Kanakansungu, what you are demonstrating here is sheer selfishness, I must tell you boldly. Unajifikiria mwenyewe tu kuhusu mambo ambayo ulikuwa unayapata kwa mkeo lakini siku hizi huyapati. Vipi kuhusu yale aliyokuwa anayapata kwako zamani na sasa hivi hayapati? Hivi yeye unamfikiria hata kidogo? Unasema unampenda mkeo? Si kweli, humpendi. Kumpenda mke hakutokani na unachosema bali unachotenda. Kwa matendo yako haya ya kibinafsi na kukiri kwako, humpendi huyu mama na mimi namsikitikia sana kuingia katika uhusiano wa namna hiyo. Na usitake kudanganya watu kuwa wanaume wote wako kama wewe, HATUKO HIVYO, ni wewe tu unataka kuhalalisha ubinafsi wako kwa kudanganya watu kwamba wanaume ndivyo tulivyo. Narudia, wanaume waaminifu, wema kwa wake zao, ambao wako sensitive na feelings za wake zao, wapo wengi, na ndoa zao zimejaa mapenzi, hakuna ulalamishi kama huu wa kwako.
Hivi huoni kwamba hayo unayomshutumu nayo mkeo kuwa yanakupunguzia starehe, yametokana na upendo wake kwako? Ungekuwa unampenda ungeyapokea kwa shukrani, na kujadili naye jinsi ya kupunguza impact ya hayo mambo na kuboresha mapenzi yenu. Kwa mfano unadai baada ya kuzaa amenenepa na hawezi tena mitindo yenu ya zamani! Lakini kumbuka amezaa na wewe kwa sababu anakupenda, ni mkeo, na watoto waliomfanya awe hivyo ni wanao! Ni sadaka kubwa sana amejitolea kwa ajili yako, wewe unamshutumu? Pili unamshutumu kuwa muda mwingi amechoka na eti ukitaka ngono hadi ubembeleze! Mbona unasahau hayo yanayomchosha ni kwa ajili yako na wanao? Unadhani yeye anataka kuchoka tu, hapendi kupumzika na kufurahia ngono kama wewe? Anachoka kwa sababu ya kukuhudumia wewe na wanao, na huu pia ni upendo na kujitolea sadaka kwa hali ya juu. Badala ya shukrani unatoa shutuma!
Nakutahadharisha, na hili limewatokea wanaume wengi. Haya unayofanya sasa hivi yanamuuma sana mkeo na anatunza kumbukumbu akilini. Siku itafika haya majukumu yatapungua, watoto watakua, na atakuwa na muda wa kutamani naye tendo la ndoa. Lakini wakati huo, kama utakuwa umeendelea na tabia hii, atakuwa hana tena hisia juu yako, na usishangae akipata mwanaume mwingine (tena kijana mdogo tu sana kwako) ambaye watapagawishana kisawasawa. Ndipo utakapoanza kulia wivu, na kama JF bado itakuwepo, utaleta mada hapa ya kuomba msaada kuwa mkeo anatoka nje ya ndoa wakati ana "umri mkubwa"! Utakuwa umeyataka mwenyewe!