Lost Book of Black People

Lost Book of Black People

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Za leo ndugu zangu wana JF:
Leo ninapenda niongelee kitu ambacho nimekuwa nakifuatilia kwa muda mrefu. Imenibidi nikusanye researches zangu zote niweze kuziweka hapa.

TAMADUNI ZA MTU MWEUSI
Nimefuatilia kwenye tamaduni mbalimbali za mtu mweusi nimekutana na ufanano wa mambo mengi sana. Moja ya ufanano wa mambo ni kuptia katika imani zao. Watu weusi walikuwa na imani zinazofanana hususani kuamini kuwa yupo mwenye nguvu zaidi ambaye hatumuoni.

Imani hiyo ilikuwa presented kwa kupitia vitu vinavyoonekana. Si kwamba watu weusi walikuwa wanaabudu miti, milima au jua bali walikuwa wanapitisha hisia zao za imani kupitia vitu vinavyoonekana.

Watu weusi wamekuwa wakitumia dawa za miti kwa miaka mingi sana. Imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.

SAFARI YANGU YA KWENDA UGRIKI, ITALIA, IRAN NA UJERUMANI KUFANYA UTAFITI

Niliamua kufunga safari ya kiutafiti na kwenda kwenye nchi hizo tajwa. Hii ni kutokana na kwamba
1. Ugriki ndio nchi ilikuwa na watalamu na wameandika vitu vingi sana kuhusu dunia
2. Italia ilikuwa na utawala mkubwa sana hapa duniani na imeathili tamaduni nyingi kupitia Roman Empire.
3. Iran ni kutokana na kwamba waajemi wameongiliana sana na waafrika katika biashara mbalimbali
4. Ujerumani ni moja ya mataifa yaliyoshiriki katika kuligawa bara la africa

Periplus of the Erythraean Sea
Hiki kilikuwa kitu changu cha kwanza kufanyia utafiti. Periplus of the Erythraean Sea maana yake voyage of the Erythraean Sea. Erythraean sea ili husisha Red Sea, Arabian Sea, Persian Gulf, and Indian Ocean.
Ndani ya bahari hiyo kulikuwa na bandari kubwa kubwa msafiri wa kipindi hicho cha 1 CE alizitaja.
Moja ya bandari iliyotajwa katika kitabu hicho cha safari ya baharini ni Rhapta.

Lakini kuna bandari nyingine liyotajwa kwenye kitabu hicho iliyoitwa Muza na kwa sasa eneo hilo linaitwa Yemen.
Sasa nimekusanya taarifa nyingi ambazo zinaeleza kuwa Tanzania ambayo katika kitabu hizo ilijulikana kama Azania na mji wake Mkubwa kabisa kando kando ya bahari uliitwa Rhapta, kuonesha kitabu kilichopotea cha mtu mweusi.

Kitabu hicho kina mambo mengi nitayaeleza kituo kwa kituo.
Huu ulikuwa utangulizi uwe macho nitakavyoendelea kukielezea kitabu hicho na maeneo ya masalia yake yalipoweka na kufichwa.
 
KITABU GANI UNAKITAFUTA?
Baada ya kusafiri huku na huku kutafuta ukweli wa mtu mweusi. Niliweza kufika huko Italia. Lengo langu lilikuwa ni kwenda kufika huko vatican maana kuna historia ya mambo mengi sana ipo huko.

Lengo langu lilikuwa siyo kujua jamii nyingie duniani bali ni kujua ukweli kuhusu watu weusi.
1. Nilikutana na watu mbalimbali wakanizungusha kwenye makumbusho mbalimbali ya tamaduni za dunia jinsi walivyozihifadhi. Lakini ilipofika kwa mtu mweusi nilkutana na kumbukumbu zilizoandikwa na wao hao wazungu. Kumbukumbu hizo zilikuwa za kukatisha tamaa maana zinaonesha ubaya wa watu weusi pekee.

Iliniuma sana kuona safari yangu kufika huku nimekuja kukutana na vitu vya ajabu hivi?

Kuna mwana zuoni mmoja huko Italia akaniambia kwanini unatafuta historia ya mtu mweusi? Kama unataka kuipata historia yenu mpo nayo huko huko afrika imefichwa

Kwakweli nilitafuta namna ya kumuelewa huyu jamaa. Sikumuelewa kiindi hicho. Baadaye akaniambie wewe unatafuta Historia ya mtu mweusi kwa kutumia mentality ya watu wa magharibi. Huwezi ukaipata kwa namna hiyo. Huku kwetu hakuna kitabu kitamuelezea mtu mweusi kama mtu. Hata kama tutamwelezea kuwa mtu mweusi ni mtu basi tunamwelezea kuwa huyu amelaaniwa.

Safari yangu ya kwenda italia iliishia hapo ikabidi nirudi Tanzania, kufanya biashara za hap na pale ili niweze kupata pesa zingine zinisaidie kwenye kufanya utafiti zaidi. Wakati nikiwa hapa Tanzania:-

MAPANGO YA KONDOA
Nilipokuwa hapa Tanzania nilipata wazo la kwenda kwenye mapango ya Kondoa. Nilienda huko na kwenda kufanya utafiti wangu. Niliweza kuitembelea michoro yote. Kisha nikaja kuanza kuidadavua.

Michoro hiyo inaonyesha watu warefu, wanyama na matukio ya uwindaji. Nikaweza kutafakari kwa kina. Maeneo hayo lipo kabila la wasandawe. Likini kuna utamaduni wao wa kuomba mvua, utamaduni huo unafanana kabisa na tamaduni za wabatu.

Kwa namna hiyo nilikuwa kujifunza huenda Wasandawe na Wabantu wapo na uhusiano.

Naomba muendelee kunifuatilia...
 
kimepoteaje au kimejipoteza chenyewe
GSY2ZwAWwAAXivk.jpg
 
Tupo hapa tukikusubiri...ila najua ukitaka kila ukweli wa Mtu mweusi nenda kwa Nubians na Kush...wapo Ethiopia, Sudan na Egypt....na Libia ya zamani kabla ya kuvamiwa na Mroma
 
SANAMU NYINGI ZA WATAWALA WA ZAMANI WA MISRI KUVUNJWA PUA
Baada ya kupata taarifa kutoka kwenye mapango ya Kondoa, ilinibidi nisafiri kwenda misri kwenda kujifunza zaidi. Nilipofika kule kuna mambo mengi sana ya kushangaza niliyaona.

Sanamu za watawala wa mwanzoni kabisa nchini misri pua zao zimevunjwa.

Khasekhemwy alitawala kuanzia mwaka 2690 BC. Sanamu yake pua imevunjwa

1720959854739.png

Sikuweza kupata jibu. Niliona labda ni kwa bahati mbaya.

Mtawala aliyefuata baada yake Djoser Vilevile sanamu yake pua imevunjwa

1720959956360.png

Nipo na picha nyingi hapa nawaomba wenzangu muweze kuzipitia pua zao zimevunjwa:

Huni

1720960071267.png

Djedefre

1720960205208.png

Nyuserre Ini​

1720960280807.png
 
Za leo ndugu zangu wana JF:
Leo ninapenda niongelee kitu ambacho nimekuwa nakifuatilia kwa muda mrefu. Imenibidi nikusanye researches zangu zote niweze kuziweka hapa.

TAMADUNI ZA MTU MWEUSI
Nimefuatilia kwenye tamaduni mbalimbali za mtu mweusi nimekutana na ufanano wa mambo mengi sana. Moja ya ufanano wa mambo ni kuptia katika imani zao. Watu weusi walikuwa na imani zinazofanana hususani kuamini kuwa yupo mwenye nguvu zaidi ambaye hatumuoni.

Imani hiyo ilikuwa presented kwa kupitia vitu vinavyoonekana. Si kwamba watu weusi walikuwa wanaabudu miti, milima au jua bali walikuwa wanapitisha hisia zao za imani kupitia vitu vinavyoonekana.

Watu weusi wamekuwa wakitumia dawa za miti kwa miaka mingi sana. Imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.

SAFARI YANGU YA KWENDA UGRIKI, ITALIA, IRAN NA UJERUMANI KUFANYA UTAFITI

Niliamua kufunga safari ya kiutafiti na kwenda kwenye nchi hizo tajwa. Hii ni kutokana na kwamba
1. Ugriki ndio nchi ilikuwa na watalamu na wameandika vitu vingi sana kuhusu dunia
2. Italia ilikuwa na utawala mkubwa sana hapa duniani na imeathili tamaduni nyingi kupitia Roman Empire.
3. Iran ni kutokana na kwamba waajemi wameongiliana sana na waafrika katika biashara mbalimbali
4. Ujerumani ni moja ya mataifa yaliyoshiriki katika kuligawa bara la africa

Periplus of the Erythraean Sea
Hiki kilikuwa kitu changu cha kwanza kufanyia utafiti. Periplus of the Erythraean Sea maana yake voyage of the Erythraean Sea. Erythraean sea ili husisha Red Sea, Arabian Sea, Persian Gulf, and Indian Ocean.
Ndani ya bahari hiyo kulikuwa na bandari kubwa kubwa msafiri wa kiindi hicho cha 1 CE alizitaja.
Moja ya bandari iliyotajwa katika kitabu hicho cha safari ya baharini ni Rhapta.

Lakini kuna bandali nyingine liyotajwa kwenye kitabu hicho iliyoitwa Muza na kwa sasa eneo hilo linaitwa Yemen.
Sasa nimekusanya taarifa nyingi ambazo zinaeleza kuwa Tanzania ambayo katika kitabu hizo ilijulikana kama Azania na mji wake Mkubwa kabisa kando kando ya bahari uliitwa Rhapta, kuonesha kitabu kilichopotea cha mtu mweusi.

Kitabu hicho kina mambo mengi nitayaeleza kituo kwa kituo.
Huu ulikuwa utangulizi uwe macho nitakavyoendelea kukielezea kitabu hicho na maeneo ya masalia yake yalipoweka na kufichwa.
Barikiwa mkuu

tuna subili
 
Ukweli wa Mtu Mweusi
Ndugu zangu ilinibidi sasa kuanza kuchimba kwa undani zaidi ili niweze kuanza kupata ukweli. Hivi kweli sisi watu weusi hatuna historia ya maana? Maana historia tunazozipata ni baada ya kuja wakoloni na watawala kutoka nchi zingine.

Eti historia yetu inaanza baada ya waarabu na kusambaa kwa dini ya kiislam, ambayo ilienea kwa kasi sana mpaka kule Mali Empire!!!

Kusema ukweli mtu mweusi alikuwepo kabla ya kuja kwa hawa watawala na kulikuwa na civilization kubwa tu.

Mtu mweusi hukufundishwa na wazungu namna ya kufuga mifugi, mtu mweusi hakufundishwa na wazungu teknilojia ya kujenga nyumba. Kwahiyo kabla ya wageni kuja kwetu tulikuwa tayari tupo na maisha yetu na historia zetu.

HISTORIA YETU ILIANDIKWA WAPI
Mtu mweusi alikuwa anaoitisha utamaduni kutoka kizazi kwenda kizazi kwa njia:-

1. Kuandika michoro kwenye miti, mawe na ngozi za wanyama.

2. Kupitia nyimbo mbalimbali

3. Kupitia hadithi zilizokuwa zinasimuliwa kutoka wazee

4. Kupitia mafunzo ya vijana yaliyokuwa yanaandaliwa kwanye jamii husika.

Maandishi na michoro iliyokuwa imeandikwa kwenye miti, mawe na ngozi mpaka sasa ipo

KUKUA KWA MJI WA KIBIASHARA RHAPTA

Tafiti zinaeleza kuwa mnamo karne ya kwanza, kulikuwa tayari na mji mkubwa wa kibiashara katika pwani ya Tanzania uliokuwa unaitwa Rhapta. Utafiti unasema kuwa mji huo ulikuwa kando kando ya mto rufiji.

Kwenye delta za mto Rufiji tafiti zinaeleza kuwa kulikuwa na mji mkubwa wa kibiashara.

Kula kwanza hicho kisha nikuletee zaidi kuhusu rhapta...*
 
LOCATION OF RHAPTA
1720968019355.png

Aprili 2016 Alan Sutton, a South African diver living in Tanzania aliweza kuona masalia ya misingi ya majengo. Na katika kuangalia hayo yalionekana kuwa ilikuwa misingi ya nyumba.

Kutokana na msafiri wa kigiriki kuelezea kuwa kulikuwa na mji wenywe bandari na kando ya mji huo kulikuwa na mto mkubwa, ilifanana kabisa na huyu mwageleaji aliyezama na kuona hiyo misingi ya majengo.

Kwakuwa maji yalikuwa yakikupwa na kujaa. Walisubiri kipindi maji yakiwa yamepungua eneo hilo. Waliweza kuruka na helkopita kisha kuchunguza eneo hilo. Kweli waliona misingi na matofari makubwa ya majengo.

Mpaka sasa haijulikani kipi kilitokea mpaka mji huo ukazama baharini.

Mimi ninaendelea na uchunguzi zaidi. Mwezi wa 11 mwaka huu nimeamua kwenda katika eneo hilo na vyombo vya kisasa vya kiteknolojia vyenye kutazama mitetemo na kujua ni miaka ipi kulikuwa na watu kiasi gani. Vilevile kuweza kuona masalia ya mifupa na kuweza kupima DNA zake.
 
Pia Nilisoma sehemu kuna mwanafunzi wa udsm from Kenya if not mistaken aliombwa na Prof wake afanye research ya huo mji wa Rhapta. Problem ya historia ya mtu mweusi yote imeandikwa na walio na wanaoendelea kutukandamiza so tusitegemee kuandikwa vzr.
 
Kuna clip moja ya watu wa Asia sijui specifically ni nchi gani, ni shule walikua wanawafundisha wanafunzi somo la communication skills, na sub topic ni kuhusu jinsi upashwaji wa taarifa toka mtu na mtu unaweza kutofautiana mpaka mtu wa mwisho akapata taarifa isiyo sahihi kwa kutafsiriwa vibaya na watoa taarifa hapo katikati.

Kulikua na wanafunzi karibu 50, wote wametizama mbele. Yule wa mwanzo toka mwisho, alipewa taarifa ya signal na mwalimu wake kua sio muda mrefu atamumuua(ishara ya kuua kwa kukata shingo). Ile taarifa ilitakiwa ifike kwa mtu wa kwanza kule mbele kama ilivyo.

Ajabu ni kua kuanzia mtu wa 10 walianza kutoa signal tofauti kabisa, mpaka mtu wa 30, signal ikawa imebadilika toka kuua kwa kukata shingo mpaka alama ya dole gumba(kwamba huko nyuma mambo ni fresh)..

Mpaka yule mtu wa 1 anafikiwa signal aliyoipata hata yeye hakuielewa kabisa.
Mtu wa 50 na wa 1 wakakutanishwa yule wa 50 atoe ishara aliyopewa na mkufunzi na yule wa 1 toe ishara aliopewa na mtu wa 2.

Ilikua ni vituko, mtu wa 50 alicheka mpaka akakaa chini, kutoka ishara ya kuua mpaka ishara ya isiyoelewaka kabisa.

Na hivyo ndivyo wazee wetu walipokosea, unapotoa masilimulizi.. unayempa nae atampa atakaempa story tofauti na ile halisi.

Wenzetu walituzidi kwenye maandishi, sijui wavumbuzi halisi wa maandishi ila wazungu waliyatumia ipasavyo kujenga vizazi vijavyo.
 
Hawakufunuliwa upande huo
 
Back
Top Bottom