Polisi wa doria ya mipakani nchini Afrika Kusini wamekamata lori lililokuwa likitokea nchini Malawi likiingia nchini humo likiwa limesheheni dawa za kulevya zenye thamani ya karibu randi bilioni moja (sawa na dola milioni 61). Katika msako huo, vikosi vya usalama viligundua zaidi ya kilo 700 (pauni 1,540) za kemikali ya methaqualone, ambayo hutumiwa kutengeneza dawa za kulevya za Mandrax zinazolevya kwa kasi kubwa, kwa mujibu wa mamlaka ya mipaka.
Taarifa iliyotolewa ilieleza kuwa thamani ya soko ya mzigo huo inakadiriwa kufikia karibu randi bilioni moja.
Msemaji mmoja ameiambia chombo cha habari AFP kuwa raia wawili wa Malawi na raia mmoja wa Zambia wamekamatwa kufuatia tukio hilo.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kumekuwa na angalau matukio manne makubwa ya kukamatwa kwa viwanda vinavyotengeneza dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, yakihusisha raia wa Mexico; hali inayozua mashaka kwamba mitandao ya kulevya ya Mexico (cartels) inajaribu kujisika na kuweka mizizi katika ukanda huo.
Shirika la kimataifa linalopambana na uhalifu wa kupangwa lenye makao yake makuu Geneva (Global Initiative Against Transnational Organized Crime), lilisema katika ripoti yake ya Julai 2025 kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la viwanda vya siri vya "Mexican meth" duniani kote katika muongo mmoja uliopita.
Mnamo Julai 2024, kikosi kazi maalum cha polisi wa Afrika Kusini maarufu kama 'Hawks', kiliwakamata raia watatu wa Mexico kwenye uvamizi uliofanyika katika kiwanda cha dawa za kulevya kwenye shamba moja karibu na mji wa Groblersdal, umbali wa takriban kilomita 200 kutoka Johannesburg, ambapo walikamata dawa za kulevya aina ya methamphetamine zenye thamani ya trakriban randi bilioni mbili.
Source: TRT AFRIKA