Looking for part-time job

Looking for part-time job

JituParaTupu

Member
Joined
Nov 20, 2008
Posts
92
Reaction score
9
Wakuu,

Natafuta "Part-time" job inayohusiana na Inventory Management. Ningefurahi sana kama ningepata katika kampuni ya TBL hasa wakati wa stock-taking exercises (Perpetual or annual) ambayo niko mahili nayo sana. Niko "literate" na package ya SAP ambayo nadhani TBL wanaitumia. Nataka msaada wenu ili niweze kuongeza kipato kidogo wakati nitakapokuwa kwenye likizo yangu ya mwaka.

Natanguliza shukrani na najua hapa jamvini pana kila msaada na najua nitasaidiwa. Asanteni.
 
Maadam umeshajichagulia TBL, manake ni kuwa hutaki sehemu nyingine. (Au mkuu unapenda kuutandika mtungi wa bure?).TBL iko wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. Iko karibu na shule ya Uhuru upande wa kulia wa Uhuru Road kama unaelekea Buguruni. Fika getini uwaulize walinzi wakuelekeze mhusika akusaidie. Tunakuombea kila la kheri.
 
asee mkuu nasikia pale TBL hakuna kunywea kwenye glass, yani unafungua bomba na unamimina kwenye bilauri!!, kitu cha motooo.
 
Inventory Management

Hii Kazi anaweza pata hata Muhimbili Hospital ama kwenye Kambi ya Jeshi Kule Mbagala, ila mkuu anataka tu TBL!
 
Huyu akipewa pande East Africa Breweries Ltd hakatai lazima ni mlevi!
 
ama kwenye Kambi ya Jeshi Kule Mbagala

Mpwa nina utaalamu kama wa Jeetu Para tupu i mean invetory management, unamjua mtu anayeweza kunifanyia mipango kwenye kambi hiyo na mimi nipige part time pale, nasikia kuna deal sana.
 
Nitakuja jina la kamanda mmoja, mtalaam wa milipuko!
 
Mkuu huyu jamaa tumshauri atumie jina ulilompa, hilo la kwake labda akafanye inventory management pale Muhimbili National Hospital Mortuary.
 
Shukran in advance mpwa, sasa inabidi nianze kujifua kwa kutembelea pande za kunduchi au tegeta kwenye machimbo ya kokoto maana huko si ndio kuna milipuko ya baruti?
 
Mimi si mnywaji wa kilevi cha aina yoyote ile. Ila nimependa kufanya TBL kwa sababu ya kupractise package ya SAP. Huko Muhimbili au jeshini sidhani kama wana hii package. Hata hivyo nawashukuru.
 
Shukran in advance mpwa, sasa inabidi nianze kujifua kwa kutembelea pande za kunduchi au tegeta kwenye machimbo ya kokoto maana huko si ndio kuna milipuko ya baruti?
teh teh teh
 
utapata kaka, we jipe moyo tu. unajua tatizo ni kwamba utaratibu wa part time jobs kwa tanzania bado haujakolea sana lakini usikate tamaa.
 
Back
Top Bottom