London hakuna Migahawa ya Vyakula vya Kiswahili

Zanzibar2014

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2022
Posts
743
Reaction score
591
Habari zenu nyote,

Natafuta Migahawa ya Vyakula vya Kiswahili London au mtu anayepika nyumbani na kuuza chakula kwa mtu mmoja mmoja.

Napika lakini siyo siku zote kutokana na majukumu ya kazi.

Waswahili wa London tafadhali nijuzeni, ahsanteni sana.
 
Daah hivi mlio huko mambele tutoeni ushamba aseee mmetutangulia vingi wadau ! Huwa mkifika kwa upande wa vyakula vya kiswahili mfano najua mkitoka huku wali maharage , au ugali dagaa sijui makande , vitumbua vyakula mbalimbali vilivyotulea mirenda na majani ya maboga huwa mnavikuta huko ulaya ? Na kama hamvikuti huwa mna mbadala gani ? na huko kweli kuna magenge kweli au viduka vya mangi ? Au ndo kila kitu supermarket ?
Chapati je ?😃😃😃😃
 
Migahawa ya posta na masaki unaijua? Basi tofauti hakuna
Daah hivi mlio huko mambele tutoeni ushamba aseee mmetutangulia vingi wadau ! Huwa mkifika kwa upande wa vyakula vya kiswahili mfano najua mkitoka huku wali maharage , au ugali dagaa sijui makande , vitumbua vyakula mbalimbali vilivyotulea mirenda na majani ya maboga huwa mnavikuta huko ulaya ? Na kama hamvikuti huwa mna mbadala gani ? na huko kweli kuna magenge kweli au viduka vya mangi ? Au ndo kila kitu supermarket ?
Chapati je ?[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
London kuna migahawa mingi tu inapika vyakula vya kibongo. Wapo wazungu na wapemba kibao wanaendesha migahawa ya chakula. Bahati mbaya sana, muundo wa vyakula, migahawa na bei vimekaa kitalii zaidi kuliko kiuhalisia wa maisha ya ulaji wa kibongo, hivyo huuzwa kwa bei ghali, huuzwa kwa kufanya order, na taste inaweza isiwe kivileeee.

Jambo lingine ambalo watu wanapaswa kujua ni kuwa, upishi na wapishi kwa zama hizi wamekaa kimataifa zaidi (kuhudumia watu kutoka mataifa tofauti tofauti) hivyo kila siku wanajifunza upishi wa namna tofauti tofauti ili kukidhi haja ya wateja. Mteja akifika tu akimpa order ya chakula basi kinapikwa chap chap. Ni pesa yako tu.

Nadhani mleta mada ameandika hapa for fun tu, hayuko serious na huenda hata London hajawahi kufika.
 
Na mimi nasubir , maana ninahamu na makongoro ya mbuzi pamoja na ugali wa mtama....
 
Daah hivi mlio huko mambele tutoeni ushamba aseee mmetutangulia vingi wadau ! Huwa mkifika kwa upande wa vyakula vya kiswahili mfano najua mkitoka huku wali maharage , au ugali dagaa sijui makande , vitumbua vyakula mbalimbali vilivyotulea mirenda na majani ya maboga huwa mnavikuta huko ulaya ? Na kama hamvikuti huwa mna mbadala gani ? na huko kweli kuna magenge kweli au viduka vya mangi ? Au ndo kila kitu supermarket ?
Chapati je ?😃😃😃😃
Vyote unapata kwasasa, chapati vitumbua ni kuorder tu wanaopika wanaleta.
Au kujiongeza upike, unga,aina zote upo mpk wa bajia,ndizi za mtori kila kitu ,mihogo, magimbi
 
Tafadhali nipatie jina lao, nilitizame, ashante saaana
 
Back
Top Bottom