Umenifurahisha sana Mwafrika unajua CCM wanataka lazima tukubaliane na ideology zao sasa fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung'amua hebu niulize tuchambue sentensi ya huyu mama inasema hivi " kushawishi, watu waipigie kura CCM nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na ikibidi shuka kwa shuka!"
Tukianza kuna neno ushawishi - kuwavutia watu waje , kuwarubuni kwa njia mbali wavutiwe,kimsingi kuwafanya watu wakubaliane na hoja zako. Sasa vishawishi vinaweza kuwa matendo yako mazuri, haiba, elimu, undugu, cheo, pesa na pia mtazamo wa mtu mfano mwanamke mzuri au mwanaume mzuri.
Halafu anasema wa kushawishiwa ni akina nani ni watu - mimi na wewe .
Kufanya nini kuipigia kura CCM.
Sasa shida inakuja katika njia hizo za ushawishi ndio watu wanapingana na mama huyu. Maana anasema nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba hizi mbili zinaeleweka na zinaweza kuwa maana wazi kabisa. Shida inakuja shuka kwa shuka tunavyojua kwa mila na desturi za mtanzania ni kwamba anayeingia ndani ya shuka ni mkeo au mwenza (tukiassume wote sie ni watu wazima). Sasa huyo anayekuja shukani ni nani!!!! Na anakuja kukushawishi nini alichoshindwa kukushawishi nyumbani, chumbani sasa mpaka katika mashuka???
Nawaachia mjijibu wenyewe CCM