Lowassa amenifanya nikuchukie Diamond Platnumz

Usimfanyie hivo King, unampenda kimahaba au anamziki mzuri?? kama kimahaba upo sahihi na maamuzi yako

Mkuu mimi ninavynendelea fauatilia mchakato huu wa uchaguzi mwaka huu, ninagundua vijana wengi Tanzania wanaongozwa na mihemko(emotions), chuki kali(hatred,deep hostility), kulipizana visasi (avenge) lakini wengi wao nimegundua ni wajinga na wafuata mkumbo(nyumbu).
 

Ni laana kufuatilia maisha ya mtu na kutaka awe kama wewe, umekosea kuanzia kuja kulialia Jamii forums

Kizazi cha 95 kinashida saana hahahahahaha Somo la uraia muhimu sana...
 
kwa mtindo huo unawatukana wazazi wako kwa kuwaweka CCM madarakani miaka yote hiyo maana mabadiliko watu walikuwa wanayataka tokea vyamavingi vimeanza 1995 mambo yalikuwa moto sana, ila bado ccm ikaendelea kuongoza TZ
Wapiga kura wa 1995 sio sawa na wa mwaka 2015.Wapiga kura wa mwaka wengi walikuwa ni kizazi cha Tanu/Asp ila kizazi cha sasa si kama kile na wamejiandikisha vya kutosha
 
Inaelekea haujamletea upungufu, siku aliyorusha ya ccm akikywa na followers eg. Instagram 943k, leo kazidi million.

Pole unaumia roho mwenzako anapiga pesa.

Una akili Sana mkuu we endelea kuhangaika na namba za follower WA instagram kumbuka katika idadi hiyo wapo wengine ambao walisha fariki kufa na wengine hawamfatilii jamaa kwa sasa kabisa ila bado wapo katika idadi hiyo.

Na ujue kuwa Kuna wengine wana ID za insta hata kumi na zote wamemfollow jamaa Kama watu tofauti kumbe mtu mmoja endelea Tu kushangaa hizo namba!
 

Kweli kabisa mkuu, wamesahau hii nchi ina demokrasia isiyo na mipaka na ikiwa hivyo kinyume na katiba basi haki inakuwa haitendeki


Yani wenyewe walivyo hawajielewi wapo Chama ca demokrasia na maendeleo lakini hata hiyo "DEMOKRASIA" hawaifuati hivi wanaweza wakawa sawa kichwani kweli?

Somo la uraia muhimu sana, maana unaweza ukawa umefika miaka 18 kama vijana wetu hawa ila kichwani ikawa tatizo kidogo, wewe unachojuwa ni matatizo tu yanayoikumba hii nchi afu unajiona mkomavu kisiasa hatariiiiiiiii


TEAM DIAMOND PLATNUMZ


KING OF AFROPOP


MICHAEL JACKSON WA AFRIKA



TANZANIAN ICON
 
Ni laana kufuatilia maisha ya mtu na kutaka awe kama wewe, umekosea kuanzia kuja kulialia Jamii forums

Kizazi cha 95 kinashida saana hahahahahaha Somo la uraia muhimu sana...

huyu dogo mi ndo namuona hapa leo, anadai eti alikua anampigania diamond!!?
 

Mkuu umeona idadi ya viewers instagram????

Umeona idadi inayoongezeka kila siku kumfollow mtoto wake?? hadi kumzidi karibia mara mbili Lowasa na nyota zake anazodaiwa kuwa nazo...

Umeona shangwe alilopata Tanga??

Na mwisho wa siku tunajumuisha na nguvu ya kipaji na juhudi zake


UMEONA NOMINATION LIST YA WASANII WAKALI ZAIDI AFRIKA MTV EMA???

NA LEO PROJECT HEWANI YA UNITED NATIONS

TEAM DIAMOND PLATNUMZ
 
Ni laana kufuatilia maisha ya mtu na kutaka awe kama wewe, umekosea kuanzia kuja kulialia Jamii forums

Kizazi cha 95 kinashida saana hahahahahaha Somo la uraia muhimu sana...

Wewe ndo unalia lia nani kakuita uje kuhangaika katika thread za watu,Kuna mtu kakutag hapa?

Kama wewe ni wa60s just chill out there!

Au umevutiwa!
 
huyu dogo mi ndo namuona hapa leo, anadai eti alikua anampigania diamond!!?

Hahahahahaha hata mi simfahamu ila dawa ya mjinga ni somo sio kumpuuzia ili wajinga wenzake wajifunze


SHULE BILA ADA


TEAM DIAMOND PLATNUMZ
 
Wewe ndo unalia lia nani kakuita uje kuhangaika katika thread za watu,Kuna mtu kakutag hapa?

Kama wewe ni wa60s just chill out there!

Au umevutiwa!

Kwanza hatupo PM hapa

Hili ni jukwaa, la Celebritis na kwa sasa tunamzungumzia King of afropop diamond platnumz Nitakosaje kuwepo??

Afu mi nisipokutoa ujinga unafikiri ni nani atakutoa??

SHULE BILA ADA


TEAM DIAMOND PLATNUMZ
 
Last edited by a moderator:
Diamond Platnumz amepata nafasi nyingine ya
kushirikiana na mastaa mbalimbali wa Afrika
akiwemo Wizkid wa Nigeria, kurekodi wimbo wa
kampeni ya Umoja wa mataifa, ‘United Nations
Global Goals campaign’.

Hit maker huyo wa ‘Nana’ na Wizkid
wameungana na wanamuziki wengine wakubwa
wa Afrika kama Yemi Alade (Nigeria), rapper
Sarkodie (Ghana), kundi la Mafikizolo (South
Africa), Sauti Sol (Kenya), Becca (Ghana) na
Toofan (Togo).

Maproducer ambao wameshiriki kutengeneza
wimbo huo ni Cobhams Asuquo (Nigeria), David
KING DAVID Muthami (Kenya) na Ellputo
(Mozambique).

SOURCE : BONGO5
 

nooma sana
 
Kichwa cha bongo fleva, kinazidi kutuwakilisha vema anga za kimataifa, na hii ni zamu ya MTV EMA ambapo huwa wanachaguliwa wasanii bora watano tu!! wa kwenda kujumuika na wasanii wa marekani katika utoaji tuzo huko Ulaya..

Mpaka sasa wameshatangazwa wasanii wanne
+ diamond
+Yemi Alade
+Aka
+Davido

na wa tano, anatangazwa hivi punde nitawaleteeni

Hakika ni furaha kubwa kwa wapenda burudani, kwa uwakilishi wa kipekee wa Diamond platnumz... piga keleleeeeeeeee oyooooo

mtanyooka tu
 
Last edited by a moderator:
Hii ni TOP 10 kati ya video za wanamuziki wa Afrika 2015 zilizotazamwa zaidi Youtube.. Na kati ya mafanikio anayoweza kujivunia mwanamuziki, ni suala la youtube ambapo inaonyesha;-

+ Ni jinsi gani kazi yako imekubalika na mashabiki
+ Ni jinsi gani una mashabiki wengi walio active kukupa support na wanaopenda kufuatilia kazi zako
+ Na ni jinsi gani unaingiza pesa kupitia video zako, hata bila ya kufanya shows, mikataba, au hatimiliki..

Hayo yote amezidi kuyadhihirisha nguli wa Bongo fleva diamond platnumz licha ya kuwepo mashabiki wachache wasiopenda maendeleo yake, lakini amezidi kuwatia pilipili na mchanga machoni kwa juhudi na mafanikio anayozidi kuyapata kila siku..

Na ukijaribu kuitazama list hii utagundua nyimbo 8 ni za wasanii wa Nigeria na mbili tu sio za Nigeria ambapo ni za Diamond, na Tanzania na Afrika mashariki kiujumla kwa mtu anaejitambua na mpenda burudani hana budi kujisifu kwa uwakilishi mzuri wa kichwa hiki cha bongo fleva, ambapo wasanii wenzake pia wamekuwa wakijifunza na kuiga mengi kutoka kwake na kuwa role model wao licha ya wao kukataa kuliweka hilo wazi, kiufupi amekuwa kama chuo cha bongo fleva

Hii ni mpaka leo tar 08, september
1. Psquare ft. Don jazzy - collable
11,076,652 views

2. Mr Flavour ft. Chidinma - Ololufe
4,796,162 views

3. diamond platnumz ft. Mr Flavour - Nana
4,550,423 views

4. diamond platnumz ft. Khadija Kopa - Nasema nawe
3,978,387 views

5. Wizkid - Ojuelegba
3,630,991 views

6. Davido ft. Uhuru + Dj Buckz - The sound
3,248,037 views

7. Kiss Daniel ft. Davido + Tiwa Savage - Woju
3,070,540 views

8. Davido ft. Meek mill - Fans mi
2,737,313 views

9. Olamide - Bobo
2,577,288 views

10. Korede bello - Godwin
2,405,917 views
 
Watu wa ukawa wana msongo wa mawazo ndio maana wanaota mabadiliko ambayo hayapo... We mtu anaamini eti lowassa akiingia Tanzania hakutakuwa na maskini sasa hizo akili au mafuta ya taa!

Umaskini ni fashion?. Kamasi .
 

Hakuna tatizo mkuu Ni jambo jema sina tatizo na Hilo;hata Mimi nilikua namwombea jamaa mafanikio;nilicho toa Ni ushauri Tu huna haja ya ya kuhangaika Na takwimu kwani wewe umesoma statistics?

Wenye akili wamenielewa hili swala Ni la natural conflict Na sio maamuzi ya hiali ndo maana nikashauri kwa faida yake Na si kwa hasara yake;sababu huwezi jua ameafect WA ngapi kwa ishu hiyo cha msingi ilibidi awaze kuwa Kuna maisha baada ya oktoba 25.hilo Tu.

Waswahili wanasemaga usiache mmbachao kwa msaala upitao!
 
Producer Sheddy Clever aliyehusika na upishi wa
collabo kubwa ya kimataifa ya staa wa Tanzania,
Diamond Platnumz na mwimbaji wa R&B kutoka
Marekani, Ne-Yo amedokeza kidogo kuhusu
wimbo huo.

Mtayarishaji huyo wa Burn Records amesema
kuwa Ne-Yo aliimba baadhi ya maneno ya
Kiswahili katika verse yake.
“Ne-Yo kaimba Kiswahili katika single hiyo,
Diamond alimuimbisha Kiswahili siwezi kusema ni
maneno gani ya kiswahili bali watu wakae mkao
wa kula” Sheddy aliiambia Millardayo.com.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond
kuwaimbisha Kiswahili wasanii wa kimataifa
anaofanya nao collabo, alifanya hivyo pia kwenye
remix ya Number One aliyomshirikisha Davido,
ambaye naye aliimba maneno machache ya
Kiswahili.

SOURCE : BONGO5
 
Kwanza hatupo PM hapa

Hili ni jukwaa, la Celebritis na kwa sasa tunamzungumzia King of afropop diamond platnumz Nitakosaje kuwepo??

Afu mi nisipokutoa ujinga unafikiri ni nani atakutoa??

SHULE BILA ADA


TEAM DIAMOND PLATNUMZ

Tuende nako taratibu haka ka nyuli kakomae akili.

Tusikakatishe tamaa mapema. Kanajifunza ku argue.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…