Lori lafeli breki na kuua 11 Tanga

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Watu 11 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga Watu waliokuwa wakishangaa ajali ya gari dogo aina ya Tata katika Kijiji cha Changombe, Kata ya Segera, Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kwa sababu waliofariki walikuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.

Lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea Tanga, lilifeli breki na kuwagonga Watu waliokuwa pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya Watu 11 papohapo na kujeruhi wengine 11.

Mkuu wa Mkoa ametoa pole kwa Familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote na ametoa wito kwa Madereva na Wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hii.

 
Pole Yao lakini waishakatazwa kupenda kushuhudia maajali any way wapumzike Kwa aman
 
Wakati mwingine wanasaidia mkuu

Kama KUNA MAJERUHI rahisi kuwaokoa
Wezi tu hao wameenda kuvaa maroho ya mauti hatimae wametwaliwa. Ila jina lako mkuu c ungejiita ata baltazal 🤣
 
Wezi tu hao wameenda kuvaa maroho ya mauti hatimae wametwaliwa. Ila jina lako mkuu c ungejiita ata baltazal 🤣
Hahaaa Feb ntaitwa
Sio Mimi
MKUU
Mabadiliko yako brella wanalifanyia kazii
 
Naambiwa ni Segera.
 
Ila handeni 🤲
 
Habari ya kusikitisha sana hii, na sio mara ya kwanza ajali kama hiyo kutokea Handeni

Ila lori namba B, bado lipo barabarani kupakia mizigo mizito?
 
Kafara
 
Barabara ya tsnga inaua sana watu.....🙂 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…