kuna stori ya jamaa mmoja ilikuwa hivi:-
Jamaa alikuwa kiwembe sana anakula mademu kama chizi, sasa kuna duka moja alikuwa anapenda sana kwenda kununua condoms, na hilo duka alikuwa anauza mama wa makamo. Maisha yakaendelea kama miaka miwili hivi kwenye mizunguko huko jamaa akawa amekutana na binti mmoja wakawa wamependana mpaka kufikia kuamua kwenda kutambulishana. Kumbe yule binti mama yake ni yule mwenye duka ambalo jamaa alikuwa ananunua condoms. Ikafika siku ya kijana kwenda kujitambulisha kwa akina binti, yuko na mshenga wake wamekaa sebuleni, mara wanaingia wazazi wa binti, kijana uso kwa uso na yule mama, kumbukumbu ikamjia ghafla, na yule mama akaonyesha kushtuka sana......................sasa pata picha kilichoendelea hapo