Habari ndugu msomaji. Ningependa tukumbushane jambo la muhimu sana tunalopaswa kujifunza na kuzingatia katika maisha.
Kuna baadhi ya misemo inaonekana kama imezoeleka lakini ina maana kubwa sana. Mfano: Maisha ni hapa hapa duniani, dunia ni duara.
Jambo la msingi ninaloweza kusema ni kwamba, LOLOTE UFANYALO KWA MWENZAKO LITAKURUDIA SIKU MOJA, UPENDE AMA USIPENDE. Hata kama lisiporudi maishani mwako, basi kizazi chako kitakutana na matokeo ya yote uliyofanya kwa wenzako ukiwa hai.
Kuna baadhi ya watu walitenda mema sana, walikuwa na huruma kwa wenzao, walikuwa na upendo na moyo wa ukarimu, walijitoa kutenda mema kwa wenzao na walikuja kulipwa mema katika nyakati walizokuwa hawategemei.
Pia, kuna mtu flani alitenda mabaya, alionea wengine, alitoa rushwa akapindisha haki, alidharau wengine, alitoa machozi kwenye macho ya watu, na siku asiyoitegemea alipokea mambo magumu yaliyogharimu maisha yake na furaha yake daima.
Ndugu zangu, tujitahidi kutenda mema ili mema yarudi katika maisha yetu. Tusipende kuumiza mioyo ya watu kwani machozi yao hayadondoki bure ipo siku machozi hayo yatatiririka kwenye macho yetu. TENDA WEMA NENDA ZAKO.
Tafadhari bonyeza Vote hapo chini kama umependa chapisho hili. Asante sana.

Upvote
11