Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Tatizo hapa sio richmond au makosa yake mengine ya utawala tatizo hapa anadhamira ya kweli ya kuwa kiongozi wa nchi hii?atatufanyia nn watanzania,anayo agenda ya kuingia ikulu au anataka kutimiza ndoto zake tu?kuna mawili kwa EL anataka kuingia ikulu kutimiza ndoto zake za kuwa rais kama alivyo Jk mwisho wa cku yy anatimiza ndoto zake kuliko kutimiza ndoto za watanzania,anataka awe anashuka na ndege kia aje apokelewe na magari 120 vigora kuelekea monduli kwao,ikulu ni mahali patakatifu,hatuhitaji rais aliyewahi kutuhumiwa na rushwa hata ya peni au saa ya mkono,kama ww unaona richmond ndogo kwa taarifa yako ndio imerudisha nyuma maendeleo yetu cos umeme ndio kila kitu kwenye sector za uzalishaji na viwandani
 

Bado mka-mpa uwaziri mkuu!! nyie guys vipi? kwa nini Lowasa peke yake? huwa napata taabu kuona CCM wote wengine ni wasafi!
 

Mtu anadaiwa kuwa mwenye hatia (guilty) inapokuwa proved beyond reasonable doubt kuwa ana hatia bila kujali ana dhambi ngapi, 2namhukumu Lowassa kwa dhambi hyo hyo 1 unayoijua wewe, 2nataka kiongozi atakaye kaa ikilu na ku2ongoza awe msafi, muadilifu, na MTAKATIFU kwa kuwa ikulu ni mahali patakatifu. Na katika kumtafuta, na kuwapima wanaoonyesha nia ya kutaka kutuongoza tutaongozwa na ule usemi wa waroma unaosema CAESAR'S WIFE MUST BE ABOVE SUSPICION..

Aacheni ujinga, acheni kupotosha umma, eti oh kwakuwa Lowassa ni kiongozi asiyeogopa kufanya maamuzi na nch ye2 inahtaji wa2 wa aina hyo na kwa kuwa Hana kashfa nyingne apart from ile ya richmond (sio kwakuwa hana kashfa hata moja!!") basi anafaa kuwa rais!! Hizo ni fikra mgando inazobd zpgwe vita, baba wa Taifa alisha shauri kabla hata lowassa kuhusishwa na ufisadi wowote kuwa HATUFAI, hafai kuwa raisi, aliona mbali. Nyie ni kina nani hasa mpaka mje kumtakasa Lowassa na hatia ya Richmond na kudiriki kunyanyua midomo yenu kusema anatufaa kwa kuwa hajafanya sana ufisadi??? Nani kawaroga vijana wa Tanzania??
 
Kikwete anamuogopa lowassa,akishika madaraka atamfunika,lowassa anataka kuwathibitidhia watz kuwa yeye sio fisadi.
 
Ndugu zangu mtakauka mate mkihubiri. Lowasa na Jk pete na kidole. kumbuka uchaguzi wa 1995!? ukodishaji wa ndege na kadhalika.
Ufisadi wa JK ni sawa na wa Lowasa huwezi kuwatenganisha. Ukitaka uliza utajiri wa Ritz1 na kikwete na masalma!! Kwenye Richmond ni wazi Lowasa ameshasema JK alimkataza wasiishughulikie mapema1. Sitaki na sipendi hawa watenganishwe!!!!!!!!????? mmoja ana mbinu ya kulaghai kwa meno nje mwingine ana uso wa chuma hiyo ndiyo tofauti yao basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 

utajisikiaje ukivaa shati lenye rangi nyeupe sana pamoja na tai pana lakini kifuani ktk shati hilo kuna doa jeusi?
 
Mwalim alikuwa hapendi watu aggressive wanaojitafutia maisha, mwalim mwenyewe aliwahi kutuambia mkapa ni Mr Clean!

Shiiit! Ufisadi kwa tafsiri yako ni kutafuta maisha? Unachekesha!
 
naona jf kuna baadhi ya members wana kampeni za kumsafisha lowasa ...
 

Hutaki kujua fizikia ya unajimu kujua Lowassa siyo Richmond peke yake...hizi hela zimetoka wapi? mfanyakazi wa serikali toka 1989 hadi 1995 tayari milionea (in dollar terms) haingii akilini...hamna mtanzania wa kizazi cha pili (waliozaliwa miaka michache kabla ya uhuru kama akina Lowassa) ambaye anaweza kusema aliachiwa utajiri mkubwa na baba yake..hamna.

ushaidi wa moja kwa moja sina, lakini hii haiwezi kunizuia na kuwazuia watz wengine kumjaji mh Lowassa kama ni mwizi..kumbuka maoni ya jamii hayahitaji ushaidi wa kimahakama na katika siasa haya yanajenga au kuaribu kabisa taswira ya mwanasiasa......wizara ya ardhi lowassa alijitajirisha binafsi kwa deal za viwanja na nyumba za NHC na alimweka rafiki yake Masebu kuwezesha haya....wizara ya mifugo tunajua kuhusu kujimilikisha ranch ya serikali kule Handeni...jengo la umoja vijana je wakati akiwa mlezi wa uVCCM? TRC ilipouzwa mkurugenzi wa PSRC aliwekwa na Lowassa kuhakikisha mgao unaenda vizuri...wengine wataongeza madudu mengine
 
Wengi wa members mnaojitahid kumsafisha EL mlikua humu JF wakat wa saga ya richmond mbona hamkuuliza kuhusu ushahidi na kusema kwamba ni shujaa?acheni unafiki ahiitaji kuwa genius kujua nini kinaendelea!
 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa jana alitoa kile kilichokuwa kikimsibu moyoni mwake kwa muda mrefu na kusema kuwa atashinda vita dhidi yake.

Akitumia vifungu vingi vya Biblia, Lowassa ambaye amekuwa katika misukosuko mingi ya kisiasa tangu alipojiuzulu Februari 2008, alisema kuwa sasa yamekwisha baada ya kuvumilia kwa muda mrefu sana huku akisemwa maneno ya ovyo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Amani mjini hapa.

“Wamesema maneno mengi ya ovyo sana juu yangu lakini nilivumilia siasa hizo kwa kiasi kikubwa sana hadi leo nimesimama katika imani na bila shaka nitashinda,’’ alisema Lowassa na kushangiliwa na umati wa waumini waliohudhuria.
......
Alisema mke wake alichukua Biblia na kusoma katika kitabu cha Isaya sura ya 41 mstari wa 10 na kisha akamtia moyo na kumfanya avumilie kwa kipindi chote cha misukosuko hiyo huku akimuomba Mungu.
.......
Tofauti na alivyokuwa akionekana baada ya kujiuzulu, Lowassa jana alikuwa mwenye furaha zaidi akionyesha ujasiri wakati wote wa shughuli hiyo ya uchangiaji ambayo alisimama kwa zaidi ya saa nne akichangisha fedha za ujenzi wa kanisa hilo....

“Nawashukuru sana mashehe, viongozi wa dini, wana maombi, wake kwa waume, pamoja na viongozi mbalimbali bila ya kuwasahau marafiki zangu ambao kwa namna moja au nyingine walifunga kwa maombi juu yangu, nasema asanteni sana.’’

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Kati, Eliufoo Sima alisema hata kama mawingu yatapita juu ya jua, haina maana kuwa jua limekwisha.
NINAWASILISHA SHUKRANI ZA MH. EL.
 
Kazi ipo na gamba hili....na haya mambo ya kujisafishia uchafu wa 'kisiasa' kwenye majukwaa ya dini mbona yanashamiri sana?! Huyu si alituhumiwa kutaka kumng'oa askofu mkuu wa KKKT Dk Malasusa, sa mbona anajisafishia huko huko na askofu anamfagilia? Dini-Siasa zote viini macho...
 
kule kwenye face buku anajiita Edward Lowasa the next president of united republic of Tanzania
 
Lowasa kakomaa kisiasa anajua nini cha kusema na kwa wakati gani.....haya si maneno yake hata kama ningeamka saa nane usiku ningemkania.Haya ni najungu fitna na umbea,unadhani utarudisha maamuzi kwa majungu haya the train has gone no reverse.

usiwe kama tomaso lowasa kayatamka hayo maneno kwa kimywa chake tena altalen kanisani kuwa amewashinda mahadui zake.jaribu kuwa karibu na vyombo vya habari mkuu.
 
Jembe Lowasa limeshinda vita na mapigano hakuna kama Lowasa nchii hii, big up the next president Lowasa and ur PM Slaa hata Chadema wamekubali LOwasa ni Jembe lenye makali, usiwe na shaka mkuu watanzania wote pamoja na CDM wako pamoja nawe katika harakati zako za kuikomboa Tanzania.
 
mhe. Lowassa ametangaza rasmi ushindi wa kisiasa katika kanisa la kkt singida dhidi ya wabaya wake kisiasa na kusema wameshindwa.

Mi kwa kweli lowassa bado najaribu kutafuta wa kumpambanisha naye uraisi 2015, zaidi ya mhe dr slaa nakosa!

usiwe na wasiwasi fedrick sumaye atamuweza, ni waziri mkuu aliyepandisha uchumi wa nchi
 

Ngamiamzee, hivi umetumwa na hao wakina lowassa au na wewe ni mjinga kama huyo unaemtetea, mwambie Lowassa kama amesingiziwa neno hata moja aende mahakamani ili tujue ukweli, ni mtanzania yupi hawa wa kijijini ambaye hajui kuwa Lowassa ni fisadi na amejilimbikizia mali zisizo na maelezo. kweli Nyerere sio nabii ila ni kiongozi aliyekuwa anaona mbali kwani alimjua Lowassa kabla hata ya wewe kumjua na baada ya kuwa waziri mkuu, bado dhambi zake zilimtafuna na hata akiwa rais bado dhambi zake zitamtafuna tu. ni mungu pekee ndio anajua maisha yetu ya baadae si kwa kulazimisha kwa nguvu ya pesa. atakwenda kwenye makanisa na misikiti yote ila dhambi zake ziko palepale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…