Liz Truss dhidi ya kodi kupindukia

Liz Truss dhidi ya kodi kupindukia

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Alipoulizwa kwa nini serikali yake inapunguza kodi wakati huu wa kindumbwendumbwe cha uchumi kote duniani, Liz Truss, Waziri Mkuu wa Uingereza alisema: ' We want people to keep more of the money they earn, so they can have more control over their lives and invest'

Tunataka watu wasalie na kiasi kikubwa cha pesa wanayoichuma, ili waweze kuwa na udhibiti (uhuru) zaidi juu ya maisha yao, na waweze kuwekeza'

Naye Waziri wake wa Fedha, ambaye kwa mara ya kwanza ni wa asili ya Afrika, Kwasi Kwarteng, anasema: 'Sera za makodi makodi hizi ndizo zilizotufikisha hapa! Huwezi kutoza na kutoza na kutoza halafu utarajie maendeleo!'

Tozo ni kodi maradufu, maana wanapotoza tozo huwa tayari umekwishalipa kodi kadhaa. Ukinunua simu, au salio, ujue umeshalipa kodi tayari, na ndiyo maana hizi sasa wakaziita 'tozo' kwa vile huona 'soni' wasiite hiyo 'kodi' kwa mara nyingine.

Kila mwenye akili atakubaliana na Liz na Kwarteng kuwa huwezi kufinya mifuko ya watu mpaka wakashindwa kufanya mambo mengine, halafu utarajie watu hao hao wafanye hayo mambo mengine- it's bizzare!

Kwa sababu unapozungumzia kuwekeza unazungumzia watu wenye fedha 'zaidi' (disposable), ndiyo wafanyao uwekezaji, ambao ndiyo unaondeleza uchumi.

Waziri asema haoni vizuri kuwapa mzigo Watanzania, ila hana budi! Siamini. Petroli pekee inayotumiwa na Mawaziri wenzake, marais wastaafu na Mawaziri wakuu wao, kwa muda wa mwezi tu ingempatia hiyo milioni 200 na zaidi. Kilichopo ni kulindana katika kula mkate wa taifa.

Nchi inayoongozwa na watu wanaowaonea haya au kuwalinda wengine haifiki popote. Haya siyo maneno yangu ni maneno ya Waziri Mkuu wa zamani wa Singapore, Lee Kuan Yew. Nawe unajua Singapore ni nani katika dunia hii. Nchi ndogo kuliko Mkoa wowote wa Tanzania, Ilipoanza miaka ya 60 ilikuwa haina chochote ila michikichi na bandari !....lakini leo inaitwa kwenye vikao vya mataifa 20 bora kwa uchumi duniani!

Natoa fikra. Waziri ahamasishe haraka ichimbwe gesi ya Helium tuliyonayo kwa wingi, na ambayo inakaribia kwisha duniani, atapata fedha hizo chap chap, ili mifuko ya wananchi ipumzike. Sharti tu aweke mazingira shindani ya uwekezaji.

Hakuna nchi nyingine ina Helium kama sisi, hata ile ya Marekani inakwisha!
 
Back
Top Bottom