Hongereni wale mlioshinda kule Dodoma, lakini pia poleni sana WANA WA EMAMNUEL NCHIMBI, KINGUNGE NGOMBALE MWIRU, SOFIA SIMBA NA ADAM KIMBISA.Faida za kuwa maarufu wa asili na maarufu wa kutengeneza zimejidhihirisha kwa kile kilichotokea Dodoma. Ni matokeo ya kuwa na hamu ya kweli ya kuwatumikia wananchi na hamu ya kutengeneza ambayo hapana shaka huambatana na matamanio ya kupita kiasi ya madaraka.
Nudgu zangu kuna taarifa ya kuwepo kwa Mkutano baina ya Edward Ngoyai Lowassa na wana Habari, nia na madhumuni kwa mujibu wa chanzo cha habari ni Lowassa kutaka kufukisha ujumbe kwa wafuasi wake kile anachodhani ni kutotendewa haki na vikao vilivyompa ushindi John Pombe Maghufuli kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM hapo mwezi Oktoba, 2015.*
Maswali yangu kwa Lowassa ni machache tu, anishawishi labda mimi na hata wengine ambao wanataka kuaminishwa kuwa bila Lowassa mchakato ule haukuwa na maana.
1. Lowassa anataka kutuambia kwamba Vikao vilivyofikia uamuzi wa John Pombe Maghufuli kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM si halali?
2.Kati ya Wagombea 37 walioachwa wakiwemo Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri Mkuu mstaafu(siyo aliyejiuzulu), Fredrick Tluway Sumaye, yeye ndiye alikuwa na sifa zote kwa maana ya uadilifu, uzoefu ndani ya chama na mwenye kuweka maslahi ya Chama na Taifa mbele kwanza na siyo maslahi binafsi kuliko wenzake?
3. Ni ukweli usiopingika kwamba Lowassa ndiye aliyetumia pesa nyingi kwenye mchakato huu kuliko wagombea wenzake inawezekana kabisa kiasi alichotumia kikawa zaidi ya mara 50 ya kiasi alichotumia John Pombe Maghufuli. Je hilo ndilo tatizo?
4. Haya yaliyotokea yalisha wakuta aliyekiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi kuru za Afrika, OAU wakati huo, Dr. Salim Ahamed Salim, Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee john Samwel Malecela na hata Rais wa Sasa Jakaya Mrisho Kikwete. NIni cha ziada alichokuwa nacho Lowassa mpaka aanze kulalamika tofauti na waliomtangulia ambao kimsingi waliona CCM ni taasisi na siyo mali ya mtu na hivyo busara ikatawala na maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla vikatawala? Lowassa ni mwadilifu, ni mchapakazi kuliko hao wazee, enzi za utumishi wao?
Lowassa aache kutudanganya bwana, angekuwa msafi kiasi hicho angekuwa lulu kwa wapinzani, kwa Chadema ambao kwenye Orodha ya Mafisadi walioisoma pale Mwembe Yanga jina lake limo au hata ACT ambako kauli mbiu yao ni "MUHIMU SIYO MADARAKA, BALI UZALENDO", Chama ambacho sharti moja wapo la kuwa mwanachama wake ni lazima ukataje mali ulizo nazo, LOWASSA atatumia siku ngapi kutaja mali zake ili awe na uhalali wa kuwa mwanachama wa kweli wa ACT kama kweli wanamaanisha? Mrema ni mfano mzuri wa mwadilifu aliyetoka CCM kwenda NCCR tukaona athari zake kwa CCM na siyo Lowassa ambaye ameanza kwanza na kupoteza kabisa Kauli mbiu ya baadhi ya vyama kwa kufadhili mikutano ikiwa ni hatua ya kujitengenezea mazingira ya kukubalika lakini baada kuyafunika macho ya viongozi wa vyama hivyo kwa UTANDO wa buibui ili wasahau kuwa nao walikuwa wapingaji wakubwa wa ufisadi wake huko nyuma.