Livingstone Lusinde(Mb): Muuza kahawa aliyemuoa house girl!

Livingstone Lusinde(Mb): Muuza kahawa aliyemuoa house girl!

Professor Lipumba achukue mfano wa Bwana Kibajaji, akaanze kuuza kahawa sasa.
 
Katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.
Umeona mkuu, hatari sana hii
 
Kwa hiyo kichomsaidia kupata hiyo prado ni nidhamu au kahawa? Aache upuuzi aseme tu fursa ilimtoa ni ubunge na si vinginevyo
 
Basi sitakaa nimlaumu tena Lusinde, mtu anatembea na Housegirl? tena ukute under 18? Kha
 
Basi sitakaa nimlaumu tena Lusinde, mtu anatembea na Housegirl? tena ukute under 18? Kha
Mkuu....
Haujaelewa kilicho andikwa.
Sikujiyo binafsi nilikuwepo pale Rayal Village, wakati lusinde alipokua akitamka vile
 
Basi sitakaa nimlaumu tena Lusinde, mtu anatembea na Housegirl? tena ukute under 18? Kha

Acha ' dharau ' Weye kwani ' mahausigeli ' hawana Mbunye? Tena yawezekana wakawa na ' Mbunye Chocolate ' kuliko hata ' Mbunye Mwarobaini ' aliyonayo Mkeo au Hawara yako? Narudia tena acha dharau kwani kuna hata Rais wako mmoja ( sasa Mstaafu ) Mke wake alianzia kuwa House Girl Nyumbani Kwake na pale Mkewe wa Kwanza alipofariki basi akamuoa Yeye na maisha yakaenda, akamuendeleza Kielimu na hatimaye akawa First Lady wa Taifa hili. Namalizia tena kusema acha dharau. Nimemaliza.
 
Katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.
Kwanza maisha mazuri yakoje?

Yaani ana maisha mazuri kuwashinda Prof Luoga na Kabudi, hii dharau kubwa sana
 
Katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.

Kuna maproffesa na phd holder wengi wanauza kahawa wengine makuli sokoni vile walikosa fursa ya kusoma.

Kuna watu wana vyeti vya uproffesa na phd kwa ujanja ujanja tu , kwa vile wali pata frusa ya kusoma japo kichwani sio kuzuri sana.
 
Ndani ya kila biashara iliyofanikiwa kuna biashara ya siri inayobeba ile inayoonekana. Hata Lugumi alianza kama mpiga brush. Je, kupiga brush ndio kulikompa mafanikio yote hayo?
 
Maisha hayana fórmula mtu yoyote anaweza akawa vizuri ktk nafasi fulani...

Ova
 
Katiba ya kujua kusoma na kuandika kama sifa ya mbunge inaleta dharau kwa wasomi,yaani muuza kahawa anakuja sema ana maisha mazuri kuliko msomi kisa kupiga domo na kujipendekeza tu.
changamoto unasema dharau?
Hivi kweli ukae darasani haswa ushindwe kusukuma prado?
 
Yaani ana maisha mazuri kuwashibda Prof Luoga na Kabudi, hii dharau kubwa sana
Maisha mazuri ni nini? Wanayapimaje? Ni magari, nyumba, elimu, vyeo au ni nini? wanatumia vigezo gani kuhitimisha kuwa Lusinde ana maisha mazuri kuliko maprofesa na wasomi waliotajwa humu?
 
Mbunge wa Mtera mh Lusinde ( Kibajaji ) amesema katika ujana wake alikuwa ni muuza kahawa maarufu pale Kawe ambapo alijulikana kama Stone. Lusinde amesema yeye elimu yake siyo rasmi na kwa hiyo hana cheti chochote cha taaluma ila anajivunia mafanikio makubwa aliyonayo kuwapita hata hao wenye PhD.

Amesisitiza kwamba akiwa muuza kahawa alibahatika kumuoa house girl na waliishi maisha ya kuunga unga lakini kwa sasa mke wake huyo anaendesha Prado VX, hivyo anamshukuru Mungu na kufafanua kuwa kiini cha mafamikio yake ni uaminifu, nidhamu na heshima ya hali ya juu aliyonayo.

Mh Lusinde ameyasema hayo yote katika semina ya fursa anzia sokoni iliyoandaliwa na Clouds Media na kurushwa luningani mubashara kupitia Clouds Tv jana mjini Dodoma.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Nawasilisha!
Mtu anasimama kwenye mkutano wa fursa kisha anaongea huu utumbo? serious? ndo maana nasemaga kuwa hii mikutano ya fursa ya kina clouds ni upotoshaji wa hali ya juu, mimi ni navyojua kuwa mafanikio hayana formula la kama ni hivyo je kuna wauza kahawa wangapi wamefikia hatua ya ubunge ambao wametumia njia alotumia yeye?
 
Hahahaa......!!!
 
changamoto unasema dharau?
Hivi kweli ukae darasani haswa ushindwe kusukuma prado?
acha kuita dharau changamoto, haya majivuni ya kijinga ndo huwa siyapendi hapa jf. sisi ambao hatusukumi prado na tumekaa darasani unatuona punda kweli.

kama umebahatika kusukuma prado mshukuru Muumba, kuna watu wamekaa darasani na wako njema kichwani na harakati za maisha zaidi yako ila mambo si mambo hadi nauli wanaomba.
 
anaheshima huyo? aua wakati akiuza kahawa mitusi anayoporomosha
 
Back
Top Bottom