"Long Distance Relationship" yako ilidumu kwa muda gani au huataki hata kusikia mahusiano ya mbali?

"Long Distance Relationship" yako ilidumu kwa muda gani au huataki hata kusikia mahusiano ya mbali?

Ilidumu mpaka pale aliponiambia nimtumie suti kwa ajili ya kaka yake kuolea na mimi nikatuma kuja kugundua ilikuwa ni suti ya bwana harusi anaemuoa yeye, kuvaa siku ya ndoa yao.
Nawewe ulituma kabisa 😂
 
Yalichonitenda Mungu mwenyewe anajua, jamaa nilidumu nae miaka mitano sikuwahi kumsaliti ila alichonilipa najua mwenyewe kidogo nipelekwe milembe ila nikapelekwa kwa Mwamposa mpaka sasa huyo mjinga amenifanya kuwa single mother wa mtoto ambaye baba yake sikuwahi kumpenda ila nilienda kwake kama kupunguza machungu nikaambulia mtoto. hila yule mb*a popote alipo Mungu amlinde tu make nilimuona mungu mtu nikaambulia kuona picha za harusi mtandaoni.
Polee sana dada, umekosa kotekote
 
Mbona wanasema wanawake wanastahimili sana hisia zao kuliko wanaume mkuu
Wanastahimili sana as long hawakutani na wanaume 🤣 ila kama routine yake 24/7 yuko nje na anakutana mabaharia hawezi kubaki salama. Yupo mmoja tu ataomba namba na atapewa right on time na mchezo wa kuchatishana ukianza jua imeenda.
 
Kuna mmoja anaitwa Kitombise ukimtagi kwenye ishu zinazohusiana na id yake anamaindi hahahaha
IMG_20240717_022119.jpg
 
Mi naona dar ndo sehemu rahisi kwa mwanamke kutulia maana maisha ya mjini tu ni hekaheka tosha, pia wanawake ni wengi na wazuri kiasi wanaume wana machaguo mengi, tofauti na huko miji midogo wanawake wachache hivyo inafanya wawe wa kugombania kama na mchuchu nae anavutia mji mzima utamtaka yeye tu
Hahahahah hakuna sehemu hatarishi kama Dar, kuna kila aina ya starehe na walimu wa kila somo.🤣

Yani mpenzi hata awe decent kiasi gani akiingia tu bandari salama lazma atiwe nyavuni. Oya kuna watu hawaangalii sura amini kwamba tena wanaotoka mikoani ndio huwa so vulnerable.
 
Kwa mwanamke naona kinyume chake kuliko miji midogo mzee, ila kwa mwanaume ndo hakufai pisi ni nyingi na kali halafu rahiiiiiiisiii yani za kuzoa
 
Back
Top Bottom