Ndio kwani katiba itamwona hana akili timamu, ingawa wakati anagombea alikuwa na akili timamu.
Kwa kutumia hoja ya kushambulia kwa matusi mfululizo kwa dakika 16,na baadae kwa maneo yake amekiri yeye ni kichaa wa kuzaliwa imedhirisha kuwa sheria haimruhusu kuendelea kuwakilisha wananchi, kwan uwakilishi unataka mtu mwenye upeo na akili timamu.
Atajitetea, kuwa kweli alikuwa amechanganyikiwa, lakini sasa ni mzima, sheria itatamka kwamba tangu tarehe alipochanganyikwa, inabidi litangazwe jimbo wazi.
Atajitetea, ule ulikuwa ni utani tu, sheria itambana kwani kipindi anatania hakuwa kwenye kitchen party, bali alipewa na katiba kisheria, uhuru na jukwaa kwa ajili ya kampeni.
Na kwa kuwa mh lusinde aliapa kuilinda katiba, ni wazi asingetania kwani alijua madhara yake, hapo ndipo utamu wa sheria utakapo letwa. Maana ataambiwa leta mashahidi kama ulikuwa mzima wakati unaropoka ropoka maneno yaajabu.
Kama unataka kum,shtaki, mimi nitakuwa wakili upande wako.