Tatizo ni kuwa kafara huwa haisaidii sana. Ndo maana mzimu wa Liyumba unaendelea kuitafuna serikali. Na utaendelea kuitafuna milele. Kesi ya msingi ya matumizi ya bilioni 221 alishinda wakaishia kumfunga kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo asilimia 90 ya watendaji wetu ndo wako hivi. JK mwenyewe anaongoza kwa matumizi mabaya ya ofisi ndo maana kaishia kuchagua mawaziri ambao hawana tija kwa taifa. watendaji wanaongoza kwa mipango mibovu ambayo inafanya taifa liyumbe kwa kukosa umeme, mafuta, sukari, madarasa mabovu ya shule za msingi, barabara mbovu, makazi mabovu na mengineyo mengi. Kwahiyo, kuendelea kunyanyasa Liyumba eti kwa kuwa alipiga Vicky Kamata ambacho ni kiburudisho cha mzee haisaidii sana. Kesi za wanawake haziwezi kuwa jamabo la msingi kwa taifa wakati watuhumiwa mbalimbali kama kina Chenge, Lowassa, Rosatam Aziz, nk wanapeta mtaani. Heri Liyumba ametuachia majengo pacha ya BOT. Hao wengine mabilioni yetu wameamua kuyalimbikiza nje ya nchi amabayo yanafaidisha mataifa mengine wakati sisi tunataabika. Tanzanians lets change. Lets look issues critically and not superficially. Ukweli ni kuwa Liyumba ni mmoja kati ya maelfu ya wafungwa wetu wanaomiliki vitu mbalimbali magerezani. Kwahiyo ni wazi system ya magereza yetu ni mbovu, ndo maana kabla ya kuwakamata watuhumiwa wa EPA serikali ilitoa mamilioni kukarabati maeneo ya kuwahifadhi watu kama hawa.