Liwake jua inyeshe mvua, Murtaza Mangungu ndiyo Mwenyekiti wetu. Shime wana Simba tumpe ushirikiano

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Ikiwa kesho ndio tarehe ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa klabu ya Simba, shime kwa wanachama wote wa Simba ambao wamelipia kadi zao kesho tujitokeze Kwa wingi kumchagua ndugu yetu Murtaza Mangungu Kwenye nafasi ya Uwenyekiti wa klabu yetu kwani ametenda makubwa na ndio mbeba maono wa klabu yetu kufikia mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja.

Pia chonde chonde wale wanachama ambao bado hamjalipia ada, muda bado upo wakulipia ada kadi zenu ili kesho kwa pamoja tukahakikishe ndugu yetu Mangungu anapata nafasi nyingine tena ya kuiongoza klabu yetu.

In Mangungu We Trust [emoji123][emoji123]

[emoji881][emoji881] Nguvu Moja
 
Umejoin January 2023 unajifanya Mwanasimba humu. Na uchaguzi ukiisha ID inaisha. Wanasimba mkataeni huyu akajipie kura mwenyewe
 
Uchaguzi wenu haukuwa na wagombea.Mlilazimishwa kumchagua Hersi Said kuwa Rais.Mpinzani wake alikuwa "stuli".
Simba kuna demokrasia ndio maana kuna wagombea wawili.Wanasimba watamchagua wanayemtaka. Nyie migongo wazi mlitishwa kwamba msipomchagua Hersi hakuna ufadhili.
 
Umejoin January 2023 unajifanya Mwanasimba humu. Na uchaguzi ukiisha ID inaisha. Wanasimba mkataeni huyu akajipie kura mwenyewe
Pamoja na ugeni wa I'd hii ila haiondoi Ukweli kuwa Murtaza Mangungu ni kiongozi Bora zaidi Kwa Sasa pale Simba. Tumpe kura za ndio kwani hakuna kama yeye[emoji3577][emoji123][emoji1732]
[emoji881] Nguvu moja
 
Chawa? Kadi nnayo naenda mchinjia mbali hiyo kesho
Sasa kwa ushauri wa Bure acha kupoteza iyo kura. Kupiga kura upande unaoenda kushindwa Tena kifo Cha mende ni kuikosea kura Yako. Chagua Mangungu Kwa maendeleo ya Simba[emoji881][emoji881]
 
Wanasimba wale wenye kadi halali za uanachama ndio tunaelekea kumchagua ndugu yetu kiongozi shupavu bwana Murtaza Mangungu Kwenye nafasi ya Uwenyekiti
 
Naombeni kujua iwapo yule dada mzuri
Pendo Aidan Mapugilo
alifanikiwa kupata kura za kuwa mjumbe wa Bodi?
 
Azipatie wapi mkuu? Simba ina wenyewe

Amaaa kweli
hivi mtu kama Asha Baraka ana jipya gani?
si mgewachagua watu wengine ili angalau nao muwapime ndani ya hiyo miaka minne?
Kuna Mwnykt nasikia alikuwepo madarakani
bus la club linauzwa then anasema yeye hajui lolote na usikute wamemrudisha tena huyo huyo!
 
... Timu apewe mwina kaduguda ili muendelee kula uji na chapati kama zamani
Mkuu, kwani uji na chapati ni chakula kibaya au kilicho duni? Mbona wengine chapati ndio breakfast yenyewe ukiwekewa na maharage pembeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…