Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Watu 11 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga Watu waliokuwa wakishangaa ajali ya gari dogo aina ya Tata katika Kijiji cha Changombe, Kata ya Segera, Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kwa sababu waliofariki walikuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.
Lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea Tanga, lilifeli breki na kuwagonga Watu waliokuwa pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya Watu 11 papohapo na kujeruhi wengine 11.
Mkuu wa Mkoa ametoa pole kwa Familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote na ametoa wito kwa Madereva na Wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hii.