Quinn
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 473
- 1,184
Watu wachache wanalaumu hatua zilizochukuliwa Tanzania kwenye kupambana na Corona, wengine wanafikiri serikali inapaswa kufungia wananchi ndani (lockdown).
Wananchi wanafikiri Uchumi wa Tanzania hauna uhusiano na Uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uchumi wa Tanzania ukianguka basi jua na uchumi wa mtu mmoja mmoja utaanguka na maisha yatakuwa magumu.
Maisha ya watu wowote pale Duniani utegemea uchumi wa Nchi. Uchumi wa Nchi ukianguka basi maisha ya watu yanakuwa magumu sana maana hata akiba ya taifa ya kununua huduma za jamii kama vifaa tiba na madawa unakosekana.
Nchi itakosa kulipa watu mishahara, mabenki yatafirisika maana BOT itashindwa ata kuongeza ukwasi kwenye mabeki “liquidity injection”.
Gharama za maisha zitakuwa juu maana serikali itakuwa haina uwezo hata wa kustabilize vitu, mfano sukari ikipanda bei kutokana na uzalishaji mdogo wa ndani basi serikali inayojiweza kiuchumi inaagiza sukari nje ili kushusha bei ya sukari iliyopo na hvyo maisha kuwa nafuu.
Mfano wa madhara ya kuanguka kwa uchumi wa nchi ni nchi ya zimbabwe ambapo maisha yamekuwa ghali sana na kusababisha wananchi wengi kukosa huduma za kijamii asa wale maskini.
Lawama zinazotolewa na watanzania kuwa Serikali inathamini Uchumi kuliko maisha ya watu na kusahau kuwa Uchumi wa Nchi ndio Maisha ya watu, Uchumi wa Nchi ukianguka basi tegemea Vifo vingine kutokana na kukosa mahitaji muhimu, leo hii Trump kagoma kuongeza muda wa kukaa ndani, Brazili uko wananchi wanaandamana watoke nje na south Africa wameanza kuweka utaratibu wa kutoka nje.
“Lockdown haifai kabisa Tanzania”,
Sent from my iPhone using JamiiForums