Loan Calculator ya HESLB ina kasoro gani? Huyu mnufaika Loan Board anadaiwa mkopo wa karibu Bilioni 48!

Loan Calculator ya HESLB ina kasoro gani? Huyu mnufaika Loan Board anadaiwa mkopo wa karibu Bilioni 48!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hebu kila mtu atazame kwa umakini Risiti ya Mshahara (Salary Slip) ya mtumishi huyu (Mwalimu) aliyesoma kwa pesa za bodi ya mikopo - HESLB...

Ni mjadala unaoendelea ktk group moja la WhatsApp huko na hiki ni kilio cha mwalimu huyu ambaye sasa yuko very frustrated na hajui afanyeje ku - overturn mambo.

IMG-20210110-WA0000.jpg


Huyu mnufaika mikopo ya elimu ya juu anadaiwa na Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) almost Tshs. 48,000,000,000 - yaani bilioni 48...!!

Baada ya kuona hili nikajiuliza maswali haya na naomba tujadili kwa pamoja;

1. Nimejaribu kujiuliza, hili linawezekana vipi? Ni figure ambayo iko pale kimakosa au ndiyo uhalisia wenyewe?

2. Na nikajiuliza hivi HESLB walimkopesha huyu kijana shilingi ngapi na akaenda kusomea ualimu wa aina gani na wapi hapa duniani..?

3. Na hivi sheria ya mikopo ya elimu ya juu kuanzia utaratibu wa kukopa na namna ya kurejesha ikiwemo riba iko vipi...?

4. Kama huu ndiyo UHALISIA, hebu tujiulize, kuwa, hivi serikali ipo kwa ajili ya nani?

5. Kama ipo kwa ajili ya wananchi, mbona kama inafanya biashara haramu ya fedha kupitia kwa wananchi hawa hawa masikini na wanyonge..?

UPDATES:
.......................


Baada ya malalamiko kuzidi hatimaye, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) wamejitokeza na kutoa ufafanuzi...

Japo ufafanuzi wao haujibu maswali mengi ya msingi, lakini at least wamesema kitu..
IMG-20210110-WA0004.jpg
 
Jamaa deni lake kama taasisi kubwa inadaiwa, so sad!
Body ya mikopo hainipati ng'o...natamba nimesoma bure sirudishi hata senti.
Rudisha pesa na wengine wasome asee.. mnataka usawa na haki wakati nyie wenyewe mnaonesha makucha mapema kabisa.. ya kukosa uzalendo
 
Rudisha pesa na wengine wasome asee.. mnataka usawa na haki wakati nyie wenyewe mnaonesha makucha mapema kabisa.. ya kukosa uzalendo

Taifa linakusanya kodi kutoka kwa wananchi kisha inawakopesha kodi hizo hizo kuwasomesha wananchi halafu inawadai na riba kubwa.. yaani pesa zako mwenyewe unakopeshwa
 
Mimi nimeshaandika humu mapungufu na uozo mkubwa wa HESLB katika calculations zao

Halafu tatizo kubwa hawashughulikii kero za watu, wamenikata pesa za miezi kadhaa lakini kwenye statement yao haioneshi kuwa nimekatwa

HESLB ni wezi tu kama CRDB Bank.

Waziri wa Elimu anapaswa aende pale atumbue hao watumishi wa hovyo hovyo.
 
Hiyo itakuwa na makosa. Inarekebishika... hakuna mtu anaweza daiwa 47 Billion..
Makosa kila siku huko HESLB, Nenda kwenye mayawi yao ya kanda then uanalyse makosa ya watu utakaowakuta

Ni Uzembe tu
 
Same to me
Hata wakinitafuta hawanipati. Situmii jina niliokuwa natumia chuo, pia sipo kwenye system ya ajira.
Kuna mtu hapo juu kaniambia niwe mzalendo nikalipe...yaani nijipeleke mwenyewe kweli[emoji3][emoji3]. Mimi ni mzalendo lakini kwenye hilo hapana aisee
 
Back
Top Bottom