Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Kwa kweli kama ni kwa nia njema, hakuna ubaya kwa Lowassa kuanzisha TV popote iwe Dar ama Arusha. Lakini jambo moja ambalo lazima tuliangalia kwa makini ni kwamba hawa jamaa wamepania kuchukua nchi. Mind you "kuchukua nchi" na hawatanii, mnataka ama hamtaki. Kilichompata Lowassa na wenzake, wameona ni kutokana na nguvu ya media. Wameamua sasa na mumesikia ama kuona, magazeti kibao yakiongozwa na ununuzi wa New Habari. Wamenunua Channel Ten. Hatua itakayofuata na ambayo mchakato umeanza ni kuwadhibiti wamiliki wa vyombo wanavyoona itakuwa kikwazo kwao ikiwamo IPP Media.

Kwa ufupi ni kwamba kama tukiwa makini kidogo tu tutabaini kwamba, Tanzania yetu inaelekea kubaya. Tunajua kila mtu ana haki ya kutawala, lakini si urithi Mwalimu Nyerere aliotuachia kwamba uongozi ni kwa wenye fedha na vizazi vyao. Nawaambia hata ndugu zangu humu (Nawafahamu) ambao wana nia njema ya kuja kuingia katika siasa kihalali (wakiwamo wanaoshabikia EL kuanzisha TV) wajue kwamba bila fedha (za rushwa) hawatashinda kutokana na mfumo uliojikita na unaoendelea kuimarika vinginevyo wawe vibaraka wa wenye fedha. Hii ni HATARI sana na hapa tukijadili mambo tuangalie huko (2010-2020) maana wenzetu wamejipanga hivyo na kwa gharama zozote zile ikibidi hata za HATARI (nitajadili kwa wakati).

Hiyo ni kweli tupu vinginevyo tuna sshabikia kifo chetu.
 
Kwa hiyo bandugu vita ya ufisadi tumemaliza?????????????????????Au tuko wapi tena??????????????? Kama tuna sapoti ufisadi, ufisadi ni ufisadi hata ukija kwa sura ya kuwekeze. KUNA TSHS 185,000,000,000/= (FIGURES ZA KUTISHA) Tanesco inatakiwa kulipa Richmond NO sorry Dowans. Majumba yanazidi kununuliwa Uropa. Sasa kujenga Dar jumba la Tshs 70,000,000,000/= mara kuanzisha TV STATION. Hivi tumelogwa au vipi, sisi tunashabikia tu!!!!!!!!!
TUAMKE SASA TANZANIA INAFILISIWA!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lakini isitangaze Kimasai na isitumike kujisafisha wala kampeni za Urais 2015 vinginevyo itachochea chuki mbaya katika Jamii hatujasahau:A S-alert1:
 
Jamani nazani inabidi Tuanzishe Maombi Special Tumuombe MUNGU wetu Hasiyeshindwa kitu ATUOKOE na hii mipango yao hawa mafisadi wenye tamaa na ulafi na makatili na
 
hili sio jipya kivile anweza afanye tu ne yake hiiiii
 
Hiki kirusi lowasa kikiachwa kianzishe hako ka tv........basi mafisadi papa wenzake km rostam na kikwete watapata nguvu zaidi za kuudsnganya umma............
 
Niliposema mafisadi watashinda.... sikuwa natania.. sisi wengine ni mabingwa wa kulalamika mno; aidha tuwekeze nguvu zetu kwenye urithi wetu au tuwaache watutawale wapendavyo!

MMKj
Amini hatuhitaji nguvu zetu ziende kwenye urithi wetu(rasilimali) labda kama nimekuelewa visivyo.

Kwa Mtazamo wangu kwa sasa kuliko kipindi kingine tunafaa toka level ya familia hasa wale wenye uchungu na Nchi yao au hali halisi jinsi nchi inavyoendeshwa kama nionavyoo humu JF michango mingi yenye kukemea maofu , basi wasisite kuilisha au kuiasa familia zao ili huko mbele tuendako tuwe na Kizazi chenye kutenda haki na kuchukia ufisadi kwa hali yoyote.(Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo)
 
Hivi sasa, jinamizi linalotukabili si ufisadi peke yake, bali pia umiliki-binafsi wa Taifa la Tanzania (private ownership of the country) na kikundi hiki kidogo cha mafisadi, kinachodhaniwa kutozidi 10. Hawa si wajasiriamali au wafanya biashara wa namna yeyote, bali ni kikundi cha uhalifu, ambacho si ajabu kikawa na ushirikiano na vikundi vya namna hiyo nje ya nchi. Mwishoni, wananchi watashinda kukithibiti (na kukiwajibisha kisheria), kwa maana haki itasimama dhidi ya uonevu.
Television kwenye siasa zinalipa sana
 
Naona sasa ni wakati wetu wana JF kuangalia nini cha kuifanyia nchi yetu....

hawa mafisadi muda wako ukifika watalipa na watarudisha vitu vyote walivyoiba....

tukijipanga na kuwa na msimamo mmoja Tanzania itakuwa nchi tajiri ya watu wote na ya kujivunia.
 
Kuna taarifa kuwa upande wa Radio, kuna uplinks kwa baadhi ya mikoa tayari.
 
it can be done play your part. nchi imepotea mafisadi wanafanya wanachokitaka, nini kuanzisha tv na redio wakitaka kufanya chochote. tuamke watanzania tukatae udhalimu
 
kwani kuna tatizo gani EL kuhitaji uongozi wa juu wa taifa letuu?? kama anazo sifa za kutushawishi basi tukimkubalia ni haki yake kidemokrsia. tuache personality katika kujadili hojaaaa...Rushwa ndo msingi wa CCM kututawalaaa sasa kama wachagua watu fulani fulani tuuu kwa hisia zako bado hujengi hoja endelevu...

afterall EL is better than current boss in vision, thinking, implimentation and decsion. achilia mbali intelligence level.

Hoja yako natumaini haina maana hakuna watanzania wengine ambao wana upeo, fikra, utendaji maamuzi na akili kuliko hao akina EL. Ebu nijaribu kueleza. Hapa kwetu vichujio vya watu waadilifu, bora wajuzi wenye upeo nk vilikwisha badilishwa kwa ujambazi wa CCM kukumbatiana na kukuazimia kuwa wao ndio kila kitu na si watanzania wote. Nina maana genge(watu 10 tu) lilishajisimika, kujikita na kubinafsisha nchi.

Kwa bahati sasa wananchi wanafumbua macho wanaona rasilimali zao ziiile na mafisadi. Wanajikuta hata taratibu za kudai chao zimeingia virusi. Fisadi ni hasidi, hana huruma mwizi ambaye anataka kukugawia alichokuibia. Jitihada zo zote za EL, JK, RA, AC na vizazi vyao havina nia njema na wananchi. USISAHAU HATA KODI INAYOLIPWA NA WANANCHI WOTE KWA KUPENDA AU LAZIMA HAWALIPI. Kwangu mimi nashukuru udhalimu wao kutufungua macho; ila baada ya kuona tupinge jitihada zao zote, tupiganie cha kwetu kwa silaha zilizo ndani ya uwezo wetu WOTE.
 
Kuanzisha Radio siyo jambo la ajabu kila MTZ yuko huru kuanzisha chombo cha habari kulingana na uwezo wake. Tukumbuke hizo ni moja ya kuchangia ahadi za CCM kutoa ajira kwa WATZ mie nina rafiki zangu wanafanya kazi AFRITEL, wanasema maslahi ni mazuri sana, BIG UP LOWASA FAMILY
 
nyinyi watanzania mna laana, na hamuendi popote, Lowassa hajawahi kuiba hata Pipi, alikuwa kiongozi pekee mkali kwelikweli na hana huruma wa uoga kwa vitambi au vigogo, bila kiongozi kama huyu hamna maendeleo africa hasa Tanzania, viongozi wetu asubuhi badala ya kuwa na tumbojoto ya majukumu yetu, wana tumbojoto baada ya kuvimbiwa chai heavy, na mda si mrefu lunch babkubwa na ....
Lowassa asiwekeze kwenye Media? awekeze mkenya au mhindi ndio mtafurahi? au mnapenda kuangalia CNN ya bwana R. Madorck? au mnapenda tuendelee kubembelezewa ujinga na mambo kidini yaliyopitwa na wakati na hako ka TBC ambocho kinasababisha watanzania wengi kupenda kuangalia channel za kigeni? haya tv hamtaki, akilima? akijenga? akiendelea na siasa na hatimae kuwa rais na mnajua atashinda tu akiamua? au auwawe ili asisahaulike kama kaka yake na jirani yake aliyemwachia kiti cha ubunge Monduli? angekuwa si msafi jimboni kwake yangetokea haya maajabu ya Loliondo? poleni watanzania, kama vipi wapeni wazenji nafasi japo wajaribu bila umbea wenu, wao walimpenda sana Lowassa, na alikuwa akiwatembelea kila miezi kadhaa, naona Pinda hatii mguu Zenji? sijui anaogopa popobawa?
 
Hiyo ni kweli tupu vinginevyo tuna sshabikia kifo chetu.

Aisee hata mimi nakuunga mkono kwa familia ya L. kumilikia kituo cha Television ila iwe ni kwa manufaa ya watanzania yaani kutujuza yaliyoyakweli na si propaganda. Hakuna shida yeyote kwani nae ni Mtz kama wengine na cc tunafurahia kuwa na channel nyingi hivyo na ushindani utakuwa ni mzuri.
 
Ukisema L ni msafi wewe ni nani unaejaribu kumsafisha mwana wa Adam? Ni Mungu pekee ndiye mwenye uwezo huo wa kumjua aliye msafi na mchafu, na jua ya kwamba L ni Mtz na anahaki kama Mtz mwingine yeyote yule ya kuwekeza ila nami nitawashangaa wale wanaopinga uwekezaji wake. Na maajabu ya Loliondo si kwa ajili ya usafi wa L, na lile c jimbo lake. Nami namkubali kwamba L ni mchapa kazi kweli kweli lkn huenda humo humo ndio anapitia katika kukwapua tutajua?
 
Back
Top Bottom