Low Key Wanaume Wanapenda Wanawake Wenye Hela kama tu wanawake tunaopenda mabuzi.

Hahahahaaa! Ndo maana nikawa STREET PASTOR yani tunaenda ki HARDCORE, KI STREETS, KIMTAA MTAA
Lara1 kuna demu wangu wa kishua akisoma ulichoandika tu nnajua nimeumia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mara tuambiwe tunaogopa wanawake successful leo lara 1 anasema hao ndio tunawatamani! Au unazungumzia Mario? Mimi binafsi kati ya mwanamke wa kawaida niliemzidi na mwenye hela nitamchukua wa kawaida nimu upgrade au tu upgrade-ane.
 
Kamwe usifanye kosa la kumhudumia mwanamume dadangu, labda kama awe mumewe na hata mumewe mwache afight usimlemeze kwa kumhudumia, muache mwanaume awe mwanaume. Mwanaume ambae hatafight kukuweka wewe sawa hakupendi. Me kabla sijapata kazi ya maana nilikuwa na msichana alikuwa ananifanyia kila kitu, unaweza ukaona unamsaidia ila si hatuko ivo, vya raha ni ulivyopata mwenyewe. Hata tulivoachana haikuuma kwa kweli na wala sikumthamini zaidi eti sababu alinisaidia hapa na pale, kwa kweli hata nguo alikua ananinulia yeye ila sikuwa na furaha nilihisi kama nakuwa controlled. Nikapata msichana mwingine matawi na nilimfukuzia mda mrefu. Sina hata jero ila nafanya kazi overtime kishenzi nipate vidollar kumpeleka serena enzi hizo movenpick. najitutumua kweli kupata hela ya kumpa good time na kumuanzishia vibusinesness vidogo dogo. Mwanaume akikupenda hata kama mvivu kiasi gani atafight kiume mpaka aweze kukuhudumia, hata kama una hela usimwonyeshe we uchune. Be independent but be a woman, let a man be a man. Wanaume wanaopenda wanawake wenye hela wanataka kuwatumia tu. ndo mana unakuta madada wengi wanaojiweza wako singo, kamwe siwezi kwenda kwa mtu naehisi siwezi kumhudumia.


 
Lara nahisi dishi limeyumba, haupo sawa, madhara ya kuokoka kisa matatizo ndio hayo, Okoka ukiwa huna Tatizo, Stress za ndoa Sasa dishi limeyumba, kichwa walu walu kila unaposhika shida, hata ukisifia wanaume umechelewa sana wewe tayari kubali uwe mke wa pili labda
 
Lara 1. Umesaidiwa hivyo na Wanaume! si itakuwa umechakazwa sana!

Haina USHEMEMJI WAMA MAKOMBO WENGINE WANAKULAGA TU. HAHAHAHA. Ila on serious note sio wanaume wote wanaokusaidia wanataka papa. Wengine wanakuhurumia tu mwanamke ulitakiwa uwe umewekwa ndani unashinda na kanga moja ila maisha yamekupenya unakomaa na high heels kutafuta riziki. Wanaingiwa imani wanakusaidia tu
 

Ungeliwaaaaa, ohooooo.
 
Ila we kiboko umesaidiwa sana aisee moe naogopa misaada sana huwa nahisi ntakujadaiwa
Hudaiwi wala nini, wewe kula msaada, wanaume viumbe wa ajabu sanaaa, wana roho ya kutoa hamna mfano. WOGA WAKO UMASIKINI WAKO.
 

Uchoyo nao kwenye mapenzi ni jipuuuu. Mi ndo najifunza kuacha. Mwenyewe uchoyo kwenye mapenzi umeniumizaa sanaaa. Yani unakuta una shida genuine ila haya mambo ya kuhonga na kuchunana, mwanaume hakusadiiii ngoooo mpaka uuze mechi kwengine. Sasa sio mapenzo hayo huo ni uchoyoooo. Kama unacho kula na mpenzi wako.

Na kweli mnataka wanawake wenye hela mjinufaishe ila ASIKWAMBIE MTU INAUMAAA SANAA MWANAUME KUKUACHA SABABU HUNA KITU AKAENDA KWA DEMU MWENYE PESA HATA TEMPORARY. INAUMAA SANAA. CAUSE HATA MIMI SIKUPENDA KUWA MASKINI NI MAISHA TUUUU.
 

HAHAHAAAAAAAA. Ungejua sahivi WOKUVU UMENIFUNGULIA MBINGU DUNIANI MPAKA NAOGOPAAAA. Haki vile nakwambia. Hata nikiuza mchanga watu wanagombeaaa. Wanaume nao date nao sahivi sio wa kitoto. Sikuwahi kuimagine itafika siku Lara mie, mtoto wa mama lara, mtumishi wa serikali, na baba lara mstaafu wa serikali, nimetokea familia za kawaida nitafika level hizi. Kweli Mungu Kibokoooo yao.

Mama mwenyewe haamini kabisaaa, anashinda kanisani anahisi mda wowote fairy tale itaishaaa. Hahahaaaa. Au wataniroga. Kumbe Mungu tu amechekea pande zangu. Yaani wale wanaume wa zamani ilikuwa dhiki tu, na Mungu kweli ananipenda. I dont regret even for sec kuachana nao mbali, walikiwa wananichelewesha tu. Acha maisha yawapenyeee vizuriii. Hahaaaaaaa

NAJUTAAAAAAA, NINGEJUA WOKOVU MTAMU HIVI NINGEOKOKA SIKU NYINGI SANAAAAA. Nimeteseka bila sababu yoyote. Daaah. HALLELUJAH PRAISE THE LORD
 
Ivi Hao Wanawake Wenye Pesa Wanakaa Mitaa Gani. Maana Mi Sijawahi Hata Kupishana Nae Akiwa Katika Gari Lake Mimi Nikiwa Ktk Daladala... Ama Kweli Watu Wanaishi Mimi Nasurvive...

Wapo hata hapo chuoni kwako. Hujui tu kusoma alama za nayakati. We demu ana miaka 19 ana ndinga kali unafikiri akikua atakuwa mwenzio? Thubutuuuuu. Ubamuwahi mapemaaa. Maisha yanapenyaaa mdogo wangu usisikie.
 
Hamuolewi kwasababu hamtaki maskini wenzenu!
HAHHAAAAAAAAAA! UMEJUAJEEEEEEE NDUGU YANGU. YANI UMELENGAAAA.

Sasa we live only once, afu once yenyewe utoto ulikuwa wa kuunga unga hatari, na ukubwa nao bado tukaunge unge. Aaaaaah wapi! GET RICH OR DIE TRYING
 
Mara tuambiwe tunaogopa wanawake successful leo lara 1 anasema hao ndio tunawatamani! Au unazungumzia Mario? Mimi binafsi kati ya mwanamke wa kawaida niliemzidi na mwenye hela nitamchukua wa kawaida nimu upgrade au tu upgrade-ane.

Hayo ni maneno yenu ya woga tu. Ila akitokea wa kishua akakuhitaji yeye, unalainika kama mkate kwenye chai. Low key wote mnapenda kitongaaaaa. Japo mnajitutumua because of our culture msionekane Mariooo. Ila kumpindua demu mwenye hela sio rahisiiiii kabisaaa. Hata mwanaume awe nani.
 
ameen,Safi sana lara1..
 
Mh! Nimehangaika sana kutafuta where's the catch!kwenye andiko lako mpaka nimelipata.Kwanza kwa niaba ya wanaume wenzangu nikushukuru kwa dhati kabisa kwa shukrani zako ulizotoa juu yetu.
Pili niseme tu sehemu ya pili ambayo hasa ni kiini cha andiko lako hii ya kwamba wanaume tunapenda wanawake wenye fedha yes! Tena yes!100% kwa sababu mkono mtupu ndio ambao haulambwi unaanzaje kulamba kono lisilo na kaasali hata tone basi tu inatokea makapuku wenzetu ndio wanaokuja upande huu nao wanaendekeza shida mpaka kero.Niwasilishe kwako na kwenu hata kanisani padre akigundua kwamba siku hiyo hatatoa sadaka basi hata yeye hataswalisha misa
Hii hoja yako ndio sera ya mapenzi na mahusiano kuanzia mwaka 2003 mheshimiwa professa joseph haule alipoachia wimbo wake wa zali la mentali ambao ulichagiza sera hii mpya ya mapenzi na tokea hapo tumepata kile kinachoitwa na wadau wengi kama badiliko la sera ya mapenzi na mahusiano kama "dira"yetu.
Mwisho tutaendelea kushirikiana wanawake kwa kadri mtakavyokuwa mkishirikiana na sisi.
Mwisho wa kuwasilisha hoja!
 
Sio kweli hatuko sawa.
 
Haukufundishwa KWENU VYEMA,MWANAUME MWENYE AKILI HANA SHIDA NA PESA ZAKO,YUKO TAYAR KUKUACHA NA PESA ZAKO NA ELIMU YAKO KAMA USIPOMHESHIM NA KUMTHAMINI KAMA MUME,
SIKU ZOTE WANAWAKE WANAOTAFUTA USAWA KATIKA NDOA NDIO WANAOONGOZA KWA KUVUNJA NDOA,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…