Lockdown ni hatari kuliko Corona

Quinn

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
473
Reaction score
1,184
Watu wachache wanalaumu hatua zilizochukuliwa Tanzania kwenye kupambana na Corona, wengine wanafikiri serikali inapaswa kufungia wananchi ndani (lockdown).

Wananchi wanafikiri Uchumi wa Tanzania hauna uhusiano na Uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uchumi wa Tanzania ukianguka basi jua na uchumi wa mtu mmoja mmoja utaanguka na maisha yatakuwa magumu.

Maisha ya watu wowote pale Duniani utegemea uchumi wa Nchi. Uchumi wa Nchi ukianguka basi maisha ya watu yanakuwa magumu sana maana hata akiba ya taifa ya kununua huduma za jamii kama vifaa tiba na madawa unakosekana.

Nchi itakosa kulipa watu mishahara, mabenki yatafirisika maana BOT itashindwa ata kuongeza ukwasi kwenye mabeki “liquidity injection”.

Gharama za maisha zitakuwa juu maana serikali itakuwa haina uwezo hata wa kustabilize vitu, mfano sukari ikipanda bei kutokana na uzalishaji mdogo wa ndani basi serikali inayojiweza kiuchumi inaagiza sukari nje ili kushusha bei ya sukari iliyopo na hvyo maisha kuwa nafuu.

Mfano wa madhara ya kuanguka kwa uchumi wa nchi ni nchi ya zimbabwe ambapo maisha yamekuwa ghali sana na kusababisha wananchi wengi kukosa huduma za kijamii asa wale maskini.

Lawama zinazotolewa na watanzania kuwa Serikali inathamini Uchumi kuliko maisha ya watu na kusahau kuwa Uchumi wa Nchi ndio Maisha ya watu, Uchumi wa Nchi ukianguka basi tegemea Vifo vingine kutokana na kukosa mahitaji muhimu, leo hii Trump kagoma kuongeza muda wa kukaa ndani, Brazili uko wananchi wanaandamana watoke nje na south Africa wameanza kuweka utaratibu wa kutoka nje.

“Lockdown haifai kabisa Tanzania”,


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naunga mkono hoja..
Kwasababu za kiuchumi nchi inaweza kuanguka kutokana na lockdown,hii inatakiwa dunia ijifunze na ije na mikakati kwani ipo siku kunaweza tokea tatizo Kama hili na likaleta maafa makubwa sana!.

Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa elimu na ufahamu kiujumla!,Ni dhahiri tunahitaji kuweka nguvu kubwa ktk kupambana na magonjwa ya milipuko ili yasije tokea maafa ya kiuchumi...

Hili likorona linatakiwa liwe funzo kwa viongozi ni mstakabari upi wanatakiwa wachukue ili kukabiliana na majanga kama haya.. wengi wa viongozi hawajui maana ya uongozi ila wanajua maana ya kujaza matumbo Yao!!

Kuwa kiongozi maana yake kubwa ni kulinda "HUMANITY".
 
Tulisha bugi hii issue Lockdown ingeenza mapema tena kufunga Usafiri wa Anga wasiingiee hawa wazungu na wazurulaji wa hapo Bongo kama yule Mmama aliyegundulika na Corona .Meneja wa diamond na Mwanafalisafa

Sasa hivi tungekuwa tunadunda tu kama kawa ila kwa sasa tumeshaharibu kila kitu ugonjwa umeshasamba nchi nzima
Leo utasikia kimewaka
Dar
Arusha
Dar
Mbeya
Mtwara
Kigoma
Kagera

........

.........
...
Ee Mwenyezi Mungu tunaomba utukinge na kutukoa na huyu shetana kolonya










Sent using Jamii Forums mobile app
 

Corona hailetwi na watu tu...hata tungefunga usafiri wa abiria wa kutoka nje bado Corona ingeingia maana Corona Virus anaweza kukaa masaa nane nje ya mwili wa Binadamu hivyo ndege za mizigo zinazotoka masafa yaliyo ndani ya masaa manane basi corona virus anaingia nchini na kumwingia binadamu atakaye gusa mzigo huo.

Marekani ndipo ilipobugi hapo walitumia nguvu nyingi kudhibiti na kupima watu wanaingia ila hawakujua uwezo wa kirusi kuingia kupitia mizigo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Africa Total lockdown haifai,inayotufaa ni partial lockdown,sababu zaidi 70% ya Watanzania wanategemea watoke ndio wale.
 
  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Familia ya Prof. Mahiga inaku prove wrong.
 
Kwa sasa tunavuna mbegu ya kuwaweka madarakani vilaza wasomi
 
Maneno ya kujifariji tuu haya Korona ukishindwa idhibiti huo uchumi ndio utapigika maradufu.

Tuheshimu sayansi jamani na kumuomba Mungu...... Hizi nyingine ni blah blah blah tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…