Its very painful kuona watu tunashabikia hii spinning ya ndugu yetu Mzee Mengi, waandishi wa habari waliojaa urambo walikuwa ni wa IPP MEDIA, bahati mbaya maandamano yakawa a BIG BIG FLOP, ikabidi aite waandishi wa habari nyumbani kwake nidyo aongee na kesho yake akaenda kwenye mkutano wa injili tabora mjini ili anagalau Mengi apate picha zenye umati wa watu. Gazeti la serikali Habari Leo na menigne mawili yalisema masafara ulikuwa na magari mawili urambo.. Inasikitisha na inauma, nilifikiri Sitta ni kipenzi cha wananchi.
Mbona hayo magazeti mengine 2 hujayataja? Magazeti yaliyo report safari hiyo hayakusema kuhusu msafara wa magari mangapi. Wao wali ripoti kwamba alihutubia vijiji 3 njiani akiwa anaelekea Jimboni kwake Urambo. Na alipofika Ndorobo ndipo alipokuta watu wengi wenye pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu, na ikiwa imebaki kilomita moja alishuka kwenye gari na kutembea kwa miguu. Sasa utata uko wapi and where is the BIG BIG FLOP? Kwani wapiga kura wa Sitta wako Tabora Mjini ama wako Urambo Mashariki? Na wewe naona unatuletea spin zako kwa malengo yako.
Kwenye gazeti lao la kiswahili KULIKONI walisema vikao vingne vilifanyika Zanzibar, kwahiyo hapa unaongelea kona zote za nchi, yaani Dodoma, Dsm, Mbeya na Znz, kwa maana hii upinzani wa Spika kwenye chama chake ni mkubwa sana.. tujiulize kwanini? Tusishabikie wamenunuliwa, maana yake ndiyo easy way out siku hizi, huwezi kununua wenzako wenye akili timamu ili waseme ambayo hawayaamini, hata kama ungekuwa Bill Gates.
Kinachoongelewa ni mikutano ya mafisadi katika harakati za kutafuta wajumbe wawaunge mkono kwenye hoja waliyokuwa nayo mafisadi. Unapochanganya wananchi na mikutano ya mafisadi unachanganya mambo na analysis yako inaonekana ni ya kitoto. Kufanyia mikutano kwenye hayo maeneo haimaanishi kwamba watu wa mikoa hiyo ndiyo wanampinga Sitta, bali ni juhudi za kusaka wajumbe wa kuunga mkono hoja!
Halafu hii spinning kusema a reliable source bila kumtaja nidyo yale yale ya kuaminishwa mambo ili wafikishe ujumbe wao, lakini bado hiyo source inasema hana uhakika kama Lowassa na chenge walikuwa na taarifa.. maana yake nini sasa??
Kulikoni au ThisDay siyo gazeti la kwanza kutoa habari ambazo zimetoka kwenye chanzo cha kuaminika ambacho hakisemwi. Vyanzo vya habari hizo vingekuwa vinatajwa iwapo Tanzania tusingekuwa na sheria mbaya ya Magazeti. Pamoja na hayo, mbona RA alipotoa habari kwenye gazeti la Tanzania Daima hakuna aliye-question chanzo cha habari cha Tanzania Daima? Au ni kwa vile Kulikoni na ThisDay ni magazeti ya Mengi ambaye ana ugomvi na RA & Co.?
Yale yale niliyosema ya kununuliwa, kwahiyo mnataka kuniambia Mzee Kingunge alipewa Tsh ngapi?? Alisema Sitta hatufai na arudishe kadi yetu.
Kwani Kingunge ana tofauti gani na RA? Wote ni mafisadi. Kingune is another fisadi na ufisadi wake ni wa moja kwa moja kwa kuwa unahusu familia yake moja kwa moja, biashara za kifisadi za Kingunge zinafanywa na mkewe na wanae. Mkataba wa kwanza unaomgusa Kingunge ni wa pale Ubungo, Stendi ya Mabasi ya kwenda mikoani. Kwa hiyo Kingunge anaweka uzio ili kesho na keshokutwa asije akaguswa kwenye anga zake za ufisadi. Kwa taarifa yako ni kwamba wanaompinga Sitta wako makundi 2, wako wananunuliwa na wako wenye maslahi ya moja kwa moja. Niliwahi kuhoji hapa kwamba ikipelekwa hoja ya ufisadi kwenye Kamati ya Maadili ya CCM, je, Chenge anaweza kuchangia bila kuwa biased? Tayari ana tuhuma nzito na bado miaka yake 10 ya uanasheria mkuu wa serikali ameiingiza nchi kwenye mikataba ya ajabu ajabu sana, hakuna hata mkataba mmoja ambao una nafuu kwa serikali, yote ukiingalia unaweza kujiuliza hivi huyu mwanasheria mkuu ana certificate in law ama ana degree ya sheria kabisa?
What a shame?? Tunasema leo wajumbe walipewa 3M na 5M, mimi ningekuwa mwenyekiti wa CCM ningewa-summon hili gazeti ili wathibitishe, yaani hizo pesa ndiyo za kununua wajumbe wa NEC? Embu haraka haraka jitajie mwenyewe majina ya wajumbe wa NEC wenye shida na 3M - 5M, mpaka wajidhalilishe kuongea jambo ambalo hawaliamini mbele ya umati wote huo.
Kuna wajumbe wa NEC ambao kwao hela yoyote ile inamtosha anachoangalia ni hela tu, wewe ndiyo unaona kwamba milioni 3 au 5 ni kidogo sana, lakini wako walio hongwa hizo na wakaona zinawatosha. Labda nikuulize wewe, wajumbe wengi waliokuwa wakali walikuwa ni kutoka Zanzibar, je, ni kwanini? Ukishatoa jibu la swali kwanini Wazanzibari watetee ufisadi wakati kule kwao kuko safi, ndiyo utaelewa kwamba kuna watu walihongwa hizo milioni 3 au 5.
Wengi wa waliokuwa wanadai kwamba Spika hafai ukiwachunguza kwa ndani wamezungukwa na tuhuma za ufisadi, kwa hiyo wanachohofia wao ni kwamba kama mambo yakiachwa kama yalivyo, basi iko siku na wao wataguswa na kuwekwa kikaangoni. Kama Lowassa alikaangwa na juhudi za kumsafisha zinagonga mwamba, hao wengine watapona? Ukiangalia watu kama Komba wa TOT Plus ana tuhuma za matumizi mabaya na ziko kwa Makamba, Mgeja ana tuhuma za kuifilisi SHIRECU na CCM inajua lakini inafumbia macho.
Jamani vita ya ufisadi ni muhimu kwa taifa lolote, lakini ni muhimu ifanywe bila kuonea watu fulani. Mengi anataka kutuaminisha mafisadi ni hao aliowataja yeye, bahati nzuri tukapewa facts za ufisadi wake na akabatizwa FISADI NYAGUMI, lakini zote hizo ni allegations tu ambazo zimeruhusiwa kwenye vyombo vya habari, lakini hamna mtu mwenye haki ya kumnyooshea mwenzake kidole kumuita fisadi, tusimamie sheria zetu vizuri na haya mambo hayatasumbua, UFISADI sasa hivi unatumika kama kete ya kisiasa kuwashughulikia watu wote waliokuwa karibu na JK tu. Kwa mwendo huu hatutafika popote.
Sentensi ya kwanza ninakuunga mkono, lakini maelezo yanayofuata umechemka na hasa ulivyokuja kumalizia sentensi zako za mwisho. Nina uhakika kwamba kama Mengi angekuwa na tuhuma za ufisadi ambazo zina evidence, siku nyingi sana angeishatinga Kisutu ama Mahakama Kuu, kwani siyo Mengi waliyesema wanatafuta njia ya kummaliza ili kumnyamazisha na hayo mambo yakaishia kimya kimya na waziri aliyehusika na tuhuma hiyo aliingia mitini mpaka leo hii.
Madai kwamba vita ya ufisadi imeelekezwa kwa watu waliokaribu na JK hapo umeenda nje ya mstari kabisa. Kwa hiyo unataka kutumia hiyo kama excuse kwa EL na RA ili wasishambuliwe na ilhali wao ni mafisadi? Serikali ya JK inawaogopa kwa kuwa na JK nae ni mhusika wa some of the deals na ndiyo maana Luhanjo na Rweyemamu walipoona maji yameanza kuzidi unga wakaanza kumtetea boss kwamba hahusiki na Richmond. Pia kitendo cha kutowashughulikia wale wote ambao walihusika na Richmond inaonyesha wazi kwamba kiongozi mkuu wa serikali (JK) ana mkono ama alikuwa na maslahi kwenye hilo deal na sasa mnataka kuanza kutudanganya kwamba vita ya ufisadi inapigwa kwa kuangalia walio karibu na JK.
Wahusika wa Kiwira wako karibu na JK? Wahusika wa TICTS nao wako karibu na JK? Yule aliyekuwa Mh. Balozi wa Italy (Prof Mahalu) nae ni rafiki wa JK? Mzee wa Twin Tower za Benki Bwana Liyumba nae ni best wa JK? Jamani tunapojenga hoja tuje na facts na siyo kutumia mfano mmoja tu ambao unamgusa RA na EL. Yaani hawa mabwana wawili wakiguswa tu serikali nzima na CCM yote matumbo moto na wanakuja juu kama moto wa kifuu kuwatetea kwa nguvu zote mpaka mapovu yanawatoka midomoni. Halafu baada ya hapo utawasikia kwamba kila mtu abebe mzigo wake wa ufisadi individually lakini asihushwe na chama. Ila Sitta akiruhusu mijadala ya ufisadi unaofanywa na hao vigogo kwa kushirikiana na serikali linakuwa ni kosa, what a double standard!