Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

His involuntariness to comment about Dowans raises more questions and indeed it has undone all genuine intents he had.
 
NAPE HABARI NDIYO HIYO -- HOMEWORK KALI.

1. Masuala ya Chama huwa yanaishia kwenye vikao
2. Sijakutana na rais Kikwete barabarani
3. Fedha zipo!
4. miaka bado sana, kwanini tuanze kuongelea urais wa 2015?
5. Mitikisiko ndani ya CCM ni ya muda tu, tutapita katika hali hii.
6. Kuhusu DOWANS - SINA MUDA WA KUJIBU SWALI HILO! (nimependa hii)


 
Sijaona umuhimu wa hii "Press Conference"!

Kama hajajibu kuhusu
1.. Uvuaji Magamba!
2.. DOWANS aka Richmond aka Symbion!
 
Nadhani kuna kitu kazuiliwa. Alikuwa kishakaa ili aanze kuongea mapema, akaondoka ghafla. Yawezekana alipigiwa simu na kupewa maelekezo tofauti? Matarajio ya wengi yalikuwa aongelee masuala mengi, Richmond/Dowans, hali ya usalama a nchi, afya yake (baada ya kudaiwa kuwa alikuwa nje kwa matibabu) n.k

Alichofanya kimenishangaza, not expected at all

Mkuu,

Unaweza kuwa mkweli katika hilo ila pia naona kama hizi strategy za kuelekea 2015. Lowassa ashaona CCM haina tena nguvu kama ilivyokuwa na watanzania wanabadilika (wengi wakiwa ni watu wa uelewa). Ameanza kuuza sera zake za urais kudai pesa zipo, shillingi inaporomoka na inflation juu wakati yeye ni mbunge na mjumbe wa kamati za bunge. Ameshindwa nini kushinikiza wizara anazozisimamia katika kamati kupunguza gharama za uendeshaji wizara? Pia ameshindwa nini kulizungumzia swala la shilingi na inflation bungeni?

Amedai pesa zipo halafu hapo hapo anadai kuwa yeye hana nia ya kumchafua JK . Anapozungumzia kuwa pesa zipo wakati Rais wake anasema hela hakuna siwaelewi wanatupeleka wapi.

Binafsi nasikitika kwa kunipotezea muda wangu kutaka kujua ameongea nini kwani watanzania wana mengi ya kumuuliza atufafanulie kuanzia account zake za nje ya nchi, mali zake, utajiri alionao atupatie maelezo ya kina, Richmond, EPA na uhusika wake yeye na baadhi ya watu wake wa karibu, Alipokuwa waziri wa Ardhi, Maji na kule AICC.

Nilichokiona tu ni kwamba anasema kwa kuwatisha watanzania kuwa yeyote atakayemchafua atampeleka mahakamani. Kauli ni ya kibabe kama public figure you should expect Tanzania ya sasa si kama ya zamani watu watakuchunguza wewe kweli unafaa kutuongoza au unakuja kutuibia. Dr Slaa aliwahi kusema ukituhumiwa basi jibu tuhuma na sio kutisha watu. President Obama wa marekani alituhumiwa kuwa sio mmarekani bali mkenya na pia muislamu na akawajibu with evidence from his birth certificate and church parish membership lakini hatukusikia kafikisha mtu mahakamani kwa kumchafua jina lake. Pengine angelianza na Dr Slaa alimtaja wazi pale Mwembeyanga kuwa ni mmoja wa mafisadi nyangumi nchini.
 
Sijaona jipya alilozungumza. Sasa hapa mtu unashindwa kuelewa kama haya aliyoongea yalihitaji matangazo ya kualika vyombo vya habari kiasi hicho kwamba anataka kutoa ya moyoni!

Labda kwa mbaaali jipya ni habari ya yeye kurudi toka nje ya nchi kutibiwa na kuwasalimia watanzania.

Kukataa maswali magumu ni dalili kwamba hana ujasiri tena wa kuisema serikali ya swahiba wake pamoja na chama chake.

Mambo ya kutokutana na JK barabarani sio habari tumeshamsikia sana. Sasa maajabu tutayaona kesho wale waandishi wa habari walio kwenye payroll yake watakavyompamba!
 
Ngoyai alikuwa anataka kuwasalimu watanzania tu, HAKUNA JIPYA HAPO ZAID YA KUDHIHILISHA UPUPU WAKE, ANATAKA TUJUE KUWA JAPO HAVUMI NA YEYE YUMO.
 
Hii Kauli Lowassa upenda sana kuirudia rudia - Nadhani inamantiki fulani:
Anatafuta umaarufu kwa kupitia kikwete, hata kama hakukutana ma raisi barabarani hiyo haimpi rep ya yeye kuwa raisi wa Tanzania wala kuwaibia watanzania na kuwafanya wajinga kama anavyowafanya J.K.

Tanzania kila kitu kinawezekana, Yaani waandishi wa habari wanatoka sehemu mbalimbali wanaenda kusikiliza pumba za Lowasa, Lowasa kaishiwa na hawezi hata kuona maovu yanayotendeka ndani ya chama chake. Anadai ni mambo ya kawaida na yatatulia ndani ya muda mfupi. Mlevi wa madaraka huyu.
 
Bravo Invisible kwa brekin nyuz,

Huyu Jamaa hakuna alichoongea i concur with you kuwa alichotaka kuongea amekatazwa au labda aliwapiga watu kwara kuwa atamwaga ugali hivyo wamekubaliana nae hivyo kumlazimu kuacha kufanya hivyo.

La Jamaa anatapatapa mambo yamemuwia magumu zaidi hivyo anajaribu kujikosha kiaina kwa bosi wake JK...

Kwa ujumla jamaa Hasomekiiiiiii.............
 
There are currently 523 users browsing this thread. (142 members and 381 guests)

Duh kweli Laigwanani Elowassa kigogo !.
 
Mwandishi wetu pia kamwuliza juu ya 'Uvuaji Gamba', nalo kakataa katakata kuongelea, kasema si wakati muafaka.
Sasa mkuu, huyu bwana amewaita waandishi wa habari ili awaambie wasimfuatefuate na wasiandike kashfa zake??

Zaidi ya kusema atawapeleka waandishi mahakamani, amesema nini zaidi?

NOTHING!!

1) Ugogoro wa UVCCM Arusha - waachwe wenyewe!!.......unaita watu kuwaambia nitazungumzia UVCCm Arusha then unasema waachwe!!?
2) Richmond - unagoma kuongelea chochote - wakati wake bado......Mpaka mtakapolipwa TOZO au?
3) Suluhu ya ajira kwa vijana......kama kweli ana uchungu na issue ya ajira kwa vijana, amefanya nini bungeni - wizara ya kazi na ajira, wizara ya habari......michezo, wizara ya kilimo, wizara ya viwanda na biashara.......AMEFANYA NINI?? Juhudi zake ziko wapi??

NOTHING!
 
There are currently 523 users browsing this thread. (142 members and 381 guests)

Duh kweli Laigwanani Elowassa kigogo !.

Tofauti na Rostam Mkulu huyu hatishiwi Nyau
 
invisible nakuomba ukae uipangilie vizuri hii habari coz haina mwanzo kati na mwisho.au kwasababu ameshamaliza kuongoa mwambie wa jikoni akupe copy ya aliyoyasema naamini kawagawia copy.over
 
Bravo Invisible kwa brekin nyuz,

Huyu Jamaa hakuna alichoongea i concur with you kuwa alichotaka kuongea amekatazwa au labda aliwapiga watu kwara kuwa atamwaga ugali hivyo wamekubaliana nae hivyo kumlazimu kuacha kufanya hivyo.

La Jamaa anatapatapa mambo yamemuwia magumu zaidi hivyo anajaribu kujikosha kiaina kwa bosi wake JK...

Kwa ujumla jamaa Hasomekiiiiiii.............
Hapo kwenye red pana uwezekano mkubwa, hutasikia tena issue ya kuvuana magamba, na unaweza kusikia Nape kapigwa chini uenezi, movie bado linaendelea.
 
Avue gamba aache longolongo.Sasa kama hayuko tayari kutoa majibu ya maswali magumu kawaita wanahabari kupiga porojo?
 
Back
Top Bottom