Lowassa kupigiwa saluti ni sawa?

Lowassa kupigiwa saluti ni sawa?

mkuu FMES heshima mbele.
Yote unayoongea inawezekana ni kweli kabisa ila hili la salute ndo kuna kosa kidogo.Kama uliona Mwanajeshi anampigia salute mbunge inawezekana mbunge huyo alikwahi kuwa mwanajeshi na kma uliona kwenye harusi mwanajeshi anamsalute sijui nani inawezekana kati ya waliokuwa hapo harusini alikuwepo mwanajeshi wa cheo karibu na wewe hukuweza kumwona.

Mwanajeshi kupiga salute kwenye bunge siyo kuwa anampigia mbunge bali huwa ni ku-salute proceedings ile ambayo ipo na picha ya rais mle ndani.Siyo Bungeni tuu,hata mahakamani hata mahakama ya mwanzo mwanajeshi anapiga salute kabla ya kukaa mara tu aingiapo.Hii haimaanishi kuwa mahakimu wote hadi wa mahakama ya mwanzo hupigiwa salute na wanajeshi bali wanajeshi huwa wanasalute proceedings ile iliyopo huku pia kukiwa na picha ya rais.

Mwisho kabisa tukumbuke kuwa wanajeshi hupigia salute maiti zote mara zipitapo no matter what.Hata kama maiti hiyo ilikuwa ya jambazi.Kwa hiyo mimi Lowassa kupigiwa salute means nothing.
habari ndo hiyo

Nimekusikia mkuu na sina la kuongeza isipokuwa in this process tusije tukasahau kuwa Lowassa bado ni mbunge wa kuchaguliwa,

Hayo yako mengine sina uhaklika kabisaaa na kinachosemwa lakini nitatoa pass!
 
Nimekusikia mkuu na sina la kuongeza isipokuwa in this process tusije tukasahau kuwa Lowassa bado ni mbunge wa kuchaguliwa,
Hayo yako mengine sina uhaklika kabisaaa na kinachosemwa lakini nitatoa pass!
[/QUOTE


Mkuu,
Kama suala ni salute,ubunge wa kuchaguliwa kwa sasa siyo issue.Hao hawapigiwi salute,angekuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais ungeweza`kuwepo huo mkanganyiko wa salute kwani post zote za kuteuliwa na rais wanajeshi utakiwa kusalute huku protokali ikizingatiwa/vyeo/u-senior.
 
EL ni Waziri Mkuu mstaafu na Mhe, Mbunge hivyo saluti ni halali yake. Hata kama ingekuwa si halali bado anaheshimika,

Anao ulinzi na mafao yake yote stahili. Kama Seif Shariff amerejeshewa mafao, gari na ulinzi itakuwa EL!?.

Hilo la safari must be unfortunate incident. Kwa mujibu wa mafao yao, analipiwa safari 4 za nje ya nchi zaidi ya hapo anajigharimia.
Kutopokelewa was just a miscomunication issue. In 1996 nilibahatika kusafiri ndege moja na Mhe. Sumaye akiwa PM. Kufika airport alishuka hakukuta mapokezi ya aina yoyote hivyo yeye na timu yake tulichanganyika wote kupanda lile basi la abiria la airport ambalo halina viti,
alisimama na alishika mchuma! Huku walinzi wakihaha kujaribu kumkingia asisukumwe sukumwe.

1998 nikiwa Upsala Universty ya Sweeden, Mhe. Ben Mkapa
Akiwa rais, aliwasili kwa bus kutembelea chuo. Wakati akiondoka alipanda tena basi na akina sisi kujikuta tuko basi moja na rais wetu(hakushika mchuma) kitu ambacho kwa TZ ni aghlab sana.
 
EL ni Waziri Mkuu mstaafu na Mhe, Mbunge hivyo saluti ni halali yake. Hata kama ingekuwa si halali bado anaheshimika,

saluti anapigiwa kwa sababu ya kuwa mbunge, period hakuna askari wa aina yoyote wa Tanzania,anayeweza kumpita mbunge bila kutoa heshima ikiwa ni saluti au kukunja mikono huo utakwua ni utovu wa nidhamu wka kiongozi wa taifa, akionekana na mkuu anayemzidi cheo huko aliko ni adhabu nzito sana dhidi ya yule askari.

Anao ulinzi na mafao yake yote stahili. Kama Seif Shariff amerejeshewa mafao, gari na ulinzi itakuwa EL!?.

Maalim Seif, hakuiba au kutoka kwa rushwa na pia kupewa kwake mafao ilikuwa ni part ya kukamilisha muafaka, hiyo ni tofauti na Lowassa alitoka kwa rushwa na ufisadi, kwenye kitabu cha wastaafu category yake haipo, lakini ya Seif ipo.

Hilo la safari must be unfortunate incident. Kwa mujibu wa mafao yao, analipiwa safari 4 za nje ya nchi zaidi ya hapo anajigharimia.
Kutopokelewa was just a miscomunication issue.

Serikali hai-operate this way hata siku moja inapokuja usalama wa mawaziri wakuu wastaafu na viongozi wa juu, kama hii ingekwua kweli angefukuzwa mtu kazi huko kunakohusika, just impossible bro!

In 1996 nilibahatika kusafiri ndege moja na Mhe. Sumaye akiwa PM. Kufika airport alishuka hakukuta mapokezi ya aina yoyote hivyo yeye na timu yake tulichanganyika wote kupanda lile basi la abiria la airport ambalo halina viti,
alisimama na alishika mchuma! Huku walinzi wakihaha kujaribu kumkingia asisukumwe sukumwe.

A sitting Prime Minister alikutwa na haya? Mkuu naona niwaachie wananchi waamue ukweli wa hii hoja ila mimi simo!

1998 nikiwa Upsala Universty ya Sweeden, Mhe. Ben Mkapa
Akiwa rais, aliwasili kwa bus kutembelea chuo. Wakati akiondoka alipanda tena basi na akina sisi kujikuta tuko basi moja na rais wetu(hakushika mchuma) kitu ambacho kwa TZ ni aghlab sana.

A sitting president alikutwa na haya, naona nijitoe sasa kwenye huu mjadala maana this is incredible bro! Isipokuwa siku Kawawa, Msuya, Malecela, Warioba na Salim wakikutwa na haya ya kutokuwepo mapokezi wanaposaifir naomba unifahamishe nitaamini maneno yako!
 
Wanajeshi wanapoingia ndani ya bunge ni lazima wapige saluti anyways na kutoa kofia, ambayo wanaweza kuirudisha baadaye,

mbunge ni kiongozi wa taifa anayestahili saluti ya kijeshi, vipi wakuu hatukupitia JKT nini?

Hivi kumbe wabunge wanapigiwa salute. Asante kwa kutufahamisha maana wengine tulipitia JKT miaka ya 47.

Kama kuna muheshiwa rais, inakuwaje naye mbunge anapigiwa salute?
 
Wabunge wanapigiwa saluti period, nikiwa JKT Oljoro mbunge Ole alikwua akija mara kwa mara pale, na CO mwenyewe Mnauye alikwua akimpigia saluti akwia na uniform, na akiwa na nguo za nyumbani alikuwa akibana mikono, there is no way askari wa jeshi lolote la Tanzania, anaweza kumpita mbunge bila kutoa heshima ya kijeshi,

Halafu vipi ni wapi ulimuona Lowassa akipewa heshima zote kama ulivyodai mwanzoni mkuu? Maana mimi nimemuona majuzi na hakupewa kabisaa! na ilikuwa aibu kubwa kwa wote waliokuwepo!
 
Na huko kumsalute m-bunge ni sheria au mazoea tu?
 
not certain. EL hastahili if salute to MP is not lawful
 
Kuna vyeo ndani ya system hupaswa kupigiwa saluti.......absolutely PM ikiwa ni mojawapo ya hivyo vyeo.

1.Hebu tujiulize.........kwa mfano Brigedia......akijiuzulu/resign......je ataendelea kupigiwa saluti?.....binafsi nimeshuhudia hata wale walioachishwa kazi......wakipigiwa saluti....is this a confusion or what?..........Philemon please enlighten us.......

2.Kitu kingine ...........je wanaopigiwa saluti.........ambao si wanajeshi huelekezwa jinsi ya kujibu?.........
 
.......MP Ole (sijui ndio yule aliyekuwa mwanajeshi pia.....Kapteni).........Nnauye naye alikuwa kanali wa jeshi......!!...im still confused!!
 
Ukiondoa saluti za ndani ya MAJESHI, saluti zingine ni kwa WATEULE wa RAIS( anaowaapisha). Huku kungine saluti zinatolewa kwa matukio maalum kama kwenye mazishi.
 
Ukiondoa saluti za MAJESHINI, saluti nyingine zinatolewa kwa WATEULE wa Rais (wale anaowaapisha). Huku kungine zinatolewa kwenye matukio maalum kama maziko na sherehe za kitaifa. Hayo ya Wabunge tuwaachie hao walioyashuhudia harusini,...
 
Kisheria wabunge hawapaswi kupigiwa saluti. Na kama hiyo inafanyika ni makosa au mazoea ambayo yamefanywa kuwa ni kawaida. Isipokuwa, kuna exceptional cases ambapo mbuge ni afisa mstaafu wa jeshi. Kawaida maafisa wastaafu hubaki na vyeo vyao. Wanachopumzika ni utumishi katika jeshi, na ndo maana wanakuwa kwenye "reserve army", akiitwa kama kuna dharura ya vita anarudi kutumika akiwa na cheo kile alichokuwa nacho wakati anastaafu kwa hiyo akikutana na afisa ambaye bado yuko in-service, kwa kuzingatia seniority, atapigiwa saruti. Viongozi wa serikali wanaopigiwa saruti na wanajeshi ni hawa wafuatao
1. Rais na amiri jeshi mkuu
2. Makamu wa Rais
3. Waziri Mkuu
4. Mawaziri wote wa serikali
5. Wakuu wa mikoa
6. Wakuu wa wilaya
7. IGP (Hapa ni kutegemeana na seniority ya vyeo katika jeshi, NCOs wanampigia saluti IPP na Commissioned Officers to the rank of Junior Officers (Luteni-Usu hadi Major (sina uhakika sana).
8. Mawaziri wakuu wastaafu (?), Rais Mstaafu, Makamo wa rais mstaafu.
9. Retired CDF na Maafisa wote wastaafu kwa seniority ya vyeo vyao walivyokuwa navyo.
10. Maiti (Maiti au Marehemu hupigiwa saluti na askari wote bila kujali cheo alichokuwa nacho), hii kwa taratibu za kijeshi.
11. Chief Justice (Hapa sina hakika kama naye anapigiwa saluti), ila polisi humpigia.
12. Mahakamani na Bungeni askari hupiga saruti kwa sababu ya "coat of arms" ya serikali inayokuwemo ndani ya Bunge na Mahakamani.

Kwa hiyo wabunge si miongoni mwa wanaopigiwa saluti, isipokuwa tu pale huyo mbunge ni afisa mstaafu wa jeshi.

Nadhani wengine pia wenye kukumbuka haya mambo tuelimishane. Naamini wale tuliopita JKT bado tunayo kumbukumbu. Niko tayari kusahihishwa kama kuna mahali kuna makosa.
 
Ulichokiacha hapo labda ni BENDERA na WIMBO wa TAIFA unapopigwa.
 
Hapana Ole aliyekuja kuwa waziri wa utalii sidhani kama aliwahi kuwa soldier, I rest my case, maana sioni logic wala facts zaidi tu ya majina kubadilishwa na hoja zile zile,

Na siwezi ku-betray what I have seen, kwamba ati askari wa JKT hakuwahi kutoa heshima ya either kubana mikono au kupiga saluti mbele ya mbunge, labda by the time sisi tunaenda huko sheria zilikuwa zimebadilishwa, lakini mimi nikiwa huko OP Tekeleza tulifundishwa kutoa heshima kwa viongozi wa tauifa kuanzia wabunge.

sijawahi kutaka kujua kama ni sheria au heshima, lakini siku zote ninaona wabunge akipewa slauti au kubaniwa mikono na askari, wa aina zote bongo, askari mwenye ubavu wa kutotoa heshima wka mbunge bado sijamuona, lakini huenda kuna walioona siwezi kubuisha kwenye hilo. na nimeona kuanzia kwenye harusi, kwenye mageti ya jeshi hasa Airport kwenye njia ya ndege za serikali, nimeona kwenye masherehe pia.

Yaani DC anaweza kuwa na ubavu kuliko mbunge that is wasup? RC sio mbunge? Again nikiona hoja nzito nitarudi tena, later!
Ahsante wakuu.
 
Kwa hiyo wabunge si miongoni mwa wanaopigiwa saluti, isipokuwa tu pale huyo mbunge ni afisa mstaafu wa jeshi.

Kwa hiyo mkuu wanapigia maiti lakini sio wabunge? that is wasup bro!
 
Kwa hiyo mkuu wanapigia maiti lakini sio wabunge? that is wasup bro!

WABUNGE HAWAPIGIWI SALUTE,NA KAMWE SIYO SHERIA KWA MBUNGE KUPIGIWA SALUTI labda kama aliwahi kuwa mjeshi.kuhusu maiti,acha wanajeshi kuipigia salute hata rais mwenyewe wa nchi anaitolea heshima.Siyo kama ni nini bali ni kuonyesha unyenyekevu tu.

Aliyosema Ngereja hapo juu ni sawa kabisa.Mimi nimewahi kuona wabunge wengi tu wakiwa na askari na sijawahi kuona askari wakiwapigia salute.Ieleweke pia kuwa salute ni salamu.Inawezekana mkuu FMES uliona wale askari wenye mazoea ya kupiga piga salute wakimaanisha salamu kwao wakifanya hivyo.Pia inawezekana kabisa kuwa labda unapoona mbunge yupo mahali fulni huwa kuna skari mwingine alievaa kiraia na wewe humjui so askari huyo kwa vile anamjua akampigia salute wewe ukafikiri kapigiwa mbunge kwa sababu unamfahamu.

Wakati Simon Dau akiwa RPC singida na cheo cha ACP hakuwahi kumpigia salute Kandoro akiwa DC singida.Lakini alipokuja Bachubira akiwa na cheo hicho hicho alikuwa anampigia DC salute.Bachubira alikuwa anawapigia salute hadi watendaji wa kata.Yeye alikuwa anatafasiri kama salamu tu.So utaona hapo ninapomaanisha kuwa sometimes maaskari huchukulia salute kama salamu tu.
TAHADHARI ni kuwa askari kwa askari siyo rahisi kutafasiri salute kama salamu wao hufuata seniority sana na order of command.Nitatoa mfano mwingine kuwa akiwapo Bachubira hapo singida alikuwa anam-salute RSO na cheo hicho hicho lakini alipokuja Mselemi alikuwa ham-salute RSO japo cheo kilikuwa hicho hicho.Hii ni kwa sababu ya seniority yao.

Vile vile mimi nikiwa JKT tulikuwa tuna mtindo fulani wa kudanganyia wasichana.Tulikuwa tunawadanganya kuwa mimi ni mkubwa kwa cheo kuliko ofisa fulani ama nafanya kazi fulani kubwa na ofisa wa jeshi lazima anipigie salute.Sasa tulichokuwa tunakifanya ni kuw,mara tu tukiwaona maafisa wa jeshi wakiwa na uniform,sisi tunajipitisha na kubana mikono.Kwa vile mimi nikinza kubana mikono kujibiwa kwangu na afisa huyo ni lazima ajibu kwa salute,so raia wakawa wanaamini kuwa sisi tuna vyeo kuliko wale maafisa wa jeshi.Labda mkuu FMES aliona mchezo huo na bado watu wanauendeleza huko jeshini akafikiri mbunge kapigiwa salute.Hahahahahaha
 
Kwa hiyo mkuu wanapigia maiti lakini sio wabunge? that is wasup bro!

Ni kweli kabisa, maiti wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa ajili ya kuzikwa hupigiwa saluti. Na kwa mfano askari yeyote jeshini akifa, wakati wa kutoa heshima askari wote bila kujali vyeo vyao hupiga saluti kama heshima. Hapa nina maana hata CDF atapigia saluti maiti ya askari mwenye cheo cha Koplo.
Kumbuka kijeshi, maiti hupewa heshima zote za kijeshi.
 
Wanajeshi wanapoingia ndani ya bunge ni lazima wapige saluti anyways na kutoa kofia, ambayo wanaweza kuirudisha baadaye,

mbunge ni kiongozi wa taifa anayestahili saluti ya kijeshi, vipi wakuu hatukupitia JKT nini?

Actually kaka kuna wakati wabunge walijisimika rasmi uheshimiwa huu kwa kuingiza haki ya wao kupigiwa saluti na kupepersusha bendera katika sheria za nchi....

Hivyo as long as LOWASSA anaendelea kuwa MHESHIMIWA SANA Mbunge wa Monduli ni wazi anapaswa kupigiwa salute na askari wetu walioapa kiapo cha utii.....

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom