Saa nyingine ni vizuri kuficha ujinga, hebu tuambie ni chuo gani Maguli alichukua Doctorate ya Engineering! Jaribu kufuatilia vitu na acha ushabiki mandazi
Magufuli alianza elimu ya msingi
katika Shule ya Msingi Chato
wilayani Chato mwaka 1967 na
alihitimu mwaka 1974. Alifaulu na
kujiunga na Shule ya Seminari
Katoke, Biharamulo ambako alisoma
kidato cha Kwanza na cha Pili
mwaka 1975 - 1977, akahamishiwa
Shule ya Sekondari Lake, Mwanza
ambako alisoma kidato cha Tatu na
Nne mwaka 1977 - 1978.
Masomo ya kidato cha Tano na Sita
aliyapata mkoani Iringa katika Shule
ya Sekondari Mkwawa kati ya
mwaka 1979 na 1981. Halafu alirudi
Chuo cha Ualimu Mkwawa kusomea
Stashahada ya Elimu ya Sayansi
akibobea kwenye masomo ya Kemia,
Hisabati na Elimu; hii ilikuwa
mwaka 1981 1982.
Alipopata stashahada yake, moja kwa
moja alikwenda kuanza kazi ya
ualimu katika Shule ya Sekondari
Sengerema, akifundisha masomo ya
Kemia na Hisabati. Ajira hii aliifanya
kati ya mwaka 1982 na 1983.
Kisha alijiunga na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria
akianzia Makutupora, Dodoma (Julai
- Desemba 1983), kisha akaenda
kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari
hadi Machi 1984) na akamalizia
katika kambi ya Mpwapwa mkoani
Dodoma (Machi Juni 1984).
Mwaka 1985 alijiunga Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam akisomea Shahada
ya Sayansi ya Elimu akibobea
kwenye masomo ya Kemia na
Hisabati na alihitimu mwaka 1988.
Mwaka 1989 - 1995 alifanya kazi
katika kiwanda cha Nyanza
Cooperative Union (Ltd.) akiwa
mkemia na wakati huohuo alianza
masomo ya shahada ya uzamili ya
Sayansi katika Chuo Kikuu cha
Salford nchini Uingereza,
kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam ambako alisoma kati ya
mwaka 1991 na 1994.
Magufuli aliendelea na elimu ya juu
zaidi kwa maana ya Shahada ya
Uzamivu ya Kemia kuanzia mwaka
2000 hadi 2009 ambayo aliihitimu
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na kuwa mhitimu wa shahada ya
udaktari.
Anaitwa DR. JOHN POMBE MAGUFULI
ulivo boya hjui hata hiyo Dr ya mwanzoni inamaanisha nini au ulijuwa wanaweka pambo ??? ahahahaahahash