...mama yangu weeee,zaidi ya dollar milioni mia mbili? nina uhakika hii pesa ingeweza kukata ile foleni ya magari Dar kwa 100% na kujenga Kigamboni bridge na hata kuongeza 100MW kwenye grid ya Taifa,lakini jamani kama project moja tuu imeweza kulipua 200m USD,je ile nchi ina projects ngapi ambazo nyingine nina uhakika pesa zimetolewa lakini hata hatujawahi kusikia kwa sababu mafisadi walimaliza pesa kabla hazijaanza...yaani EPA,Radar,President Jet,Richmond,Twin towers,IPTL,mikataba ya kina Karamagi ya madini mpaka bandari,mashangingi ya serikali etc wakuu hapo tunaongelea zaidi ya dollar billion moja...naamini tulitakiwa tusiwe na shida ya umeme na barabara zote kuu zingekuwa za lami kama serikali ingekuwa makini,ukiangalia vizuri huu upuuzi wote ulikuwa under Mkapa watch,kweli Mkapa was sooooo much Mr Clean!