Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jimbo la Louisiana limekuwa la kwanza nchini Marekani kuidhinisha sheria inayoruhusu kuhasiwa (kuwakata korodani) kwa wabakaji wa watoto, walio chini ya umri wa miaka 13 kama adhabu ya jinai.
Sheria hiyo, ambayo ilianza kutekelezwa Agosti 1, inawahusu wahalifu wenye umri wa kuanzia miaka 17.
Sheria imeruhusu majaji kutoa amri ya kuhasi kwa kutumia kemikali. Hata hivyo, kuna baadhi ya hali ambapo mhalifu aliyehukumiwa anaweza asistahili adhabu hiyo, jambo ambalo litabainishwa na jaji pamoja na daktari wa gereza.
Adhabu ya kuhasiwa pia inatumika katika nchi zingine zinazojulikana kwa vikwazo vikali zaidi vya uhalifu, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Czech na Nigeria.