Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Louisiana imekuwa jimbo la kwanza nchini Marekani kutaka kila darasa la shule za serikali, kuanzia msingi hadi chuo kikuu kubandika Amri Kumi za Mungu ukutani.
Hatua hiyo iliyochochewa na chama cha Republican na kutiwa saini kuwa sheria na Gavana wa jimbo hilo Jeff Landry (pichani) siku ya Jumatano, inaelezea amri hizo kuwa ni “nyaraka za msingi wa taifa letu na serikali”.
Hata hivyo sheria hiyo inatarajiwa kupingwa mahakamani na makundi ya wanaharakati wa haki za kiraia, ambao wanasema inakinzana na kifungu cha kwanza cha katiba ya Marekani cha kutenganisha baina ya kanisa na mamlaka.
Shirika la Utangazaji la BBC limesema amri hizo lazima ziwe zimebandikwa kwenye madarasa ya shule zote zinazopewa fedha za umma ifikapo mwaka 2025.
Sheria kama hizo zimependekezwa hivi karibuni katika majimbo ambayo ni ngome za chama cha Republican kama vile Texas, Okhlahoma na Utah. Kumekuwa na mpambano mkali wa kisheria kuhusiana na suala la kubandika Amri Kumi kwenye ofisi za serikali kama vile shule, mahakama na vituo vya polisi. Mwaka 1980, Mahakama Kuu ilitupilia mbali sheria kama hiyo katika jimbo la Kentucky lililotaka amri hizo kubandikwa katika shule za elimu ya kati.
Pia soma:Kuna amri 10 za Mungu. Je,ikatokea fursa ya kupendekeza Amri ya 11. Wewe ungependekeza Amri ipi mpya?