Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Niwe mkweli kabisa saa sita hii usiku nimekuwa inspired na uzi wa Robidinyo ambaye ameeleza changamoto ya kutokuwa na kazi au biashara jinsi maisha yanavyokuwa magumu.
Nikajikuta nataka kuwapa respect wale wote ambao hamchoki kutoa msaada kwa ndugu na jamaa zenu waliopata changamoto za hapa na pale,Mungu awape maisha marefu sana
Kwa kawaida mtu akikuomba msaada kwa kipindi kirefu sana huwa tuna kawaida ya kumchoka,na hapo tutaacha kupokea simu zake wala kujibu meseji zake na tunamuona msumbufu
Heshima za dhati kwako wewe ambaye pamoja na kuombwa msaada na mtu wako au jamaa yako wa karibu mara kwa mara lakini hujachoka kusaidia wala hujaacha kupokea simu za watu wako wenye shida wala kujibu meseji.
Wewe ni mtu wa maana sana unastahili medali ya dhahabu,niwaambie kitu?
Hakuna mtu ambaye anapenda kuwa omba omba tena mwenye familia ila ni shida tu imemkuta,ndio maana anajidhalilisha na kuomba msaada.
Hivyo ukimuona mtu anapenda mara kwa mara kukucheki ujue anajisikia comfortable kutaka msaada kwako,anaamini wewe ni mtu pekee ambaye unaweza kumstiri na kuficha aibu yake,basi nawe mstiri hakika hutujui kesho yetu
Binafsi nishawahi pitia hayo maisha najua yanatesa sana,una watoto halafu hujui kesho utakula nini,na ukila mchana hujui jioni utakula nini?
Nakumbuka kuna siku kumekucha mpaka mida ya saa nne asubuhi haikujulikana breakfast itapatikana wapi, Nina watoto wawili hapo,baby girl wangu analia njaa,,ukimtazama mama watoto analia hajui cha kufanya,,mara hapa na pale unamcheki mwamba unamuelezea changamoto yako mara paap muamala huu hapa,analeta tabasamu nyumbani.
Ninachotaka kusema baadhi yetu tumewahi kupitia katika changamoto na wengine wanapitia kipindi hiki,,kikubwa usikate tamaa God is always good,,ipo siku utakuja kusahau na kuwa historia
Wadau tafadhali msichoke kuwasaidia wenye shida tena wenye familia wanapitia kipindi kigumu sana,,usichoke haijalishi mara ngapi atakucheki kama unacho msaidie,hutamsaidia milele ipo siku Mwenyezi Mungu atamuinua,na hatosahau msaada wako katika maisha yake
Wakati mwingine Mungu anakutumia wewe kumstiri mja wake na atazidi kukuinua zaidi
Usichoke na usisite kutoa msaada kwa wahitaji kwani wanakuhitaji sana,,much respect kwenu enyi wenye mioyo ya utu na ubinadamu
Gracias
Ni hayo tu!