Elections 2015 Lowassa alivyoipaisha CHADEMA katika uchaguzi huu, ni asset na ataendelea kuwa asset

Elections 2015 Lowassa alivyoipaisha CHADEMA katika uchaguzi huu, ni asset na ataendelea kuwa asset

Katika jamii utapata heshima kwa kufanya biashara halali yenye kukupatia faida nzuri. Lakini ukifanya biashara haramu kama kuuza bangi au madawa ya kulevya, utapata faida kubwa lakini heshima yako katika jamii itashuka sana. Ni lazima kulinda heshima kuliko kukimbilia mapato ya aibu. Nyerere alilinda heshima yake ndo maana hadi leo fikra zake zinadumu. Hakuwahi kubadili gia angani. Ni liability.
Kwa lugha nyepesi watanzania inabidi tulinde heshima yetu kwa kuacha kuongeza kasi ya maendeleo kwani kasi kubwa inashusha heshima. Ni heri kuendelea na ukosefu wa huduma za maji, afya na elimu lakini tukabaki na heshima, kuliko kupata visima vingi vya maji, kupata fursa za elimu, kuwa na uhakika wa matibabu muda wote na mahali popote huku tukikosa hesshima. Kasi ya kuondoa umasikini na kupata maendeleo inaondoa heshima
 
kwani kilichofanyika nani asiyejua! Wizi tu na mabavu na kupokonya haki za watanzania!
acheni visingizio mlipigwa kihalali kabisa pamoja na juhudi kubwa mlizofanya za kuiba kura km kule moshi masanduku yalikutwa porini.mna matatizo makubwa ya ukabila udini ufisadi ubinafsi msiporekebisha kila uchaguzi mtalalamika kuibiwa kura tu
 
nilimpigia magufuli, huyu ni mchapa kazi si kama JK

kwa cdm kuna jambo muhimu la kulitazama
1.SLAA ALIGOMBEA DHIDI YA JK.....note jk alishakuwa madarakani na kimsingi alikuwa na ukakasi mwingi
2.LOWASSA ALIGOMBEA DHIDI YA BULDOZER....hakika magufuli ananguvu mara kumi ya JK

what if SLAA angegombea kipindi hiki against magufuli????nadhan asingefikia alipo lowassa na cdm ingekuwa na wabunge wachache sana.
pia:udini ulikuwepo kipindi cha slaa vs JK.....
 
5-23 vs 23-35 na back up ya Ukawa na mpasuko wa ccm...

CCM mnapenda namba hamjui hesabu,yani we umeona hivyo tu ,ruzuku ya 20% mliyopoteza hauoni? Halmashauri zaidi ya 20 mmepoteza hauoni? Jembe lenu pamoja na wizi wa kura limeambulia 58%??? seriously???? Mwaka 2020 mnapata 32%.
 
5-23 vs 23-35 na back up ya Ukawa na mpasuko wa ccm...

Kwa uchaguzi gani huo wa kuufanyia uchambuzi? Huu wa Tanzania uliojaa vitimbi na mizengwe ya kila aina? Wagombea wa upinzani hawatangazwi pale wanaposhinda mpaka wananchi wapige kambi kwenye ofisi za halmashauri. Ujinga mtupu!
 
Mtalia sana ukweli ni kuwa mmeshindwa tena kihalali. Ila ck zote mfa maji haachi kutapatapa. Mawakala wenu huwa mnawapaga Valium wkt wa kusimamia uchaguzi? Maana waliokuwepo, wamesaini fomu lkn bado mnabweka ka vimbwa koko. Uchaguzi umeisha sasa ni Hapa Kazi Tu. Mwacheni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli afanye kazi.
 
Ruzuku ya chadema itaongezeka. Na wabia wenu je? Cuf nccr? Au mshawafuta sio vyama vya upinzani.
 
Dr. Wa mihogo soma hiiLOWASSA ni "Asset au Liability.-Kabla ya ujio wa Lowassa ndani ya chadema, chadema ilikuwa na majimbo 23 tu na viti maalumu 26 na kuwa na wabunge 49 ktk bunge la 10 la 2010-2015, ujio wa Lowassa umeongeza wabunge kutoka majimbo 23 mwaka 2010 hadi majimbo 35 mwaka 2015 na viti maalumu kutoka 26 hadi 43 na kufanya jumla ya wabunge wa chadema 78 ktk bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chama cha upinzani tangu Tanzania ipate uhuru, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"-Kabla kuondoka kwa Lowassa ndani ya ccm, ccm ilikuwa na wabunge wa viti maalumu 79 mwaka 2010, sasa ccm itakuwa viti maalumu 62 tu kwa maana hiyo nguvu ya Lowassa imeondoka na viti maalum 17 ambao wote imebidi wapewe chadema, na ndiyo maana sasa chadema itakuwa na viti maalumu 43, which means, chukua viti 26 vya cdm 2010 + viti 17 alivyokuja navyo Lowassa = 43, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"-Mwaka 2010-2015, ccm ilikuwa inapokea ruzuku zaidi ya 78% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa kutokana na kura za urais alizopata JK, mwaka huu ccm itapokea ruzuku isiyozidi 59% ya ruzuku yote ya vyama ni sawa pungufu ya 20% waliyopoteza ccm, Na kwa mara ya kwanza chama cha upinzani chadema kitapokea 40% ya ruzuku yote ya vya siasa, hii ni kutokana na kura mil 6=39% alizopata Mhe. Lowassa. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"-Kabla ya ujio wa Lowassa, katika majiji matano (5), Mbeya, Dar, Tanga, Mwanza & Arusha, cdm ilikuwa haiongozi hata jiji moja kati ya hayo kwa mwaka 2010-2015, yote yalikuwa chini ya ccm, Ujio wa Lowassa umeifanya chadema kuongoza majiji 4 (Mbeya, Dar, Arusha & Tanga japo Tanga itakuwa chini ya UKAWA) kutokana na ushindi wa madiwani wake ktk majiji hayo na ccm imebaki na jiji la Mwanza pekee, which means ccm imepoteza majiji 4 kutokana na kuondoka kwa Lowassa. Je Lowasa ni "Asset" au "Liability"-Mwaka 2010-2015 chadema ilikuwa inaongoza halimashauri 5 nchi nzima mfano: Moshi & Karatu, mwaka 2015 kwa mara ya kwanza chadema itakuwa inaongoza halimashauri 30 Tanzania hii ni kutokana na Ushindi wa madiwani na wabunge ktk halimashauri husika. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"NB: Kwa mtu wa kawaida na anayefikiria ya leo bila kujua kesho itakuwaje alibeza ujio wa Lowassa ndani ya chadema, lakini kwa anayefikiria leo na kesho na kuangalia kwa jicho la tatu atakuwa amegundua umuhimu wa ujio wa Mhe. EDWARD LOWASSA.Ahsante...!!!
Well assessed and presented. Bravo CDM
 
Mleta mada utakuwa ulikimbia hisabati ya la kwanza hadi la saba. Inawezekana vipi ukaiona 23 iliyotokana na Dr. Slaa tena wakati ule mazingira yakiwa magumu, bado chama hakijaeleweka, bado hakijajengwa kitaasisi n.k eti ni namba ndogo ukilinganisha na 11 iliyotokana na Lowassa? kipindi ambacho upinzani umeimarika Tz, CDM imekuwa taasisi na watu wanq hari ya kubadilisha utawala mnamleta Lowassa anaishia kuwapatia viti 11 licha ya mabilioni aliyoyatumia alafu mnakuja kumsifia eti kawasaidia? how? mtatunga uongo wote na kamwe hautawasaidia labda mkawadanganye wasio na shule kichwani
 
Back
Top Bottom