Look alike. . .

Look alike. . .

ha ha ha, hako katoto kana bahati.
Labda mama ake aliwapenda hao watu wakati mjamzito.

Kama bahati kweli kanayo. . . yani kila aendako anapendwa.

Hahahaha hamna bana. Wengine hata walikua hawajulikani kipindi hicho ila ndio kama hivyo kama ingewezekana kuwasingizia sidhani hata kama wangehangaika kukataa.
 
Nilikutana na mtu fulani, kafanana na sokwe huyo, ilibidi niondoke kimya kimya!
 
Kwahiyo wewe unavyompenda mama,dada na kaka zako kunakufanya kicheche? Maana kupenda sio lazima ngono ihusike.

Wabongo kiswahili chetu chembamba au niseme tunapenda kufikiri ya hovyo kuliko ya maana!! Mtoto kupendwa na wazazi wake, kwa mfano atasemaje, kama kupenda lazima kuhusishe ngono?
Msamahe bure yawezekana uwezo wake wa kufikiri umeishia huko.
 
Niambie kwanza. . .
Alafu huyo besti maridadi wako kanipandisha na barabara siku ya leo karibu kichaa kinipande.

Nitakwambia siku nyingine! Ila hata jina lako linanikumbusha monitress wangu wa A-level, alikuwa anapenda kunitania na kiredio changu nilichokuwa simalizi muda bila kukiwasha!! Alafu nilivyokuwa doja wa vipindi, yaani ilikuwa ukifika muda flani sijarudi bwenini........utasikia anakuuliza, kulikoni mpaka mida bado upo au redio haina betri? (hapo pengine na ye anatafuta kampani lol) ....BTW, ndo maana nampenda besti....anajua kutumia vizuri muda wake!
 
Navutiwaga sana na vituko na shepu ya Anti Ezekieli (muigizaji). Mtaani kuna baa medi kafanana nae almost 95%, nimejikuta siichoki hiyo baa, na nikienda lazima nihudumiwe na yeye. Kama hayupo job namfatuta...
hmmm hii mupya!haya ukishamtafuta?
 
Napita wadau, uzi umetulia hadi raha!
Cha ku'share sasa! Kaputi !
Hayeni tanueni.
 
Wapo watu ambao hua tunawafananisha kwa muonekano, namna ya kuongea, kifikra au walivyo tu kiujumla na watu wetu wa karibu au tunaowafahamu tu.

Hii inaweza ikasababisha mtu akawa na hisia mbaya au nzuri sana na mtu asiemfahamu kwasababu tu anamkumbusha mtu ambae hayuko nae vizuri/yuko/alikua nae vizuri sana kimahusiano, awe rafiki, ndugu au hata mpenzi.

Swali langu ni je, umewahi kujikuta unampenda mtu kwakua anakukumbusha mtu fulani ambae inawezekana yuko mbali sana na ulipo wewe au hata alishaaga dunia hii?

Nimeipenda hii sred Malkia

Binafsi sijawahi...
Ila nadhani nimekuwa nawasababishia watu huo mkanganyiko wa kunifananisha na watu wao...
Cha kuchekesha wengi walionifananisha na "watu wao" niliishia nao kwenye mahusiano ya zaidi ya urafiki wa kawaida, ila ni katika mazingira tofauti-tofauti!!!
 
Mimi ni juzi juzi tu nilikuwa pale Mattako Bar kuna mdada mmoja akanifanisha na mtu fulani anaitwa X nikamwambia sio mimi akarudi kwenye meza yake akakaa. baada ya kama nusu alinifata tena akisisitiza mbona tuko copy kabisa na huyo jamaa (nahisi amepotezana mawasiliano kwa muda mrefu na huyo mtu ) nikaendelea kusisitiza sio mimi, basi akaniomba nimjoin mezani kwake.

Kilichofuata pale yule Mdada alicover all expenses tulizokuwa tunatumia pale yaani chakula na vinywaji mpaka nikapata wasi wasi may be something is cooked against me, ndipo nilipoamuwa kuwapigia jamaa zangu ambao ni Military oficers na hawakuwa mbali ili waje nihame nao sehemu nyingine na gari yangu, then tuliachana kwa style hiyo na siko interested kuchat na huyo mdada she scared me for realy.
 
Nimeipenda hii sred Malkia

Binafsi sijawahi...
Ila nadhani nimekuwa nawasababishia watu huo mkanganyiko wa kunifananisha na watu wao...
Cha kuchekesha wengi walionifananisha na "watu wao" niliishia nao kwenye mahusiano ya zaidi ya urafiki wa kawaida, ila ni katika mazingira tofauti-tofauti!!!

Hahahahaha jG bana. . .
Kwahiyo hayo mahusiano hua yanakaa lakini au ndo hata wakati wa kuachana unatupiwa "NILIKUFANANANISHA TU!!" ??LOLZZ

Missed you alafu.
 
Back
Top Bottom