Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

tembea hata uchi lakini, lakini fisadi ni fisadi tu. Udhaifu wa CCM kumwadabisha mdhalimu mwenzao haitufanyi tuone Lowassa ni msafi. Msiitie najisi nchi yetu, tumechoka na mabalaa

Habadiliki kwa lolote lile, hata akisema mishara itoke siku 5 kabla still ni yuleyule fisadi tu, hata ukitembea uchi nchi nzima he will not change.
 
hata mimi namkubali Lowassa, lakini kama fisadi la kimataifa, aliyetaka kutuletea mpaka mvua ya kichina. nazidi kumkubali kwa kuwa naona kila dalili za watu kuanza kumuabudu
Bora huyu anayesema na kutekeleza mkuu kulilo ambaye analia tv.mi lowasa namkubali sana
 
Wa kumlaumu kwa yote haya ni Mkapa,Mkapa alipoletewa kabrasha la uchafu wa mkulu na Sozigwa kule Zanzibar 1993 akalipotezea,ndio maana EL anadai kama Mkapa angemwanika juani mkulu wetu,leo hii asingekuwa amekalia hicho kigoda wanachongombania,kwa mantiki hiyo EL anajijua ni mchafu lakini naye anataka alindwe na mkulu kama vile mkulu wetu alivyolindwa na Mkapa.Kwa mtu kama EL ilitakiwe ajitetee kivyake ,ananikumbushe hadithi ya mtoto aliyeshikwa anaiba mboga jikoni na alipokuwa anaadhibiwa na mama yke akasema mama mbona unanionea mimi tu mbona naye kaka amewahi kuiba mboga na hujampiga.EL alitakiwe ajitetea mwenyewe ,alichofanya ni maamuzi mepesi inaonekana ni muoga na ana visasi,anataka aachiwe kama mkulu alivyoachwa,huyo ndio tunataka ati awe RAHISI wetu
 
helow,
ndugu EL
NAAKUPONGEZA kwa dhati enzi zako za uwazir.mkuu...........
nakumbuka, ndio kwanza mm nilikuwa naanza kazi......

nakupongeza kwa.mishahara kutoka kwa wakati...... ulitangaza tarehe 23 iwe umetoka, tena uliamuru wahasibu.walipa mishahara wafanye kazi hadi weekend iwapo tarehe inaangukia hyo tarehe

WAFANYAKAZI WA KIMA CHA CHINI TUNAZO KURA ZAKO 2015

Hadi sasa, cijaelewa sera za CDM kwa wafanyakazi......mnnn

Regeo likes this.
FF dislikes this.
Safi sanaaa......!!!!!!!!!!!!!
 
Rejao, Rejao rejaooo! You never cease to amaze me kwa kiwango chako cha ujinga! Kupinga ufisadi kumepitwa na wakati? Mh! Nashindwa hata kuendelea maana sijui nianzie wapi kukuelewesha ubaya wa ufisadi na kwa nini tunatakiwa kuupinga mpak a utokomee! Hilo la katiba ndio bora ninyamaze kabisa!
this is histry my dia...tumeshagundua tatizo tayari, cha muhimu kutafutia ufumbuzi hili suala ikiwa ni pamoja na kustrengthen auditing system yetu! Sasa hawa ndugu zangu CDM kila mara wanalishupalia hili suala. Nachotaka kusikia kutoka kwao ni malengo yao kwa Tanzania hii kama watapewa dhamana ya kuiongoza.
 
Acha hadithi za kutunga ww, kama barua ya kujiuzulu ilikubaliwa usiku wa manane, mbona hautuelezi nini kilimfanya EL kutangaza bungeni asubuhi yake kujiuzulu, na barua hiyo ya kukubaliwa EL kujiuzulu alipewa nani wakati hata spika wa kipindi hicho amewahi kukuaririwa akisema kujiuzulu kwa EL ndilo jambo lililomshtua mno kipindi cha uongozi wake- Hizi hadithi zenu za kutunga pelekeni huko vijiweni kwenu!!!
Thank U, you have put the Record clearly here
 
Tukiacha his black side, Lowassa ni mchapa kazi! hamna mtu anayeweza kupinga hilo.
Mpaka sasa sijajua msimamo wa chadema kwa nchi hii. Sijui wakiingia madarakani watafanya nini. Wana sera moja tu ya kupigana ufisadi, na hii imeshapitwa na wakati. Sera ya katiba mpya nayo tayari CCM imeshawapiga bao.
Hivi huoni sisiemu yako ilivyo pwaya?raisi hana kazi anayofanya zaidi ya Kukwea pipa everyday,hebu acha ushabiki wa simba na yanga CCM imeshindwa kazi.
 
this is histry my dia...tumeshagundua tatizo tayari, cha muhimu kutafutia ufumbuzi hili suala ikiwa ni pamoja na kustrengthen auditing system yetu! Sasa hawa ndugu zangu CDM kila mara wanalishupalia hili suala. Nachotaka kusikia kutoka kwao ni malengo yao kwa Tanzania hii kama watapewa dhamana ya kuiongoza.

mgaya wakati anapambana na CCM jamaaa walikuwa kimyaaaa

hadi leo CDM hawasemi kuhusu wafanyalazi hasa mshahara!!!"'''''

wana dili na fujooooiii, maandamano!!!'''@#%&#
 
Hivi huoni sisiemu yako ilivyo pwaya?raisi hana kazi anayofanya zaidi ya Kukwea pipa everyday,hebu acha ushabiki wa simba na yanga CCM imeshindwa kazi.
:focus::focus: hapa hatumuongelei JK, ndio maana mimi sijamwongea padre!
 
mgaya wakati anapambana na CCM jamaaa walikuwa kimyaaaa

hadi leo CDM hawasemi kuhusu wafanyalazi hasa mshahara!!!"'''''

wana dili na fujooooiii, maandamano!!!'''@#%&#
Wanajijali wenyewe, huwa nasema siku zote, CDM ni kama taasisi ya watu fulani, wenye malengo yao wenyewe wanayoyajua wao.
 
this is histry my dia...tumeshagundua tatizo tayari, cha muhimu kutafutia ufumbuzi hili suala ikiwa ni pamoja na kustrengthen auditing system yetu! Sasa hawa ndugu zangu CDM kila mara wanalishupalia hili suala. Nachotaka kusikia kutoka kwao ni malengo yao kwa Tanzania hii kama watapewa dhamana ya kuiongoza.

Tatizo co history ila ni kuwa ufisadi bado unaendelea kufanyika hadi leo hii ndo maana hawa magwanda bado wanaendelea na hilo tatizo ambalo wao may be wanaweza kulita2a wakiingia madarakani.Halafu kingine ukiangalia kwa upana zaidi utajua kuwa UFISADI ndo ume2fanya hadi leo hii 2we maskini sana.
 
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ni CHENGE au alishaondolewa??

Kamati ya Maadili ina wajumbe wazito, baadhi yao ni: Mwenyekiti Kikwete, Makamu wenyeviti, Pius Msekwa na Amani Karume, Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Iddi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Manaibu Katibu Mkuu, Kapteni mstaafu John Chiligati na Vuai Ali Vuai.
 
Nakusubiri best..Onana nae akuwezeshe viatu vya kuzunguka nchi nzima.
 
Acha hadithi za kutunga ww, kama barua ya kujiuzulu ilikubaliwa usiku wa manane, mbona hautuelezi nini kilimfanya EL kutangaza bungeni asubuhi yake kujiuzulu, na barua hiyo ya kukubaliwa EL kujiuzulu alipewa nani wakati hata spika wa kipindi hicho amewahi kukuaririwa akisema kujiuzulu kwa EL ndilo jambo lililomshtua mno kipindi cha uongozi wake- Hizi hadithi zenu za kutunga pelekeni huko vijiweni kwenu!!!

bwana mdogo ngoja tukukaze kitako kukujuza,yaelekea huifahamu siasa!!siasa sio kama hisabati,haina formula,ni mchezo mchafu dogo,kwa hiyo unaamini kabisa eti sitta "alistuka" lowassa kujiuzulu,dogo amka,hata kama usingizi ni mtamu kiasi gani inabidi uamke sasa,achana na porojo za wanasiasa eti kujiuzulu kwa lowassa ndilo jambo lililomstua,ina maana alikua hajui kinachoendelea katika harakati zile za usiku wa kuamkia tukio!kuna mbunge alilala mapema siku ile pale dodoma kweli!
 
Watu kwa kucheza na maneno ni mahodari sana, hivi Lowassa kasema nini kuhusu Richmond zaidi ya kusema alimpigia simu Kikwete alipokuwa nje ya nchi akamwambia asubiri ushauri wa makatibu wakuu.

Hapo ndiyo Lowassa kasema Richmond ya Kikwete au ina husiana na Kikwete? Mnanshangaza!

Dadangu hawa wasikuumize kichwa,wamepengwa kujaa humu na kudandia kila post yenye jina la lowassa hushangai wengi ni wale wale kila post utakayooenda,basi ndio hivyo wametwanya kila sehemu kuanzia kwenye media mpaka mitandaoni,hii ni strategy!ndio maana wanashangilia lowassa kusema alipiga simu!wanasahau kwamba nec ya lowasa imetoa kibali lowassa akashughulikiwe kwenye kamati kuu!
 
Mi nakuunga mkono ccm wasipo msimamisha lowasa inakula kwao

huu ni uongo!we chadema ama tlp kweli unaweza kuwapa ccm mbinu za kukushinda au unataka kuwaingiza choo cha stendi ili wamsimamishe lowassa kwa kuwa unaujua udhaifu wake muwashinde kirahisi!otherwise wewe mchana unawadanganya wenzako ni mpinzani usiku ni kada mzuri wa ccm!
 
Siku yaja,Siku itakafika atakaposhuka mwana waadamu na kuchagua kondoo na mbuzi....Hapa tunaumiza Comp zetu kuganga ya mwenyezi Mungu ambaye ndie aijuae siri ya nani atakayekuwa magogoni 2015.Kila mtu anajitahidi kutabiri yajayo,Mi acha nipite kwanza ntarudi siku hiyo kila chama kitakapopitisha mgombea wake.
 
Back
Top Bottom