Kama january hivi akaniambia hana hisia za kimapenzi tena kwangu. Sababu nilishaziona dalili toka mwanzo so haikunishtua sana japo "its hard to let go" nikamwambia sawa kama mapenzi yameisha basi nakuacha, uniache, tuachane! Badala yake akaniomba tuwe marafiki tu, nikamwambia haiwezekani. Mi toka siku ile nikaachana nae sikuhangaika kumpigia simu wala kumtext...
Tunakutana FaceBook kwenye (status) comment za marafiki zetu, sometime anaandika post kwenye wall yangu, so huwa inabidi nimjibu. Majuzi kama mwezi umepita akanitext kujua naendeleaje nikamjibu nipo poa nafanya vizuri.
Niwe muungwana kwa kukiri kuwa yule mtoto bado nampenda bado ila sina mpango wa kumlilia kwa penzi lake since ametamka kuwa "PENZI LAKE LIMEKWISHA", kinachoniweka kwenye mapenzi na mtu ni yeye anipende na mimi nimpende. Hiyo statement ndiyo inazunguka kichwani mwangu kilasiku na imenifanya nililete suala hili mbele ya WANAJAMII wenzangu mnisaidie kidogo, inakuwaje? eti mapenzi huwa yanakufa?
Kwa hii hali ndiyo maana nikasema "love; knocked me out"
Naomba kuwasilisha jamvini wana-JF.
Kama haupo interested potezea usizingue![/LEFT]