Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio ilivyo sikio la kufa halisikii dawa, tena wamefikia hata kumwambia kaa anataka kuhama ahame wao hawatishiki. NI JK huyu huyu majuzi tu alikuwa akisema (kumuunga mkono Nape) ya kwamba wanaotakiwa kuvuliwa magamba wataondoka!.. maskini kabakia mtupu. Sasa mimi naomba sana nijue hiyo report ya kina Daud Mwakawago maadam Lowassa kaisema nadhani wananchi tuna kila haki ya kudai kujua report ile inasema nini...Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.
Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.
Maneno ya Dr Slaa kusema Dowans ni ya kikwete yametimia kwa mujibu wa Lowasa, sasa Nape na mwenzako Chilagati mjiandae kuvuliwa gamba nyie sasa na fitina zenu. Lowasa sema watanzania wajue ukweli labda watakusamee makosa yako kama kweli unayosema ni ya kweli......
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 24 November 2011 20:29
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: "Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu".
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sasa hp ni patamu! Nasema hivyo kutokana na mawazo niliyotafakari tangu naanza kusoma thread hii,Pamekuchaaaaaa!!
Jamaa anataka kufukia mashimo haraka haraka ili kuficha uchafu wake kwa kisingizio cha kujenga chama. Utajenga chama vipi bila kuzungumzia mpasuko mkubwa uliokuwemo ndani ya chama!? USANII MTUPU!!!!
Hii ripoti inahusu madhambi yote ya JK. Kama NEC wangelitumia hii ripoti JK jina lake lisingepitishwa hata hatua za awali kugombea uraisi. Mkapa alitumia busura kwa kusema mafaili yote ya wagombea yaondolewe mezani na waangalie ni yupi alikuwa anauzika kwa wananchi.Ndio ilivyo sikio la kufa halisikii dawa, tena wamefikia hata kumwambia kaa anataka kuhama ahame wao hawatishiki. NI JK huyu huyu majuzi tu alikuwa akisema (kumuunga mkono Nape) ya kwamba wanaotakiwa kuvuliwa magamba wataondoka!.. maskini kabakia mtupu. Sasa mimi naomba sana nijue hiyo report ya kina Daud Mwakawago maadam Lowassa kaisema nadhani wananchi tuna kila haki ya kudai kujua report ile inasema nini...
Hili ndio tishio la Lowassa kwa JK kwa sababu wanajua swala hili ni wachache na Lowassa kasema kwa mafumbo ambayo JK pekee ndiye anajua kinachoendelea - Akiwa na maana mkuu wangu kumbuka tulikotoka! - Na ukiisoma vizuri hii hotuba ni kutaka muafaka baina yake yeye, Mkapa na Sumaye ili kurudisha Ufisadi wao wote kuwa chama kimoja. Lowassa amekuwa mpole kwa JK lakini mkali na mwenye matusi makubwa kwa Nape kiongozi wa chama ambaye anatimiza majukumu yake..
Sawa ni ya mwaka 1997, hakukuwa na uchaguzi...Hii ripoti inahusu madhambi yote ya JK. Kama NEC wangelitumia hii ripoti JK jina lake lisingepitishwa hata hatua za awali kugombea uraisi. Mkapa alitumia busura kwa kusema mafaili yote ya wagombea yaondolewe mezani na waangalie ni yupi alikuwa anauzika kwa wananchi.
JK siyo muungwana kipindi kingine Lowassa angegoma kujiuzuru na kulilazimisha bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu (lowassa) leo hii Jk asingekuwa raisi.
Sawa ni ya mwaka 1997, hakukuwa na uchaguzi...
Mimi nataka sana kuiona na tuna haki ya wananchi kuambiwa maanake Lowassa kasahau kama JK bado ni rais na yupo madarakani.. Kwa hiyo ni muhimu aseme kweli JK alifanya nini na alituhumiwa nini kiasi kwamba leo asingekuwepo,... sijui ndio angeuliwa ama kutokuwa rais.. Ukweli tunautaka uwe wazi, na yeye mwenyewe tuna machungu naye bado asifikirie kumtishia JK ndio kamaliza ya kwake.
Hivi na wewe ni gamba? Mimi sikuzote nafikiri gwanda! Unanshangaza.
Uchungu wa kiume huujui...remember JK is our President..Hivi wewe kauchungu kako katamfanya nini Lowassa au Kikwete?
Hakuna cha maana kwenye hiyo ripoti, ni majungu tu, unafikiri kungekuwa na cha maana hao kina Mwakawago na wazee wengine "players" wangekubali Kikwete awe Rais wa kuongoza watu zaidi ya million 40. Msidanganywe na pumba hizo.Hii ripoti inahusu madhambi yote ya JK. Kama NEC wangelitumia hii ripoti JK jina lake lisingepitishwa hata hatua za awali kugombea uraisi. Mkapa alitumia busura kwa kusema mafaili yote ya wagombea yaondolewe mezani na waangalie ni yupi alikuwa anauzika kwa wananchi.
JK siyo muungwana kipindi kingine Lowassa angegoma kujiuzuru na kulilazimisha bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu (lowassa) leo hii Jk asingekuwa raisi.
We endelea kushangaa tu...
Watanzania tunataka kujua hayo maneno yaliyosemwa na Lowassa kuhusu Kikwete maana athari zilizofanywa na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans hazikuwagusa magamba pekee bali Watanzania wote, naona msanii Kikwete haraka haraka anataka kudanganya umma wa Watanzania kwamba wanajenga chama!!!! Utajenga chama chenye mpasuko bila kuzungumzia matatizo yaliyomo ndani ya chama na ambayo yanaiathiri nchi pia!!!!?
Kama mkataba ungekuwa ni kutengeneza magwanda yenu ya kijani na njano basi Watanzania wengine ambao si magamba yasingetuhusu lakini hili la Richmond/Dowans linatuhusu na ndio maana Kikwete inabidi atueleze kinaga ubaga kuhusiana na kauli iliyotolewa na Lowassa.
Uchungu wa kiume huujui...remember JK is our President..
Pili, hapa Lowassa anataka kujikosha na najua fika kwamba mwaka 1995 JK alimshinda Mkapa, pengine JK alikuwa na mpango wa Mapinduzi 1997 ama kuhama chama... ama hasira na Nyerere. Hivyo taarifa ilipomfikia Mkapa toka kwa Daudi Mwakawago Mungu amrehemu ndio maana kafa maskini kwa uzalendo wake - Mkapa akiwa rais akapuuza. sasa kimbelembele cha Lowassa ni kutaka kumtahadharisha JK wakati huyu ni President, yeye nani?.
Aaaaah samahani nimesahau wewe shabiki sii mchezaji!
Hapo sasa!...ndio maana inakuwa kazi kwako kufikiria machungu yake. na huwezi...Kama yangekuwa na uzazi wala nisingebishana na wewe.Ustake ncheke, uchungu wa kiume unakuwaje? Wallahi siujui, makubwa haya.
Yes, naona magwanda sasa mnakubali Kikwete kuwa ni Rais wa halali wa Watanzania wote. Hongera sana.
Mchezaji unaecheza kwa "remote" si bora mimi nipo kiwanjani "live".
Hivi hapo kuna habari ya kutishwa Kikwete? Tatizo lenu kubwa huwa mnasoma muandishi anavyotaka na si uhalisia wa yaliyojiri, mtu akiogea kwenye hadhara kama ile halafu mwandishi anukuu vipande atakavyo yeye na kuvijengea hoja, ujuwe huyo mwandishi anataka wewe uyashike yake na si yaliyojiri. Hapo mmepigwa changa la macho.Hapo sasa!...ndio maana inakuwa kazi kwako kufikiria machungu yake. na huwezi...Kama yangekuwa na uzazi wala nisingebishana na wewe.
Sio swala la kumkubali JK kuwa ni kiongozi mzuri bali JK ni rais ambaye anatakiwa kuheshimiwa na sii kutishwa na watu ktk mikutano ya chama ili iweje?... hasa na watu hawa
Kama hatishiki mbona kaondoa hoja ya magamba wasivuliwe!...Unafikiri ndio kayamaliza Rostam atakuja na machungu yake yaani ngoma hii bado kabisa!Hivi hapo kuna habari ya kutishwa Kikwete? Tatizo lenu kubwa huwa mnasoma muandishi anavyotaka na si uhalisia wa yaliyojiri, mtu akiogea kwenye hadhara kama ile halafu mwandishi anukuu vipande atakavyo yeye na kuvijengea hoja, ujuwe huyo mwandishi anataka wewe uyashike yake na si yaliyojiri. Hapo mmepigwa changa la macho.
Sioni mahali ambapo Kikwete ametishwa au kuna cha kumtisha sasa hivi? Kama Ukuu ndio anao, hajatishika hiyo 1997 na akasema kama urais ni Mungu mwenyewe ndiye apangae atatishika leo hii? Unanchekesha.