Lockdown ina ukweli kiasi gani?

Lockdown ina ukweli kiasi gani?

Mtyela Kasanda

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2018
Posts
554
Reaction score
818
Mbona wenye lockdown bado wanafanya shughuli kama kawa?

Marekani tokea corona ianze hawajaacha kutengeneza filamu, na filamu zina watu zaidi ya 100 on set. Hawakuacha kufanya kampeni, japo midahalo ilikua na virtual attendees lakini mikutano watu walikua wanajaa tena wengine bila barakoa.

Korea Kusini, hawa hawajaacha kutengeneza series zao zile tangu corona ianze. Na siriz zao hawa zina watu wengi kweli, hua wanaonesha mwisho wa sirizi kwa hesabu ya haraka sio chini ya watu 200 kwa season 1.

Sisi kwanini tujiwekee lockdown? Kwanini wanaharakati wanalazimisha tuwekwe lockdown?

Mkurugenzi wa Pfizer kampuni inayotengeneza chanjo ya korona alisema "ni lazima makampuni ya chanjo yatengeneze faida". Kwanini tulazimishwe kutajirisha nchi nyingine kwa kununua chanjo zao kwa bei kubwa?

Corona ipo ila kama watanzania tujifunze kuishi nayo kwa kuchukua tahadhari, tuiamini serikali yetu pia kwakua inapokea taarifa nyingi na inajua mambo mengi zaidi kuliko wanaharakati na wananchi wa kawaida.

Pfizer CEO Says Companies Should Make Profit On Covid-19 Vaccine

7/29/2020 · Pfizer, which has long said it intends to make a profit on its Covid-19 vaccine, is alone among the leading Covid-19 vaccine makers not to have taken government research help
 
Utopolo mwingine hewani na asubuhi asubuhi:

IMG_20210218_174254_207.jpg

Hiiiiii bagosha!
 
Kwa upande wangu, lock-down ni approach ya ku'deal' na situation ambayo uthibiti wake ni mgumu. Kwa mfano, mataifa mengi ambayo yalikuwa yakipoteza watu wengi kwa siku yaliona ni njia 'effective' ya kuvunja mnyororo wa maambukizi. Whether njia hiyo imesaidia au la kumaliza tatizo, still bado binafsi natambua kwa nini nchi hizo zilizoathirika sana ziliamua kuchukua approach hiyo.

Ni kama kusema ili kupunguza au kuzuia ugonjwa wa kichocho ni kuachana na kuoga na kunywa maji ambayo yana vidudu vya kichocho. Kuna watu wameacha kunywa na kuoga maji yenye vijidudu vya kichocho na baada ya kutibiwa hawana kichocho tena.

Yet, kuna baadhi ya watu wanakunywa na kuoga maji yenye vijidudu vya kichocho na hawana kichocho au wana 'kichocho dormant' (ambacho hakiwadhuru kabisa au kinaweza kuwadhuru tu mara moja moja).
 
Haijalishi wanataka pata faida or what kinacho matter ni uhai wa mtu, magonjwa mangapi wamewatengenezea na wana make money
.ukimwi
.cancer
.Ebola
N. K

Kila kitu biashara utaki kufa
 
Kwa upande wangu, lock-down ni approach ya ku'deal' na situation ambayo uthibiti wake ni mgumu. Kwa mfano, mataifa mengi ambayo yalikuwa yakipoteza watu wengi kwa siku yaliona ni njia 'effective' ya kuvunja mnyororo wa maambukizi. Whether njia hiyo imesaidia au la kumaliza tatizo, still bado binafsi natambua kwa nini nchi hizo zilizoathirika sana ziliamua kuchukua approach hiyo.

Ni kama kusema ili kupunguza au kuzuia ugonjwa wa kichocho ni kuachana na kuoga na kunywa maji ambayo yana vidudu vya kichocho. Kuna watu wameacha kunywa na kuoga maji yenye vijidudu vya kichocho na baada ya kutibiwa hawana kichocho tena.

Yet, kuna baadhi ya watu wanakunywa na kuoga maji yenye vijidudu vya kichocho na hawana kichocho au wana 'kichocho dormant' (ambacho hakiwadhuru kabisa au kinaweza kuwadhuru tu mara moja moja).
nimekuelewa na umeeleza vizuri, ninachokisema mimi ni double standards za hawa waleta lockdown. Pamoja na Lockdown jamaa waliendelea kufanya kazi na kutuuzia bidhaa zao, mpaka sasa nchi zetu za Africa hatuna tunachouza huko kwao zaidi ya madini. Tungeweka lockdown si tungetawaliwa zaidi? na hili la kuuza chanjo kwa faida kubwa nalo ni njia ya kutudidimiza, kwasababu shughuli haziendi kutokana na ugonjwa lakini mtu anataka umpe sehemu ya bajeti yako ili akupe chanjo.
 
ndo tatizo la watoto, mnajifanya mnajuuuuuua. Ungekua na familia ya kuhudumia ungesoma mpaka mwisho.

Unajua kupitia COVAX chanjo zote zikiwamo hizi zinapatikana kwa nchi masikini bure?

Wapi unapolazimishwa kumtajirisha nani wewe au nani?

Utoto ni kuandika utopolo wa aina hii pamoja na uwepo taarifa nyingi tu za wazi zilizopo.

Huyo mwenye taarifa nyingi kutuzidi sisi, ndiyo huyo huyo mpiga nyungu mbobezi na mwenye hadithi za kumtajirisha beberu anayetuchangia chanjo za bure?

Mafikara yenu ni kinyume nyume ndiyo maana kuwataarifu utopolo wenu bila simile mbona ni wajibu wetu kweri kweri!
 
nimekuelewa na umeeleza vizuri, ninachokisema mimi ni double standards za hawa waleta lockdown. Pamoja na Lockdown jamaa waliendelea kufanya kazi na kutuuzia bidhaa zao, mpaka sasa nchi zetu za Africa hatuna tunachouza huko kwao zaidi ya madini. Tungeweka lockdown si tungetawaliwa zaidi? na hili la kuuza chanjo kwa faida kubwa nalo ni njia ya kutudidimiza, kwasababu shughuli haziendi kutokana na ugonjwa lakini mtu anataka umpe sehemu ya bajeti yako ili akupe chanjo.
Ngoja nichangie kwa kutoa mfano huu ambao ninautumia kama 'illustration'. Unatoka kwenye kitabu kinachoitwa 'The Bird's Song' by Anthony de Mello (SJ). Kicha cha habari ni 'THE DISABLED FOX'. Stori inaenda hivi: A fable of the Arab mystic Sadi: A man walking through the forest saw a fox that had lost its legs and wondered how it lived. Then he saw a tiger come with game in its mouth. The tiger had his fill and left the rest for the fox. The next day too God sent, the tiger to feed the fox.

The man began to wonder at God’s greatness and thought. “I too shall lie in a corner trusting the Lord to give me all I need.” He did this for a month, and was almost at death’s door when he heard a voice that said, “O you who are on the path of error, open your eyes to the truth! Imitate the tiger not the fox.” On the street I saw a naked child, hungry and shivering in the cold. I became angry and said to God, “Why do you allow this? Why don’t you do something?” God did not reply. That night he said, quite sudden-ly, “I certainly did something. I made you.” Ukisoma stori hii kwa makini na ukilinganisha na ambavyo mataifa yetu ya Afrika yalivyo utagundua kwamba 'almost always' sisi tumekuwa 'fox' kama hadithi hii inavyosema.

Hatufanyi lolote na tunasubiri mataifa mengine yatufanyie na yakifanya kwa jinsi tusivyopenda tunayalalamikia. Miaka nenda rudi viongozi wetu wamekuwa wakisafiri nchi mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali. Ukiondoa mbinu za kivita (ambavyo kwa mtazamo wangu ndilo eneo pekee tunalojifunza na kuja kufanya huku kwetu) maeneo mengine naweza kusema hatujaweza kujifunza na kufanya kitu kinachoonekana kama sisi. Kwenye dunia ya sasa binadamu wote tumekuwa kama wanyama wawindaji - nguvu, mbinu za kuwinda na mbio tulizonazo - ndivyo vitakavyotuokoa kutoliwa na wanyama wengine. Otherwise, tutabaki watu wa kulalamika. Angalia hata hapa kwetu - kama kuna magari mengi kwenda Gongo la Mboto, ukisafiri kutoka Tazara utaenda kwa Sh400. Kama kuna magari machache, kuna daladala zitapakia kwa Sh1,000, bajaji 1,500 au Sh2,000 na pikipiki Sh3,000.

Nadhani unakumbuka kanuni ya 'supply' na 'demand'. Kwa kifupi, wakati wa shida ndiyo pia wakati wafanyabiashara wanapata faida zaidi na huwezi kuwalaumu kwa sababu kama shida hakuna hata wao wanauza kwa bei ya kutupa. Uzalishaji wa nyanya au vitunguu ukiwa mwingi utanunua kwa bei ya kutupa, lakini zikiadimika itabidi ujikune kichwa. Makampuni yanayotengeneza dawa pia yanafuata kanuni hii ya 'supply' na 'demand' . Solution ni nini? Tusiwe kama 'fox', tumwige 'tiger' kwenye stori. Tuwekeze kwenye utafiti na matokeo yake yafanyiwe kazi na mamlaka husika na taratibu taratibu na sisi tutakuwa na mchango mkubwa kwa dunia na tutakuwa na uwezo mkubwa wa bargain' kibiashara kwa sababu na sisi tunajua tutawashika wanaotupandishia bei au wanaotuuzia bidhaa feki.
 
Back
Top Bottom