Loud speaker ilinifanya nijue fundi anatoka na jirani yangu

Loud speaker ilinifanya nijue fundi anatoka na jirani yangu

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kuna baadhi yetu hatujui ni wakati gani na mazingira gani tutumie loud speaker katika rununu zetu, kwakuwa ipo hiyo option basi wewe unatumia tu.

Kuwa muangalifu sana unapotumia loud speaker, ikiwa ni maongezi ambayo sio nyeti basi waeza kusikiliza ukiwa mbele za watu lkn kama ni mazungumzo muhimu na yenye usiri basi usitumie loud speaker mbele za watu

Inanikumbusha baba yangu mdogo ambaye ametangulia mbele za kazi, huko way back aliwahi kunionganisha na kazi moja ya supervisor wa hotel, basi akanipigia simu kunipa details za hiyo hotel khee kumbe kaweka loud speaker na yupo hadhir na boss mwenyewe!

Sasa mimi sina habar nikamuhoji mambo ambayo isingefaa boss kuyasikia toka kwa muajiri wake, lkn God is good nikapata kazi pale nikapiga miezi kadhaa.

Kwahiyo ni vizur sana kutumia loud speaker ili kupunguza madhara ya mionzi katika ubongo wetu,ndio maana mataifa yalio endelea wanapendelea sana text msgs

Sasa mchongo uko hivi sina hili wala lile nipo home mara nasikia tii tii tii tii mara pap jirani yangu anapokea simu ipo loud speaker fundi anampa maelekezo wakutane sehemu fulani, namsikia jirani yangu kwa roho safi kabisa anajibu kuwa mda si mrefu atakuwepo hapo.

Hayo ndio mambo ya loud speaker yakitumiwa vibaya,,nisingejua yaliyomo yamo kama si loud speaker ya fundi

Ni hayo tu!
 
Juzi juzi kuna mtu nilimuuliza mbona ghafla kumekuwa na ongezeko la watu wanaongea na simu kutumia loud speaker? Yaani watu hawaweki tena simu masikioni wanaishika mkononi mbele ya hadhara mazungumzo yote kila mtu anasikia? Why? Hakuna anaetaka kusikia mazungumzo yenu na hatuwezi kuziba masikio.
 
Kuna mjinga mmoja aliniweka loud speaker wakiwa kwenye kikao, baada ya kuniuliza maswali ndo ananimbia kua watu fulani wananisikia…. Fc him
 
Kuna mjinga mmoja aliniweka loud speaker wakiwa kwenye kikao, baada ya kuniuliza maswali ndo ananimbia kua watu fulani wananisikia…. Fc him
Kama inabidi kuweka loud speaker basi busara unamfahamisha mhusika kuwa nimeweka loud nipo na wadau hapa
 
Juzi juzi kuna mtu nilimuuliza mbona ghafla kumekuwa na ongezeko la watu wanaongea na simu kutumia loud speaker? Yaani watu hawaweki tena simu masikioni wanaishika mkononi mbele ya hadhara mazungumzo yote kila mtu anasikia? Why? Hakuna anaetaka kusikia mazungumzo yenu na hatuwezi kuziba masikio.
Na wengine wanakera wanaongea upuuzi mtupu

Just imagine watu wamekosa haya wanaweka loud katika daladala fc them
 
Back
Top Bottom