LOS BLANCO'S (REAL MADRID FC) klabu Bora ya Dunia ya wakati wote

United ya Ferguson

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
3,132
Reaction score
6,353
Kwenye mchezo wa golfu Kuna fundi mmoja alitawala mchezo huo Kwa kipindi kirefu sana alimarafu kama Tiger woods wazungu wanaita GOAT greatest of all time . kweny mchezo wa tennis Kuna fundi mmoja anaitwa Norvark jorkovick Kwa wapenzi wa tennis nazan wanamfahamu huyu mwamba Raia wa Serbia .katika umri wa miaka 34 ameweza kufanya mambo makubwa mengi sana hatuwezi kumaliza CV yake hap.

Kwenye mchezo pendwa zaidi Dunia mchezo wa soka wenye mashabiki takribani bilioni 5 kweny mchezo huu Kwa ngazi ya vilabu Kuna klabu moja marufu Kwa jina la Los Blanco's au Kwa jina la Real Madrid yenye maskani yake pale Santiago bernabeu jijini Madrid huko nchini Hispania
ilioyoanzishwa mnamo tarehe /6/3/1902.Real madrid ndio klabu Bora ya wakati wote ya Dunia.kuna sababu nyingi sana zilizopelekea Real Madrid kuwa klabu Bora ya Duniani

Real Madrid na ligi ya mabigwa barani ulaya, michuano Bora zaidi barani ulaya Kwa ngazi ya vilabu ikiwakilishwa na vilabu vinavyoshika nafasi za juu katika ligi kuu za nchi wanachama wa UEFA Huku mwanzo ikifamika kama European cup.kabla ya kuja badilishwa jina na kuitwa UEFA champions leuage.Real Madrid ndio klabu pekee kutoka barani ulaya iliyoshiliki michuano hii mara yingi zaidi Huku ikishiliki zaidi ya mara 50 .pia Real ndio klabu pekee imeshinda taji Hili mara nyingi wakifanikiwa kutwaa taji Hilo mara 13 taji la kwanza wakishinda mwaka1956,1957,1959,1960,1966,1998,2000,2002,2014,2016,2017,2018

Ballon dor , tuzo za jarida la michezo la ufaransa marufu kama France magazine tuzo hizi pia hutambulika kama tuzo za mchezaji Bora wa mwaka wa Dunia zilizoanzisha mwaka 1956.Real madrid ndio klabu pekee Duniani iliyotoa washindi wengi zaidi wa tuzo hizi wengi zaidi ikiwa imefanya hivyo mara 11 huku.Gwiji wa zamani wa klabu hiyo Alfredo di Stefano akitwaa tuzo hiyo mwaka 1957,
Raymond kopa1958 akitwaa tuzo hiyo kutoka Real madrid 1959 Alfredo di Stefano alishinda tuzo kwa mara nyingne tena.Los Blanco's iliwachukua takrilibani miaka 40 kuja kutoa mshindi wa tuzo hiyo tena mwaka 2000 fundi wa mpira wa miguu Luis Figo alishinda tuzo hiyo akiwa na Real Madrid . Ronaldo de Lima mwaka 2002 akiwa na Real Madrid .2006 Beki kisiki Raia wa Italy Fabio canarvallo akishinda tuzo hii.Nyota aliyevunja rekodi ya usajili mwaka 2009 Cristiano Ronaldo akitokea old Trafford Kwenda Santiago bernabeu alishinda tuzo hiyo mwaka 2013,2014,2016,2017 na mwaka 2018 Luka modric Rai wa Croatia akishinda tuzo hiyo kutoka Real Madrid

Tuzo ya klabu Bora ya Karne ya 20 ya FIFA,Gwiji wa soka wa zamani Alfredo di Stefano na Florentino Perez Rais wa Real Madrid mwaka 2000 walikabiziwa tuzo ya heshima na FIFA ya klabu Bora ya kutoka mwaka 19000 hadi 2000 .Halfa hizo za ugawaji wa Tuzo hizo zilfanyika jijini Rome nchini Italy . Manchester united kutoka ardhi ya malikia wakishika nafasi ya pili wakifwatiwa na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani

Klabu bigwa ya Dunia , michuano inayowakilishwa na mabigwa wa klabu bigwa za mabara mbalimbali duniani kama ulaya,america ,Africa ,Asia,n.k .iliyochini ya shirikisho la soka la mpira la Dunia FIFA Real Madrid ndio klabu pekee iliyoshinda taji Hilo mara nyingi zaidi ukilinganisha na vilabu vingine ikiwa imeshinda mara 4 mwaka 2014,2016,2017,2018

Galatico,neno la kispanishi lenye maana ya a super star sera hii ilianzishwa na Raisi wa klabu hiyo Florentino Perez mwaka 2000 sera hii ikijuisha sajili za wachezaji wenye majina makubwa Dunia kwenda kucheza bernabeu Kwa lengo la kufanya Real Madrid kuwa klabu ya kiushindani barani ulaya na duniani Kwa ujumla huku first Galatico ilikuwa ni kutoka mwaka 2000 hadi 2006 Real Madrid ikifanya sajili zilizovunya Rekodi ya Dunia ikiwemo usajili wa Luis Figo kutoka Barcelona ,Zinadine zidane,Aliyevunja rekodi ya usajili wa DuniaKwa kipindi hicho,Ronaldo de Lima,David, Beckham, Micheal Owen,. Sergio Ramos .n.k Kwa kipindi Cha mwaka 2000 hadi 2006 Cha uongozi wa Perez walifanikiwa kutwaa Mataji mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabigwa barani ulaya,kombe la ligi kuu Hispania n.k
Second Galatico hii ilikiua kipindi Cha awamu ya pili ya uongozi wa Florentino Perez baada ya kurejea klabuni hapo mwaka 2009 akifanya sajili za wachezaji kama Ricardo kaka kutoka Ac Milan , Cristiano Ronaldo,Karim benzema,Xabi Alonso na miaka ya 2010 na kuendelea akifanya sajili za kina Angel dimaria,meust ozil,Isco, Gareth bale,Luca modric,Toni kroos n.k Huku Real Madrid walifanikiwa kutwaa Mataji mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabigwa barani ulaya mwaka 2014,2016,2017,2018 ligi kuu Hispania, super cup n.k

Santiago bernabeu, uwanja wa nyumbani wa klabu ya Real Madrid ulioanza kujengwa mnamo mwazoni mwa miaka ya 1940s.Moja kati ya uwanja unaokwenda kuwa Bora barani ulaya na duniani Kwa ujumla badaa ya matengezo yake kumalika ambapo Kwa Sasa upo Kweny matengezo yaliyoigharimu Real Madrid takribani Euro million 800.pia Real Madrid wamesani mkataba wa kukodisha uwanja Kwa kampuni ya matamasha ya kimerani Kwa kitita Cha paund million 400 Kwa mwaka.pia uwanja huu unakumbukwa Kwa kuweza kuandaa fainali kubwa za michuano mbalimbali ikiwemo fainali ya kumbe la Dunia mwaka 1982.fainali ya michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 1964 fainali za ligi ya mabigwa barani ulaya mwaka 1957,1969,1980 na mwaka 2010.bila kusahu fainali ya michuano ya klabu bingwa ya america ya kusini kati ya Boca Juniors na River plate mwaka 2018

Kwa kifupi tuseme Aporla 14
 
Real madrid walipotea wakarudi kwa kasi ya ajabu mno. Walivyopotea ilibakia kidogo tu tuikute record yake ya champions league ilikuwa makombe mawili ty ( makombe 9 vs 7) lakini cha ajabu badala ya kuwakuta tukapotea sisi mazima hadi leo hii tumewaacha ma legend wenzetu wa champions league wanatamba tu. Dah rossoneli embu rudisha makali yako yale ambayo kila timu ikisikia kapangwa na Ac Milan anaanza kuweweseka tu kwamba hapa safari imewadia.
 
Hebu tukumbushe habari ya usiku wa maaajabu pale Arturk stadium pale Istanbul,mjii uliokaa juu ya mabara mawili.2005 hiyoo
 
Hebu tukumbushe habari ya usiku wa maaajabu pale Arturk stadium pale Istanbul,mjii uliokaa juu ya mabara mawili.2005 hiyoo
Dah nili enjoy sana kipindi cha kwanza furaha isiyo na kifani. Siku hiyo nilisema kimoyo moyo hawa majogoo watajuta kukutana na timu inayoogopwa ulaya. Kikosi cha rossoneli kilikuwa na watu haswa
Dida, Cafu, kipara Stam, Nesta,Paulo Maldini,Gatuso, Seedorf, Kaka,Crespo na Shevchenko
Hawa watu walikuwa ni watu wa kazi haswa mkuu yaani kama shabiki wa Milan unasubiri tu kusikia nani kaletwa mbele yako halafu unabaki kumuonea huruma tu.

Yap upande wa Liverpool: Dudek, Finnan, Carragher, Hyypia, Traore, Garcia, Gerrard, Alonso, Riise, Kewell na Baros.


Dakika ya kwanza tu Paolo Maldin anapiga bonge la volley kwenye 12 yard na kuiandika Milan goli la kwanza

Dakika ya 38 Crespo anaipatia Milan goli la pili sekunde chache baada ya Liverpool kunyimwa penati baada ya mpira kugusa mkono wa Nesta

Dakika ya 44 Crespo tena anaingia nyavuni kupigilia chuma cha tatu. Aisee nilifurahi sana kwa sababu mbali na kushinda goli tatu Ac Milan wali offer classic performance yaani ulichezwa mpira sio wa kawaida. Tukaenda mapumziko kwa kuongoza goli 3 kwa 0 kila mtu aliamini kazi imeisha. Nahisi hata wachezaji na benchi la ufundi likiongozwa na huyu mwamba aliyeko Bernabeu (Ancelotti)


Kipindi cha pili:

Benítez alifanya mabadiliko ya kumtoa Steve Finnan na kumuingiza Didi Hamann, bwanawe tukapigishwa gwaride la kufa mtu huku tukipaki masemi trailer kama unakumbuka kipindi hicho Ac Milan ilisifika kwa kuwa na ukuta wa chuma lakini dakika ya 54 Steven Gerrard anaipatia Liverpool goli la kwanza kwa kuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa cross na John Arne Riise. Mzee ngoma ilipinduka aisee watu wakawa wanapelekewa moto hatari, dakika mbili tu baada ya kwanza, Vladimir Smice anatandika bonge la shuti la mbali na kufanya ubao uwe Liverpool 2 Milan 3. Mashabiki wa Liverpool waliamka na kushangilia sana waliona inawezekana kufanya come back ya kukomboa magoli yote matatu. Upande wa Milan kwanzia mashabiki mpaka wachezaji walipagawa na hali ukizingatia Liverpool waliutawala mchezo kipindi cha pili chote halafu wao hawakuwa na utulivu.

Dakika ya59 Gatuso anafanyia faulo Gerrard ndani ya 18, Alonso anapiga penati kipa anapangua na kumkuta tena anamalizia na kuweka kambani goli la tatu
Ngoma tatu tatu aisee Ancelotti aliiishia kutafuna bablishi tu hajua hata nini cha kufanya.

Ngoma ikaanza na upya kwenye dakika 30 za nyongeza na hakuna aliyeweza kupata goli dakika 30 hivyo penati ndio zilizoamua bingwa ambapo Liverpool wakanyanyua kombe.

Ni fainali iliyoiweka kumbukumbu njema kwa Liverpool ila kwa Ac Milan ilikuwa ni kumbukumbu mbaya sana kwao
 
Mimi kama kop,kipindi cha Kwanza nilikosa raha kabisa,watu wakaanza kusema bora tungewaachia Chelsea.Magoli yalipoanza kurudi raha ikarejea.Anyway pole Sana mkuu.
 
Ligi yao ni ya timu mbili ukikosa ubingwa utashika nafasi ya pili


Je wataacha vp hapo kushiriki mara nyingi uefa
 
Ligi yao ni ya timu mbili ukikosa ubingwa utashika nafasi ya pili


Je wataacha vp hapo kushiriki mara nyingi uefa
Juventus,AC Milan,Inter Milan na Roma hizi si timu ndogo na kwahiyo ligi yao si ya timu mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…