo kubwa sana la kujifunza,kuna haja ya kubadili mentalit kuhusu watu wasiopata nafasi ya kukaa darasi haina maana hawana akili,wasomi wengi hujijengea atittude ya academic arrogant(ce) na wanaishia hapo tu....mifano iko mingi kwa watu waliofika mbali na wana elimu duni....
Kwani kusaga wa clouds ana elimu gani
 
Wanabodi,

Kama ambavyo huwa ninajinasibu humu kuwa mimi sina chama, na sina mtu, kwenye mazuri napongeza, na kwenye mabaya nakosoa, naangalia hapa Clouds TV, Mbunge wa Mtera, Mh. Livingstone Lusinde anahojiwa mubashara, japo elimu yake ni darasa la saba tuu, lakini kiukweli kabisa, jamaa huyu ni kichwa mbaya!, anauwezo Mkubwa sana wa uelewa wa mambo, ufahamu, uwezo wa kujieleza, lakini kwa kumsikiliza tuu, nimebaini huyu Jamaa ana kitu kingine kikubwa cha ziada, he has powers. Ni kupitia powers hizi, ndizo zilizomfanya aweze kumngoa Mzee Malecela kule Mtera.

Kwa wenye nafasi Angalieni Clouds TV saa hii, mtakubaliana na mimi.

Ameanza kwa kuelezea chanzo cha jina la kibajaji, alipewa jina hilo na Mzee Malecela baada ya yeye kujaza fomu kuchuana naye ndani ya CCM, kwa vile yeye aliitwa Tinga Tinga, akasema huu ni mpambano wa Tinga Tinga na Kibajaji, kitasagwa hadi maiti hataonekana!. Alipombwaga ndipo jina hilo likapata umaarufu..

Kibajaji anasema tangu amezaliwa hakuwahi kumjua baba yeke hadi amefariki, wamezaliwa wengi, kilichompa usongo wa maisha, ni kusikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya umasiki uliotopea katika familia yake. Kuna wakati mama yake alishindwa kutoka nje kutoka na kuwa na Kaniki moja tuu, inafuliwa usiku na kuanikwa kisha inasubiriwa kukauka ndipo mama atoke!, akaogopa kuwa kwa hali hii, siku ikitokea shida, mama yake anaweza kutembea uchi!, na kweli walikuja kupata msiba wa kufiwa na dada yake, shauri ya umasikini, walishindwa hata kupata sanda tuu ya kumzikia, wakamzika na kumviringisha kwenye gunia!. Hili jambo lilimuumiza sana, akaamua lazima apambane na kuandoka nyumbani!. (This is very bitter reality!).

Aliombwa nyumbani kwao na mama mmoja kumbebea mizigo yake kuja naye Dar, baada ya kufika jijini na kufikisha mzigo salama, kesho yake aliporudi pale yule mama alimfukuza kama mbwa!, kuwa kazi yake ilikuwa ni kuleta tuu mzigo, sasa mzigo umefika. kazi imeisha. Akiwa hana hili wala lile, hana pa kula wala pa kulala, anasema alilala juu ya mti wa mkorosho eneo la Kinondoni Moscow kwa muda wa siku saba, ndipo akaanza kujiongeza kwa kufanya chochote!.

Baada ya pele alianza kujiongeza kwa kufanya chochote, zege amebeba, vibarua amefanya, mizigo, akawa anafanya chochote, ameuza kahawa, amekuwa machinga, amefanya kila kitu. Amewataja baadhi ya aliofanyia kazi.

Anasema alipewa kazi ya ulinzi Kiwango Security, katika kazi yake ya ulinzi, kuna siku alipangiwa kulinda kwa Capt. Komba, ndipo alipokutana na mkewe Edina aliekuwa house girl kwa Komba, akiwa kazini, alipenda kuwahi kazini na kusikiliza nyimbo za dini katika redio yake ya kanda. Hivyo Edina akamuomba kanda ya nyimbo za dini akasikilize ndani, hivyo kanda ikakwama, ndipo akaitwa ndani kurekebisha mambo, na huo ukawa ndio mwanzo!. Akawa anamletea kanda zi nyimbo za dini na huo ukawa mwanzo, hadi wameona, toka kuuza kahawa sasa ni tajiri Mkubwa mwenye mashamba, majumba na magari ya kifahari!.

Anasema yeye kaishia darasa la 3, na mkewe Edna kaishia darasa la nne, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za vyuo vikuu, lakini faida za elimu hizo inaishia kwenye makaratasi tuu, lakini watu wenye elimu ya maisha, hawana makaratasi lakini wanafanya mambo makubwa!.

Anasema amewahi kudharauliwa sana kutokana na umasikini, hivyo kisiasa, amedharauliwa sana, amekiri kwenye siasa, fitna zipo. Anasema usipende kujibu kila tuhuma, amesema yeye ni msomi wa hali ya juu sana ya elimu dunia, elimu ya maisha, hivyo wanaosema hajasoma, wanamtaka aonyeshe vyeti, akasema akionyesha vyeti, watasema hajatahiriwa, then ataonyesha nini?, hivyo haonyeshi vyeti ila amesoma na sio elimu ya darasani!.

Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.

Kiukweli mimi nimeguswa na historia ya huyu jamaa, na kuna kitu nimejifunza kwake kuhusu elimu ya darasani ya ma vyeti na elimu ya maisha kutokana na usongo wa umasikini!. Hata Bakhresa aliishia elimu ya madrasa tuu!.
Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.

Asanteni kufuatilia.

Paskali
Profiles nyingine za watu mbalimbali na mwandishi huyu ni hizi
Steven Kanumba: Has a Very Touching Story!
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!
Mafuru ni Mmoja wa Mashujaa wa Taifa Hili, Kwa Kuwa Mkweli Daima, Jee Kupangiwa Kazi Muhimu Zaidi?.
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza ni Jasusi. To Hell with...!
Paskali tofautisha baina ya "interesting story" na "brilliance"; that guy is a dumbass, period. Fuatilia michango yake bungeni tangu aingie mpaka keshokutwa, kama hafanyi mizaha basi kazi yake ni kutukana Wapinzani especially Mbowe, Lissu au Halima, katika utatu wa kijinga Kibajaji, Msukuma na Mlinga! In fact tukisimamia kwenye michango yao bungeni Msukuma is a more brilliant of the trio!
 
Kibajaji alikuwa MC, ukiisikiliza the story ya maisha yake, utakubaliana na mimi, huyu jamaa ni very intelligent, shule aliishia darasa la 3, mkewe akaishia 4, wakaungana ndio ikawa la 7. Kabla ya ujio wa Wazungu, mababu zetu hawasoma hata darasa moja, bali were very intelligent. Kuna watu wana akili ila hawakubahatika kusoma for lack of opportunity na sio kwa ukilaza.
Kibajaji ni very brilliant!.
P
 
Guys,
Hakuna kitu kinaudhi kama kuona hawa Wabunge wasiokwenda shule Class 7 wanavo watukana Wabunge wasomi kiwango cha Professors kama kina Prof.Muhongo, Prof.Maghembe, Prof. Kabudi etc! Msukuma na Kibajaji ni Wabunge wapuuzi kuliko! Inaonesha chuki za wazi kabisa Darasa la 7 dhidi ya Professors Wasomi!! Sielewi hi dharau inatoka wapi???
Ajabu ni kwamba Spika Very likely Ndugai anatetea huu ujinga kwa vile hana Doctorate wala PhD...!!!

In future kuna haja ya NEC kubadilisha SIFA ZA WAGOMBEA UBUNGE ianzie angalao Form 4 not class 7 wanatia aibu sana hawa vihiyo Darasa la 7! Shame on them....!!
 
Paskali tofautisha baina ya "interesting story" na "brilliance"; that guy is a dumbass, period! In fact tukisimamia kwenye michango yao bungeni Msukuma is a more brilliant of the trio!
Msukuma pia niliifuatilia story yake, kiukweli I serious doubt utimamu wake.
P
 
Paskali tofautisha baina ya "interesting story" na "brilliance"; katika utatu wa kijinga Kibajaji, Msukuma na Mlinga! In fact tukisimamia kwenye michango yao bungeni Msukuma is a more brilliant of the trio!
Mlinga pia sio mzima kabisa
P
 
Kibajaji alikuwa MC, ukiisikiliza the story ya maisha yake, utakubaliana na mimi, huyu jamaa ni very intelligent, shule aliishia darasa la 3, mkewe akaishia 4, wakaungana ndio ikawa la 7. Kabla ya ujio wa Wazungu, mababu zetu hawasoma hata darasa moja, bali were very intelligent. Kuna watu wana akili ila hawakubahatika kusoma for lack of opportunity na sio kwa ukilaza.
Kibajaji ni very brilliant!.
P

P,
Tusitetee ujinga karne hii ya 21. Kibajaji, Msukuma, Mlinga wanabebwa na CCM kwa ajili ya kupeleka mashambulizi kwa Wapinzani and nothing else!!!
Haya majitu hayana hoja ZOZOTE za kujenga nchi Kiuchumi, kisiasa au kiulinzi acha elimu ambayo iliwapitia pembeni kwa kukosa akili!!!
Kama wana akili kweli mbona kuna fursa za kujiendeleza wakasoma mpaka F4 then Open University wakafikia hata level ya Doctors. Mbona hawafanyi hivo kama wana akili?? Tusitetee wajinga wanaotukana wasomi please!!

Nina hakika hao jamaa Kibajaji au Msukuma ikipitishwa inspection hapo Bungeni nina hakika utakuta jamaa mwili mzima umejaa CHALE, HIRIZI(IC) kwapani na viunoni!!!
Ogopa sana mijitu inayoishi au kutegemea NGUVU ZA GIZA!!
 
Paskali tofautisha baina ya "interesting story" na "brilliance"; that guy is a dumbass, period. Fuatilia michango yake bungeni tangu aingie mpaka keshokutwa, kama hafanyi mizaha basi kazi yake ni kutukana Wapinzani especially Mbowe, Lissu au Halima, katika utatu wa kijinga Kibajaji, Msukuma na Mlinga! In fact tukisimamia kwenye michango yao bungeni Msukuma is a more brilliant of the trio!
Mnao andikaga kiswaenglish hata hamnaga lolote mnalojua
 
P,
Tusitetee ujinga karne hii ya 21. Kibajaji, Msukuma, Mlinga wanabebwa na CCM kwa ajili ya kupeleka mashambulizi kwa Wapinzani and nothing else!!!
Haya majitu hayana hoja ZOZOTE za kujenga nchi Kiuchumi, kisiasa au kiulinzi acha elimu ambayo iliwapitia pembeni kwa kukosa akili!!!
Kama wana akili kweli mbona kuna fursa za kujiendeleza wakasoma mpaka F4 then Open University wakafikia hata level ya Doctors. Mbona hawafanyi hivo kama wana akili?? Tusitetee wajinga wanaotukana wasomi please!!

Nina hakika hao jamaa Kibajaji au Msukuma ikipitishwa inspection hapo Bungeni nina hakika utakuta jamaa mwili mzima umejaa CHALE, HIRIZI(IC) kwapani na viunoni!!!
Ogopa sana mijitu inayoishi au kutegemea NGUVU ZA GIZA!!
Tusidharau watu kwa elimu ya mzungu ya darasani, watu wana elimu ya asili ni kubwa na inawasaidia kuendesha maisha vizuri kuliko hata ma PhD holders!.
P
 
Wanabodi,

Kama ambavyo huwa ninajinasibu humu kuwa mimi sina chama, na sina mtu, kwenye mazuri napongeza, na kwenye mabaya nakosoa, naangalia hapa Clouds TV, Mbunge wa Mtera, Mh. Livingstone Lusinde anahojiwa mubashara, japo elimu yake ni darasa la saba tuu, lakini kiukweli kabisa, jamaa huyu ni kichwa mbaya!, anauwezo Mkubwa sana wa uelewa wa mambo, ufahamu, uwezo wa kujieleza, lakini kwa kumsikiliza tuu, nimebaini huyu Jamaa ana kitu kingine kikubwa cha ziada, he has powers. Ni kupitia powers hizi, ndizo zilizomfanya aweze kumngoa Mzee Malecela kule Mtera.

Kwa wenye nafasi Angalieni Clouds TV saa hii, mtakubaliana na mimi.

Ameanza kwa kuelezea chanzo cha jina la kibajaji, alipewa jina hilo na Mzee Malecela baada ya yeye kujaza fomu kuchuana naye ndani ya CCM, kwa vile yeye aliitwa Tinga Tinga, akasema huu ni mpambano wa Tinga Tinga na Kibajaji, kitasagwa hadi maiti hataonekana!. Alipombwaga ndipo jina hilo likapata umaarufu..

Kibajaji anasema tangu amezaliwa hakuwahi kumjua baba yeke hadi amefariki, wamezaliwa wengi, kilichompa usongo wa maisha, ni kusikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya umasiki uliotopea katika familia yake. Kuna wakati mama yake alishindwa kutoka nje kutoka na kuwa na Kaniki moja tuu, inafuliwa usiku na kuanikwa kisha inasubiriwa kukauka ndipo mama atoke!, akaogopa kuwa kwa hali hii, siku ikitokea shida, mama yake anaweza kutembea uchi!, na kweli walikuja kupata msiba wa kufiwa na dada yake, shauri ya umasikini, walishindwa hata kupata sanda tuu ya kumzikia, wakamzika na kumviringisha kwenye gunia!. Hili jambo lilimuumiza sana, akaamua lazima apambane na kuandoka nyumbani!. (This is very bitter reality!).

Aliombwa nyumbani kwao na mama mmoja kumbebea mizigo yake kuja naye Dar, baada ya kufika jijini na kufikisha mzigo salama, kesho yake aliporudi pale yule mama alimfukuza kama mbwa!, kuwa kazi yake ilikuwa ni kuleta tuu mzigo, sasa mzigo umefika. kazi imeisha. Akiwa hana hili wala lile, hana pa kula wala pa kulala, anasema alilala juu ya mti wa mkorosho eneo la Kinondoni Moscow kwa muda wa siku saba, ndipo akaanza kujiongeza kwa kufanya chochote!.

Baada ya pele alianza kujiongeza kwa kufanya chochote, zege amebeba, vibarua amefanya, mizigo, akawa anafanya chochote, ameuza kahawa, amekuwa machinga, amefanya kila kitu. Amewataja baadhi ya aliofanyia kazi.

Anasema alipewa kazi ya ulinzi Kiwango Security, katika kazi yake ya ulinzi, kuna siku alipangiwa kulinda kwa Capt. Komba, ndipo alipokutana na mkewe Edina aliekuwa house girl kwa Komba, akiwa kazini, alipenda kuwahi kazini na kusikiliza nyimbo za dini katika redio yake ya kanda. Hivyo Edina akamuomba kanda ya nyimbo za dini akasikilize ndani, hivyo kanda ikakwama, ndipo akaitwa ndani kurekebisha mambo, na huo ukawa ndio mwanzo!. Akawa anamletea kanda zi nyimbo za dini na huo ukawa mwanzo, hadi wameona, toka kuuza kahawa sasa ni tajiri Mkubwa mwenye mashamba, majumba na magari ya kifahari!.

Anasema yeye kaishia darasa la 3, na mkewe Edna kaishia darasa la nne, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za vyuo vikuu, lakini faida za elimu hizo inaishia kwenye makaratasi tuu, lakini watu wenye elimu ya maisha, hawana makaratasi lakini wanafanya mambo makubwa!.

Anasema amewahi kudharauliwa sana kutokana na umasikini, hivyo kisiasa, amedharauliwa sana, amekiri kwenye siasa, fitna zipo. Anasema usipende kujibu kila tuhuma, amesema yeye ni msomi wa hali ya juu sana ya elimu dunia, elimu ya maisha, hivyo wanaosema hajasoma, wanamtaka aonyeshe vyeti, akasema akionyesha vyeti, watasema hajatahiriwa, then ataonyesha nini?, hivyo haonyeshi vyeti ila amesoma na sio elimu ya darasani!.

Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.

Kiukweli mimi nimeguswa na historia ya huyu jamaa, na kuna kitu nimejifunza kwake kuhusu elimu ya darasani ya ma vyeti na elimu ya maisha kutokana na usongo wa umasikini!. Hata Bakhresa aliishia elimu ya madrasa tuu!.
Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.

Asanteni kufuatilia.

Paskali
Profiles nyingine za watu mbalimbali na mwandishi huyu ni hizi
Steven Kanumba: Has a Very Touching Story!
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!
Mafuru ni Mmoja wa Mashujaa wa Taifa Hili, Kwa Kuwa Mkweli Daima, Jee Kupangiwa Kazi Muhimu Zaidi?.
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza ni Jasusi. To Hell with...!
Unamjua mtu ambaye hajui kitu anaweza kuwa na confidence kubwa sababu yupo yupo tu kushinda anayejua maana anayejua huwa na uoga kwenye approach zake. Lakini haiondoi ukweli kwamba huyo jamaa ni mjinga sana
 
Naendelea kusisitiza, tusidhsrau watu kwasababu ya ukosefu wa elimu ya darasani na papers qualifications!. Kuna elimu mbili na faida mbili za elimu hizo. Elimu ya kwanza ni elimu ya maisha, na elimu ya darasani. Elimu ya maisha ni wale ambao wana elimu ya nature ambao hawakubahatika kupata elimu ya darasani ya papers qualifications, lakini wameyapatia sana maisha, they are successful, wanaishi maisha bora, nyumba nzuri, gari zuri, kula vizuri, miradi kibao ya investments etc. Hawa ndio kina Kibajaji, Kishimba, Musukuma, Bakhresa and the like, ni darasa la Saba lakini wamefanikiwa.

Na kuna watu wamesoma sana, wana elimu kubwa ya darasani, wengine hadi Ph.D, wana ma vyeti ya kutishia, lakini zote hizi ni papers qualifications, lakini maisha yanawapiga!. Hawa ndio kina Dr. Shika!. Wengine ni ma rugged trousers philanthropists, tunawajua.

Hivyo the value ya elimu ni kuyawezea maisha na kusaidia wengine. Kama mtu ameelimika vizuri sana with papers qualifications lakini maisha yanampiga na hasaidii jamii, na mwingine ni darasa la Saba aliye win, who is better?.
P
 
Guys,
Hakuna kitu kinaudhi kama kuona hawa Wabunge wasiokwenda shule Class 7 wanavo watukana Wabunge wasomi kiwango cha Professors kama kina Prof.Muhongo, Prof.Maghembe, Prof. Kabudi etc! Msukuma na Kibajaji ni Wabunge wapuuzi kuliko! Inaonesha chuki za wazi kabisa Darasa la 7 dhidi ya Professors Wasomi!! Sielewi hi dharau inatoka wapi???
Ajabu ni kwamba Spika Very likely Ndugai anatetea huu ujinga kwa vile hana Doctorate wala PhD...!!!

In future kuna haja ya NEC kubadilisha SIFA ZA WAGOMBEA UBUNGE ianzie angalao Form 4 not class 7 wanatia aibu sana hawa vihiyo Darasa la 7! Shame on them....!!
PHD holders wanaongea nonsense, ndio maana wanadharauliwa. Yaani ukiwasikiliza wasomi wengi walioingia kwenye siasa utatamani usisomeshe wanao
 
Guys,
Hakuna kitu kinaudhi kama kuona hawa Wabunge wasiokwenda shule Class 7 wanavo watukana Wabunge wasomi kiwango cha Professors kama kina Prof.Muhongo, Prof.Maghembe, Prof. Kabudi etc! Msukuma na Kibajaji ni Wabunge wapuuzi kuliko! Inaonesha chuki za wazi kabisa Darasa la 7 dhidi ya Professors Wasomi!! Sielewi hi dharau inatoka wapi???
Ajabu ni kwamba Spika Very likely Ndugai anatetea huu ujinga kwa vile hana Doctorate wala PhD...!!!

In future kuna haja ya NEC kubadilisha SIFA ZA WAGOMBEA UBUNGE ianzie angalao Form 4 not class 7 wanatia aibu sana hawa vihiyo Darasa la 7! Shame on them....!!
Akimpongeza mbunge wa Mtera mh Lusinde kwa uchambuzi mzuri wa hotuba ya Waziri Mkuu uliotumia dakika 15 Spika Ndugai amesema Kibajaj anawazidi wasomi wengi mle bungeni.

Spika amesema bungeni yanahitajika maarifa huo uprofesa ni kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti hivyo katika siasa uprofesa hauna maana yoyote.

Ndio maana wabunge watatu wamewaponda maprofesa tukianza na Kishimba, Kibajaji na kuna wakati Dr Ndugulile aliwahi kumuita waziri fulani Profesa Ziro nikamtoa nje haa haaa amecheka Ndugai.

Ndugai amewataka maprofesa kuwa makini wanapohutubia bungeni kwani darasa la 7 akina Kibajaji, Msukuma Tabasamu, Jah people, Kiinanasi, Babu Tale nk nk wako makini kweli.

Chanzo: TBC

My take; Mbona wabunge wa darasa la 7 ni wanaume watupu!
Mimi naunga mkono hoja za Spika.
P
 
Nilimfamu yangu akiwa chadema . Tulipoteana punde nikasikia ni mbunge, tukakutana pale Kawe , nikamuuliza ubunge umeupataje? Alichonijibu " Mimi Ni professor wa elimu dunia ." Hongera kibajaji, una upeo mkubwa wa mambo .
 
Back
Top Bottom