Lowassa ampinga Warioba serikali tatu


Ila utetezi wako una mushkeli! Sijamsikia Lowassa akisema I was wrong! Never! Labda nitafutie hiyo clip!
 
Kweli mahaba niue...

mtu akipenda chongo anaita kengeza...
 
Hii ni sawa na kumlaumu mtu mliyekuwa mnajua kuwa ni mlevi akisema pombe ni mbaya baada ya kuuona wokovu na kuokoka. Binadamu hatuwezi kuendelea kuwa na msimamo wa aina moja hata pale kweli inapotufikia, ukiujua ukweli huna budi kuukana uongo.
Ndio maana tunatubu makosa yetu na kuwa watu wapya.
 

Huwezi fananisha kiongozi na mlevi hata sikumoja.
 
Huwezi fananisha kiongozi na mlevi hata sikumoja.
Kama ungekuwa na uwezo wa kiakili jingalao ningekuambia tafuta kauli za Mwalimu Nyerere 1978/79 juu ya Muamari Gaddafi kisha linganisha na zile za kumhusu mtu huyo huyo miaka kadhaa kabla hajaaga dunia 1999.
Dunia inabadilika kulingana na wakati nasi binadamu lazima tukubali kubadilika.
 
Last edited by a moderator:
Huwezi fananisha kiongozi na mlevi hata sikumoja.

Hasa yule kiongozi anayebadili msimamo tu kwa kusababu ya jina lake "kukatwa" na kamati fulani ya CCM. Angeamua hivyo kabla hata hajachukua fomu CCM, ningemsikia.

Hata hivyo Uchaguzi umeshapita, aliyekosa keshakosa na aliyepata keshapata; tusubiri tena miaka mitano ijayo. Lowassa aliiambia BBC kuwa akikosa atakwenda kuchunga ng'ombe wake huko Moduli; ngoja tunaone kama ni mtu sereious anayetimiza ahadi zake. Asipkwenda kuchunga ng'ombe Monduli basi ujue kuwa hata kama angechaguliwa kuwa Rais asingefanya lolote kule Ikulu zaid ya mwendelezo ule ule; yaani ubabaishaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…