"Long Distance Relationship" yako ilidumu kwa muda gani au huataki hata kusikia mahusiano ya mbali?

Ilidumu mpaka pale aliponiambia nimtumie suti kwa ajili ya kaka yake kuolea na mimi nikatuma kuja kugundua ilikuwa ni suti ya bwana harusi anaemuoa yeye, kuvaa siku ya ndoa yao.
Nawewe ulituma kabisa 😂
 
Polee sana dada, umekosa kotekote
 
Mbona wanasema wanawake wanastahimili sana hisia zao kuliko wanaume mkuu
Wanastahimili sana as long hawakutani na wanaume 🤣 ila kama routine yake 24/7 yuko nje na anakutana mabaharia hawezi kubaki salama. Yupo mmoja tu ataomba namba na atapewa right on time na mchezo wa kuchatishana ukianza jua imeenda.
 
Hahahahah hakuna sehemu hatarishi kama Dar, kuna kila aina ya starehe na walimu wa kila somo.🤣

Yani mpenzi hata awe decent kiasi gani akiingia tu bandari salama lazma atiwe nyavuni. Oya kuna watu hawaangalii sura amini kwamba tena wanaotoka mikoani ndio huwa so vulnerable.
 
Kwa mwanamke naona kinyume chake kuliko miji midogo mzee, ila kwa mwanaume ndo hakufai pisi ni nyingi na kali halafu rahiiiiiiisiii yani za kuzoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…